Serikali yashindwa kumsomea mashtaka 'malkia wa meno ya tembo'

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961
Kesi dhidi ya mwanamke Mchina ambaye anatuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa pembe za ndovu kutoka Tanzania imeahirishwa tena.

Kesi hiyo dhidi ya Yang Fenglan, maarufu kama ‘Malkia wa Pembe’ imeahirishwa hadi tarehe 6 Juni.

Upande wa mashtaka uliambia mahakama kwamba faili ya kesi hiyo bado imo mikononi mwa afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma.

Maafisa hao wameambia mahakama kwamba wanatarajia kuipata faili hiyo kabla ya tarehe 6 mwezi Juni.

Kesi hiyo ilikuwa awali imetarajiwa kuanza Dar es Salaam tarehe 9 Mei lakini ikaahirishwa kwa wiki mbili.

Yang, 66, anatuhumiwa kuongoza kundi la walanguzi waliohusika kusafirisha pembe karibu 700 za ndovu za thamani ya $2.5m (£1.7m) kutoka Tanzania hadi mataifa ya Mashariki ya Mbali.
 
Kwa Dalili Hizo za Kuhangaika na Mafaili Tena Ndani ya Ofisi ya Serikali, Malkia Ameshashinda Kesi.
kwa nionavyo hapa, upelelezi upo shaky, na kesi wanaweza wakashinda, kwa hiyo kuzubaisha zubaisha huko ni ku buy time kwa upande wa serikali kujipanga zaidi
 
hawa wachina weeengi wanafanya mambo batili humu ndani ya hii nji ikiwemo kutuuzia masimu fake eti wawekezaji wa icecream ifike mahali warejeshwe makwao
 
Hivi kuficha uso mahakamani inaruhusiwa kisheria? hakimu anajuaje kuwa anayemsomea mashitaka ndo huyo? msaada tafadhali
 
Wapu


Wapuuzi tena wana dhalau sana, akili zao wanafikiri waswahili hatuna akili.
kabisaa wengi wanaishi kinyume cha sheria

wana maviwanda yanatitririrsha maji taka mitaani wananyanyasa wafanyakazi wao yaani wafanyakazi wako katika hali hatarishi ya afya zao
wengi wanazuga kuwa wawekezaji kumbe wanalia mingo nyara za serikali..... ni viumbe hatari ukifika kariakoo utadhani upo uchinani wanasukuma matoroli kule balaa yaani sijui km serikali inawaafwatiliaga
 
Back
Top Bottom