Serikali yashauriwa kushughulikia tatizo la utoroshwaji fedha


R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Messages
6,294
Points
2,000
R.B

R.B

JF-Expert Member
Joined May 10, 2012
6,294 2,000
SERIKALI imeshauriwa kushughulikia tatizo la utoroshwaji wa fedha na upotevu wa mapato ya kodi, kwa namna ya dharura na kuwachukulia hatua wahusika. Ushauri huo ulitolewa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki (EASTC), Camillus Kassala, alipoendesha mdahalo uliohusu Utoroshaji wa Fedha na Maficho ya Kodi Kimataifa.

Alisema kwa takriban kipindi cha miaka 10, suala la ukwepaji kodi unaofanywa na baadhi ya kampuni za kimataifa na kutorosha fedha katika maficho ya kodi, limekuwa likizungumzwa na limeshamiri zaidi barani Afrika.

Alisema suala hilo limepewa kipaumbele katika mijadala ya kimataifa kuhusu maendeleo ya Afrika, lakini pia ni kiini cha majadiliano kuhusu mitaji au fedha kwa ajili ya maendeleo.

“Inasemakana kuwa, kuna utoroshwaji wa mitaji kwa njia za kukwepa kodi kutoka nchi masikini, ambapo mitaji hiyo hufichwa katika nchi mbalimbali duniani ambazo kampuni husika hufanya biashara au shughuli za kiuchumi.

“Shughuli hizo ni pamoja na uchimbaji wa madini, dawa za kulevya, usafirishaji wa nguvu kazi za binadamu katika biashara ya utumwa na ukahaba,” alisema Kassala.

Alisema kwa maelezo hayo ambayo yalitokana na utafiti wa awali uliofanyika kwa njia ya hojaji, taarifa za Benki ya Dunia (WB) na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), imeweza kutoa dhana ya utoroshaji mitaji na maficho ya kodi ilivyo.

Alisema katika biashara au shughuli za kiuchumi za kimataifa, hususan zinazotumia maliasili kama madini, misitu, wanyama pori na kilimo kikubwa kutoka nchi masikini, kampuni mengi hutumia mbinu za kutorosha fedha kwa ajili ya kuficha mapato.

“Njia ya kuepuka kulipa kodi inakubalika ni halali, lakini kukwepa kulipa kodi haikubaliki kisheria na ni haramu katika nchi zote zenye mfumo wa utawala wa sheria ulio bora na unao walazimu wafanyabiashara na shughuli nyingine za uchumi kulipa kodi,” alisema Kassala.

Aidha, alizitaja baadhi ya athari zinazotokana na utoroshwaji wa mitaji katika maficho ya kodi ni pamoja na kuhujumu mifumo ya kodi ya fedha za umma na kuongeza mgao wa mapato ya kodi usiokuwa wa haki.

Alisema Serikali inatakiwa kuwa na sera za nchi za maendeleo, uwazi katika masuala ya fedha na hesabu zake na kuhusu mikataba ya kodi.

“Kunatakiwa kuwe na ushauri wa wanataaluma katika masuala ya nchi na kuhusu upangaji wa bei za rasilimali na kodi zinazotozwa, kwa ajili ya kuweza kupunguza na kutatua tatizo hili nchini,” alisema Kassala.
 

Forum statistics

Threads 1,284,539
Members 494,169
Posts 30,831,030
Top