Serikali yashangaa gesi ya kupikia kupanda bei, yataka viwanda vieleze sababu ya ongezeko hilo

Serikali imesema viwanda vya gesi ya kupikia havijafata utaratibu katika kupandisha bei hivyo bei mpya hazitambuliki.

Afisa wa Ewura mr Kaguo amesema viwanda vya gesi vimetakiwa vipeleke vigezo vya kupandisha bei na serikali ama itavibariki na kukubali bei mpya ama itavikataa kama havijitoshelezi.

Hata tozo serikali inashangaa pia
 
Sasa wao wakishangaa sie tufanye nini, nchi ya maajabu hii na viongozi wake
 
Inahitaji tone Moja tu la akili kutambua sababu za kupanda bei ya bidhaa. Tozo za kijinga Kila mahali zinapunguza mzunguko wa pesa. Kwa bahati mbaya tuliopo kitaa tuna mawazo mazuri ya maendeleo lakini walio na wadhifa na nafasi ya maamuzi, hawawazi lolote zaidi ya kulinda nafasi zao watawale milele
Wanapokea mishahara mikubwa na marupurupu kibao changanya na rushwa mkuu watakukumbuka wewe mzee wa kajamba nani?
 
Wananchi wanashangaa na serikali inashangaa maajabu

Halafu kuna watu wanasema siasa haina maana

Nasubiri kuona wapinzani wakiumia kwa hili swala.
Wapinzani wenyewe sijui wanapewaga mlungula wanatulia, tusiokuwa wanasiasa ndiyo tunaumiaga zaidi
 
Angalia kwenye mafuta ya kula, sukari kila mtu anaongea lake kama mazombi, aliyeturoga kajifukia kichwa huku makalio yakiwa juu kama mbuni, sasa tunaogopa kumsogelea kisa kulaaniwa
 
Wenyewe wanashangaa wameshika je madaraka?wanashangaa tozo kuwaumiza wanannchi,wanashangaa mafuta kupanda bei wanashangaa gesi kupanda bei kila kitu kushangaa hata katiba mpya watu wanapoidai bado wanashangaa kila kitu kushangaaa serikali ya kushangaa .Uwauliza swala la ajira kwa vijana watakwambi hata wao wanashangaa haya tuendelee kushangaaa
Kwenye madaraka waliwekwa tu hilo hawawezi kushangaa wanashangaa mengine.
 
Yeye ndo chanzo cha yote kwa kuanzisha miradi kwa pupa Ili kupata sifa awakonge waliomtangulia bila kujali tunaoumia ni sisi,dabo tozo ni matokeo ya hazina kukauka Wawekezaji walikimbia sera firishiki sasa tajiri akiwa masikini kodi utapata wapi?.

Rais inafaa atoke familia ya matajiri au wafanyabiashara ndie anaweza kuwa na nyota ya pesa.
Wananchi wakiwa na pesa tele uwekezaji na manunuzi yataongezeka yakiongezeka, makusanyo ya kodi yataongezeka.
Nasikia hata chanjo zikibuma mmepanga kusema ni Magufuli
 
Wanazidi kuongeza pressure ya wananchi kudai katiba mpya.

Hakuna uhusiano wa bei ya mkaa na katiba mpya.

Hiyo katiba mnayoiota ikigusa kila kitu katika maisha si utakuwa mzigo mkubwaaa!!?? Kiutekelezaji na kuibeba kwa ajili ya kwenda nayo mahali fulani 🤣🤣🤣.

Hata kwenye biblia wameandika, kama kitabu hiki kingeandika mambo yote ya manabii, kingekuwa kikubwa hata mtu asiweze kukibeba.
 
Kama gari za kusambaza gesi zinatumia mafuta kwa nini gesi isipande wakati bei ya mafuta imepanda?
 
Tic / mabalozi tafuteni mwekezaji aweke kiwanda achakate gesi ili kila mwananchi mjini na vijijini anufaike ili matumizi ya gesi yawe kama Simu. Nchi imebarikiwa rasilimani tujue namna ya kuzitumia kwa manufaa ya kiuchumi
 
Wewe ulichukua hatua gani? Kwa sababu ww nawe ni mwananchi hetuambie!
Hata mafuta ya kupikia yalipopanda bei Serikali ilishangaa pia na mpaka leo hii hayajashuka bei. Wananchi goigoi huzalisha Serikali goigoi.

Imagine Serikali hii iliyokosa kibali cha wananchi iliingia madarakani kwa kupora uchaguzi huku wananchi waking'a ng'aa macho tu badala ya kuchukua hatua.

Matokeo yake imepatikana serikali goigoi ambayo tatizo linapotokea inatoa macho na haijui cha kufanya.Kikubwa ambacho huwa inaweza kufanya ni kudanganya wananchi hasa kupitia waziri mkuu.Wananchi wajiandae kulipa uzembe waliofanya.Period.
 
Back
Top Bottom