Serikali yashangaa gesi ya kupikia kupanda bei, yataka viwanda vieleze sababu ya ongezeko hilo

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesitisha upandaji wa bei za gesi za kupikia zilizopanda maradufu katika baadhi ya maeneo nchini hadi hapo itakapotangazwa tena kutokana na upandaji wa bei hizo kutofuata taratibu.
iwe imezua kupandishwa kwa bei ya jumla? ila kama inazuia bei ya rejareja,wataishia kama ilivyokuwa kwenye sukari.itaadimishwa
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesitisha upandaji wa bei za gesi za kupikia zilizopanda maradufu katika baadhi ya maeneo nchini hadi hapo itakapotangazwa tena kutokana na upandaji wa bei hizo kutofuata taratibu.
22,000/= 15kg
 
Hawa EWURA kwenye mafuta kuna mlungula wanakulaga sio buree.
 
Hao Uwura mbona bei ya Mafuta ya Magari n.k hawaingilii kupunguzwa au sababu kuna percent zao humo so wanaingilia yasiyowahusu tu kenge zao.

Wacha kila kitu kipande bei maana Nchi ndio inaendeshwa hivyo yaani wapandishe wao tu wengine hapana kama vipi kila kitu kipungua na tozo ziondolewe... Naomba nauli za Mabasi daldala zipande pia kama Mwendokasi 650
 
Mbona Maisha ya mtu wa chini yanazidi kua magumu awamu hii ya sita?
Mara tozo
Mara Bei ya mafuta na Sasa hii bbei ya gesi.
Hivi viongozi wa hii serikali hawajui kwamba Bei ya gesi ikipanda misitu itazidi kuteketea.
Bora umeliona hilo mkuu, yaani tunarudi kulekule kwenye kuteketeza misitu kwa kuendekeza haya mazwazwa yanayoshangaa shangaa tukija kukurupuka nchi haina mti hata mmoja.....
 
Maeneo mengine serikali wako makini, ila sehemu nyingine wanawaachia wananchi mizigo waibebe wenyewe, au kwasababu hili halijapitia bungeni ndio maana serikali imesimama na wananchi? kwa sababu kama likipitia bungeni hata likiwa na maumivu kwa wananchi lazima lipitishwe.
Mkuu na wewe umeamini kama wenye viwanda wamejipandishia tu bei?
 
Maeneo mengine serikali wako makini, ila sehemu nyingine wanawaachia wananchi mizigo waibebe wenyewe, au kwasababu hili halijapitia bungeni ndio maana serikali imesimama na wananchi? kwa sababu kama likipitia bungeni hata likiwa na maumivu kwa wananchi lazima lipitishwe.
Mkuu ndio maana tunasema bunge halina impact yeyote kwa maendeleo ya wananchi. Kwa sasa halifai kuwepo kwani ni mzigo kwa taifa, kama lingekuwa ni shirika la Umaa (ATCL, UDA n.k) basi tungesema linaendesha shughuli zake kwa hasa na kutakiwa kulifunga na waajiriwa wake kupatiwa haki zao za redundancy.
 
Wananchi wanashangaa na serikali inashangaa maajabu

Halafu kuna watu wanasema siasa haina maana

Nasubiri kuona wapinzani wakiumia kwa hili swala.
Mkuu mimi nawaomba wapinzani wasiumie kwa suala hili, hili ni suala la wananchi wenyewe waachwe wapambane na hali zao, maana wao wanataka unafuu wa maisha kupitia majasho ya wengine. Waache wapinzani wapambane na KATIBA MPYA.
 
Back
Top Bottom