Serikali yashangaa gesi ya kupikia kupanda bei, yataka viwanda vieleze sababu ya ongezeko hilo

Mkuu hapo hakuna kitachobadilika, hao wenye viwanda watatoa pesa na mambo yataendelea
Hao Ewura watakuwa na utapiamlo wa akili.

Hiyo gas inasafirishwa kwa maji kwenda kwenye masoko? Umepandisha bei ya mafuta, gharama za malori mpaka bodabida zimepanda, sasa hiyo gas inabebwa kichwani?
 
Mbona Maisha ya mtu wa chini yanazidi kua magumu awamu hii ya sita?
Mara tozo
Mara Bei ya mafuta na Sasa hii bbei ya gesi.
Hivi viongozi wa hii serikali hawajui kwamba Bei ya gesi ikipanda misitu itazidi kuteketea.
Wanasema kuwa kuke kanda ya ziwa kuna uwezekano wa kutumia kinyesi cha ng'ombe. Na bei za nyasi porini hazijapanda.

Kule ambako hakuna ng'ombe, wanakima sana mahindi, watumie mabua na magunzi ya mahindi kupikia.
 
Inahitaji tone Moja tu la akili kutambua sababu za kupanda bei ya bidhaa. Tozo za kijinga Kila mahali zinapunguza mzunguko wa pesa. Kwa bahati mbaya tuliopo kitaa tuna mawazo mazuri ya maendeleo lakini walio na wadhifa na nafasi ya maamuzi, hawawazi lolote zaidi ya kulinda nafasi zao watawale milele
Jumong anafungua nchi
 
elezeni
Serikali imesema viwanda vya gesi ya kupikia havijafata utaratibu katika kupandisha bei hivyo bei mpya hazitambuliki.

Afisa wa Ewura mr Kaguo amesema viwanda vya gesi vimetakiwa vipeleke vigezo vya kupandisha bei na serikali ama itavibariki na kukubali bei mpya ama itavikataa kama havijitoshelezi.

ELEZENI TOZO ZA SIMU KWANZA ZINAUHALALI GANI ,KABLA YA KUGEUKIA GESI
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom