Serikali yasema treni ya SGR haitokuwa na tatizo la umeme

Sasa hivi yenyewe hapa nilipo umeme umekatika na kurudi ni saa 12 jioni na hii ni kila siku mwezi mzima sasa,sembuse huo mradi mkubwa ndio watauweza vipi.

Uongo mtupu.
 
Nalo litatuletea hasara kubwa zaidi ya yale madege.

Hakuna mradi wa Magufuli utakaoleta tija kwa walipa kodi. Waajirwa wa maahirika husika ndio wataonufaika kwa overtime na mishahara.
hii italeta faida mizigo ya kubeba ipo tofauti na biashara kichaa ya ndege ni hasara dunia nzima.
 
Hawajatatua matatizo ya huu unaokatika Mara kwa Mara, wanaongelea wa SGR. ?
Kwanza abiria watawapata wapi ilhali mabasi yanaboresha huduma?
Labda SGR ya Dar Mza abiria watakuwepo.
Waziri akae na ma engineer wake wa solve tatizo la umeme wa viwandani na majumbani kukatika Mara kwa Mara. Kama ma engineer hawana huo uwezo ruksa ku import toka Burundi
 
hii italeta faida mizigo ya kubeba ipo tofauti na biashara kichaa ya ndege ni hasara dunia nzima.
Kama watafungua inland container Depot pale Moro ili wazambia, warundi na watu wa Mwanza wachukulie makontena yao pale hii reli itakua na tija sana. Na foleni ya Kibaha Chalinze itapungua sana.
Hili wazo sijui Kama serikali yetu sikivu inalo...
 
Umeme wa Tz huwa unakatika kwa dakika 10 tu!! Tutaona.
 
Serikali imewahakikishia Watanzania kuwa Treni ya Kisasa (SGR) haitakuwa na tatizo la umeme, kwa sababu mabehewa yatakuwa na uwezo wa kuhifadhi umeme wa ziada kwa saa moja hadi mbili.

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani, alibainisha hayo mwishoni mwa wiki mjini Morogoro wakati akifungua kikao kazi kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Dk Kalemani alisema kumekuwa na wasiwasi kuhusu umeme utakaotumika katika uendeshaji wa SGR, lakini hilo halipaswi kuwa tatizo, kwani mabehewa yatakayoendesha mradi huo yatakuwa ya kisasa.

“Kumekuwa na wasiwasi kwamba umeme unaweza ukakatika na hivyo treni hii isiweze kutembea, lakini ukweli ni kwamba mabehewa yatakayokuja katika mradi huu ni mabehewa yanayotumia teknolojia ya juu inayoweza kutunza umeme kwa saa moja hadi saa mbili. Kwa hiyo hata umeme ukikatika kwa dakika 10 bado SGR itaendelea kutembea,”alisema.

Dk Kalemani alisema hadi sasa Tanesco imekamilisha uwekaji wa umeme katika kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa kilometa 160 na kwamba hata mradi huo ukitaka kuanza leo, wako tayari kuuendesha kwa kuwa nishati hiyo ipo.

Alisema wamefunga minara 456 katika njia hiyo inayoanzia Dar es Salaam hadi Kingolwira na kwamba serikali imetumia Sh bilioni 71.1 kukamilisha kipande hicho.

Reli hiyo ya kisasa itaunganisha Tanzania na nchi jirani za Rwanda, Uganda, Burundi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa lengo la

kupunguza gharama za usafiri, muda wa kusafiri, ufikishaji rahisi huduma za jamii kwa jumuiya ya eneo la mradi na uwezeshaji wa biashara kati ya Tanzania na nchi za jirani.

Mradi huo ulianza Aprili mwaka 2017 na awamu ya kwanza ujenzi ni kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, umbali wa Kilometa 300 (maili 186).

Mradi huo kiujumla utaanzia Dar es Salaam hadi Mwanza na utapitia maeneo ya Dar es Salaam, Morogoro, Makutopora (Dodoma), Tabora, Isaka (Shinyanga), Mwanza, Rusumo (Kigali, Rwanda), Bunjumbura (Burundi), Goma (DRC) na Kampala (Uganda).

Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Reli ya kisasa ambayo inatoka Makutopora, Dodoma mpaka Tabora, imefikia katika kiwango cha juu cha maandalizi. Utafiti umekamilika na ujenzi kuanza hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, Dk Kalemani alisema Tanesco kwa sasa iko imara na inafanya kazi vizuri, na kwamba serikali haina mpango wa kuligawanya au kulibinafsisha shirika hilo, kwa sababu licha ya kutopewa ruzuku na serikali pia halitengenezi hasara.

Alisema shirika hilo wakati fulani lilikuwa likipewa na serikali ruzuku ya Sh bilioni 438 na lilikuwa ikitengeneza hasara ya karibu Sh bilioni 478, lakini hadi sasa hali ya kifedha ya shirika hilo imekuwa nzuri.

Alisema, hali hiyo imetokana na shirika hilo kuacha mipango ya dharura iliyokuwa ikiendeshwa na mafuta mazito, pia kufunga mitambo yake iliyokuwa ikitumia mafuta katika vituo 12 nchini na hivyo kuokoa Sh bilioni 730 zilizokuwa zinatumia kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo.

Aidha, alisema miradi inayoendelea na ile iliyotekelezwa imewezesha Tanesco kuongeza upatikanaji wa umeme nchini na hivi sasa taifa lina umeme wa kutosha kwa matumizi mbalimbali.

Aliipongeza Tanesco kwa kusimamia vizuri Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere, ambao unaendelea vizuri na pia serikali imekuwa ikilipa fedha zake kwa wakati za mradi huo, kiasi kwamba sasa wakandarasi watatoa asilimia nne badala ya tatu kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya kurejesha faida kwa jamii.

Akizungumzia sekta ya mafuta, Dk Kalemani alisema maeneo ya mkoani Singida na Simiyu, yameonesha kuwepo kwa viashiria vya kuwepo kwa nishati ya mafuta, hivyo serikali hivi karibuni itaeleza kwa kina hatua hiyo, ikiashiria kwamba Tanzania huenda ikaanza uchimbaji wa nishati hiyo.

Chanzo: Habari Leo
Labda kama baadhi ya mabehewa yatakua ni power bank
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom