Serikali yasema itagharamia mazishi na haitokabidhi fedha kwa familia

Ila Mange hupendi amani. ...yani hata pasipokuwa na haja wewe ni kuchongea tu. Siku zingine unaongea point siku zingine pumba tupu.... yani ni shida
 
Familia ya marehemu Akwilina Akwiline inaendelea na maandalizi ya mazishi, huku ikielezwa kuwa Serikali imekubali kuyagharimia lakini si kutoa fedha.

Serikali imefikia hatua hiyo baada ya jana Februari 20,2018 familia ya Akwilina kueleza kuwa bajeti ya mazishi ni Sh80 milioni.

Katibu wa kamati ya mazishi Moi Kiyeyeu, ambaye ni kaka wa Akwilina amesema Serikali imewajibu kuwa haitawapa fedha taslim bali itagharimia vitu vilioorodheshwa katika bajeti ya mazishi hayo.

"Tulipotoa bajeti hatukuwa na maana kuishinikiza Serikali itoe fedha zote bali ilikuwa mahitaji ya msiba hadi pale utakapoisha. Tunashukuru Mungu kwa Serikali kuridhia kugharimia," amesema Kiyeyeu.

Kuhusu hilo, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika taarifa iliyotolewa leo Februari 21,2018 imesema kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Dk Leonard Akwilapo ilipokea makisio ya gharama za mazishi ya Sh80 milioni kutoka kwa msemaji wa familia, Festo Kavishe.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha wizara hiyo, Mwasu Sware alisema baada ya kupokea makisio hayo Dk Akwilapo alitahadharisha kuwa kuna baadhi ya matumizi hayatakubaliwa kwa kuwa kisheria hayagharamiwi na Serikali.

Pia, katika makisio hayo kuna gharama ambazo zilikuwa zimepewa makadirio ya juu.

Alisema katibu mkuu aliagiza kuwe na kikao kati ya wizara na ndugu wa marehemu ili kuweka sawa changamoto hizo na kuwa na bajeti ya pamoja ambacho kilifanyika jana jioni Februari 20,2018 na kufikia muafaka.

“Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa taratibu nyingine za maandalizi ya mazishi zinaendelea vizuri,” amesema.

Wakati huohuo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amefika nyumbani kwa dada wa marehemu Mbezi Luis kuhani msiba.

Dk Mwakyembe amesema tukio la kifo cha Akwilina ni la kusikitisha.
 
Wao si waliona serikali itawapa pesa wakawa upande wa serikali haya sasa hamna pesa watapewa mahitaji
Hiyo familia ingekuwa upande wa wananchi na uhakika michango ingekuwa zaidi ya hiyo milioni 80
 
Familia ilikosa tu watu wenye msimamo nakuendelea kuwaamini hata wale wala rambirambi

Hili jambo lingesimamiwa na wananchi naamini lingeenda murua kabisa
iyo hela inatosha wao kununua mbunge na madiwani kadhaa kwao ndo kipaumbele chao inauma sana

Kuwaamini hawa watu nisawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano ona sasa ata wale wafiwa wanazidi kutoneshwa vidonda vyao

Yohana ata kama sio mtanzania kua na huruma ata na majirani zako tu
Acha ikuume
 
Hawa ndugu zetu wachaga kwenye pesa sio watu kabisa nahisi hii familia ya marehemu walikuwa na mipango ya kupiga pesa tu za biashara
Sidhani kama uko sahihi. Je, kabla ys msiba huu, hawakuwa na mtaji wa biashara? Ukijibu hapo na kwa takwimu nitakuelewa vinginevyo ni uzushi usiofaa.
 
They get what the deserve. Huu msiba watu walikua wameuvalia njuga na wafiwa wangechangia na wananchi Tanzania nzima na kupata hela ya kutosha.

Kama sijasahau kuna mwanaJf alikua amejitolea gari la kubeba maiti, je kulikua na watanzania wangapi ambao walikua wapo tiari kujitolea kwa huo msiba!,but walituona hatufai badala yake walichagua other side, so let them know what's feel like when you choose wrong side.
 
Kuna watu/mtu ameishauri hii familia vibaya sana. Inasikitisha.

Kuna watu kweli hawana hofu ya Mungu. Tuendelee, labda ikifika pigo la kumi watawaachia wana wa Israeli waende.
 
NDUGU MEXENE MELLO et al.,
Naomba mnipige ban ya miaka miwili mpaka 2020.siwezi kuendelea kusoma maoni ya / comment ya wana Lumumba wapumbafu na machoko.
Ila endeleeni kushangilia, wakati bado unakuja .Magufuri kaweka vyombo vya habari kwapani, mahakama kwapani, jeshi la polisi kwani, bunge kwapani,shughuli za kisiasa na democrasia kwapani, taasisi za kidini kwapani nadhani uchunguzi kakobe mmeusikia. Shangilieni ,imbeni mtakavyo weza, tukaneni vyama pinzani mtakavyo weza, nunueni madiwani na wabunge mtakavyo weza ,ueni upinzani kadiri nguvu zenu zitakavyo weza.Ule mwisho badoo, Magufuri akianza kuuwa watu wake ndani ya ccm akihisi wanamuhujumu na wengine ndani ya chama chake , ndipo ule wakati uliotabiriwa utakuwa umewadia. Mtatafuta pa kukimbilia mtakosa, mtalia na kusaga meno ,mtaomboleza lakini hamtaona msaada wala hakuta kuwa na kimbilio. Endeleeni kushangilia, endeleeni kusifia.....siku zaja.
 
Wao si waliona serikali itawapa pesa wakawa upande wa serikali haya sasa hamna pesa watapewa mahitaji
Hiyo familia ingekuwa upande wa wananchi na uhakika michango ingekuwa zaidi ya hiyo milioni 80
Mshika mawili moja humponyoka
Familia watalia mara mbili kwani mil80 atafaida alikwenda msibani kula ubwabwa na aliyebaki Daresalama akipunga upepo
Wameyataka wenyewe.... Tamaaa imewaponza
Na movie imeishia hapo hakuna fidia wala faida ni machozi tu wameambulia
 
1. Magari yote yatatumiaka ya serikali na mafuta ya serikali.
2. Chakula chote kitatoka serikalini ( mchele kutoka hifadhi ya chakula, nyama kutoka ranchi za taifa, maharagwe hifadhi ya chakula ya taifa)
3. Jeneza kutoka karakana za magereza ( THey make best quality ).
4. MC na PA system tutatumia za wizara yoyote ( we have best PA systems, tunaweza azima hata TOT, we have good MC's for free).
5. Shughuli za kuchimba kaburi tutaweka vijana wa JKT na watakuja na vifaa vyote.

1. Posho ya viongozi wa seikali watakaoshiriki na kusafiri kwenda moshi msibani milioni arobaini,
2. chakula na vinywaji kwa viongozi wa serikali milioni 30,
3. posho za madereva wa serikali wakati wa shughuli nzima milioni 20.
Hivo vyote si vitazidi hio 80
 
Msemaji wa familia ya Akwilina amesema serikali imeikubali bajeti waliyoiandaa na kwamba gharama zote kama zilivyo zitalipwa na serikali na si kwamba familia itakabidhiwa fedha hizo. Msemaji huyo ameishukuru sana serikali kwa kuwaelewa na kuwashika mkono. Aliyasema hayo mbele ya Dr Mwakyembe aliyefika msibani hapo kuwapa pole. Source ITV habari!
 
Mshika mawili moja humponyoka
Familia watalia mara mbili kwani mil80 atafaida alikwenda msibani kula ubwabwa na aliyebaki Daresalama akipunga upepo
Wameyataka wenyewe.... Tamaaa imewaponza
Na movie imeishia hapo hakuna fidia wala faida ni machozi tu wameambulia
Walifikiri hii serikali ni ya watu wa maana.
 
Back
Top Bottom