Serikali yasema imewashtukia wawekezaji wanaobadili majina

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Mwigulu-Nchemba--December4-2014.jpg

Naibu Waziri Wizara ya fedha,Mwigulu Nchemba

Wizara ya Fedha imewashtukia wawekezaji wanaobadili majina ya kampuni kwa lengo la kutaka kukwepa kulipa kodi baada ya kuamua kubadilisha sheria.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, (pichani) alisema hayo katika mahojiano na Redio One kwenye kipindi cha Kumepambazuka kuhusu mbinu zinazotumiwa na baadhi ya wawekezaji kukwepa kulipa kodi kwa kubadili majina ya kampuni.

Mwigulu alisema serikali ilishachukua hatua kwa kubadilisha sheria ambayo sasa haitoi fursa kwa wawekezaji kupata unafuu wa kodi anapobadili jina la kampuni.

"Kubadili jina haihusiani na badiliko lolote la jina la kampuni, akibadili jina kodi ipo pale pale, kwa hiyo wanaobadili majina ya kampuni wanajidanganya watatakiwa kulipa kodi kama kawaida kwa mujibu wa sheria," alisema.

Mwigulu alisema kutokana na mabadiliko hayo ya sheria mwekezaji au mtu yeyote akibadili jina la kampuni mmliki wa kwanza ndiye anakuwa bado anatambuliwa na akiuza hisa bado taifa itanufaika kwa kodi.

Alisema serikali imejipanga kuhakikisha kila mtu analipa kodi kwa mujibu wa sheria na kwamba serikali haitakubali kuona baadhi ya wawekezaji wanakwepa kulipa kodi na kuikosesha nchi mapato.

CHANZO: NIPASHE
 
Kwa hili nimewapongeza ingawaje fedha ikipatikana wanagawana wenyewe.
 
Ndio wameshtuka leo? Mwekezaji asemehewe kodi kwa lipi wakati ana uwezo wa kuinunua nchi
 
Wizara ya Fedha imewashtukia wawekezaji wanaobadili majina ya kampuni kwa lengo la kutaka kukwepa kulipa kodi baada ya kuamua kubadilisha sheria.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, (pichani) alisema hayo katika mahojiano na Redio One kwenye kipindi cha Kumepambazuka kuhusu mbinu zinazotumiwa na baadhi ya wawekezaji kukwepa kulipa kodi kwa kubadili majina ya kampuni.

Mwigulu alisema serikali ilishachukua hatua kwa kubadilisha sheria ambayo sasa haitoi fursa kwa wawekezaji kupata unafuu wa kodi anapobadili jina la kampuni.

“Kubadili jina haihusiani na badiliko lolote la jina la kampuni, akibadili jina kodi ipo pale pale, kwa hiyo wanaobadili majina ya kampuni wanajidanganya watatakiwa kilipa kodi kama kawaida kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Mwigulu alisema kutokana na mabadiliko hayo ya sheria mwekezaji au mtu yeyote akibadili jina la kampuni mmliki wa kwanza ndiye anakuwa bado anatambuliwa na akiuza hisa bado taifa itanufaika kwa kodi.

Alisema serikali imejipanga kuhakikisha kila mtu analipa kodi kwa mujibu wa sheria na kwamba serikali haitakubali kuona baadhi ya wawekezaji wanakwepa kulipa kodi na kuikosesha nchi mapato.

SOURCE: NIPASHE
 
Porojo tu! Serikali ya CCM haina jipya! Miaka yote wawekezaji wamekuwa wakikwepa kulipa kodi, kwani wameishachukuliwa hatua gani mpaka sasa?
 
Wanakumbuka Blanket wakati jua limeshachomoza - Skintight zimewashapwaya
shakebutt.gif
 
Kama yakuongea yameisha bora aimbe iyena iyena tu, kuliko kubwabwaja
 
Hili mbona Watanzania wengi tulilijua siku nyingi, huyu alikuwa hajui hili la hawa wakwepa kodi kama wanalitumia? Labda anaishi mwezini kule hakuna print media, radio wala luninga.

Halafu wakisema hivi na sisi tunawapongeza kaazi kweli kweli miaka yooote hii walikua wapi.
 
Back
Top Bottom