Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 588
- 1,698
Naibu Waziri Wizara ya fedha,Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, (pichani) alisema hayo katika mahojiano na Redio One kwenye kipindi cha Kumepambazuka kuhusu mbinu zinazotumiwa na baadhi ya wawekezaji kukwepa kulipa kodi kwa kubadili majina ya kampuni.
Mwigulu alisema serikali ilishachukua hatua kwa kubadilisha sheria ambayo sasa haitoi fursa kwa wawekezaji kupata unafuu wa kodi anapobadili jina la kampuni.
"Kubadili jina haihusiani na badiliko lolote la jina la kampuni, akibadili jina kodi ipo pale pale, kwa hiyo wanaobadili majina ya kampuni wanajidanganya watatakiwa kulipa kodi kama kawaida kwa mujibu wa sheria," alisema.
Mwigulu alisema kutokana na mabadiliko hayo ya sheria mwekezaji au mtu yeyote akibadili jina la kampuni mmliki wa kwanza ndiye anakuwa bado anatambuliwa na akiuza hisa bado taifa itanufaika kwa kodi.
Alisema serikali imejipanga kuhakikisha kila mtu analipa kodi kwa mujibu wa sheria na kwamba serikali haitakubali kuona baadhi ya wawekezaji wanakwepa kulipa kodi na kuikosesha nchi mapato.
CHANZO: NIPASHE