Serikali yasema ifikapo Machi 31 wakulima wote watakuwa wamelipwa pesa zao za korosho

NyotaMalaika

Senior Member
Aug 6, 2012
167
77
Serikali imewahakikishia wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuwa kufikia tarehe 31 Machi 2019 wakulima wote watakuwa wamelipwa fedha zao kwani uhakiki umekamilika kwa kiasi kikubwa.

Hakikisho hilo mbele ya kamati hiyo limetolewa leo Tarehe 16 Machi 2019 na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) katika ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati akitoa ufafanuzi katika mkutano uliowakutanisha wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wake Dkt Christine Ishengoma, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Naibu Katibu Mkuu wizara ya Kilimo, wataalamu serikalini sambamba na wakulima.

"Kumekuwa na urasimu mkubwa tangu kuanza kwa zoezi hili la uhakiki lakini sasa tumeamua kama serikali kabla ya mwisho wa mwezi huu wa tatu wakulima wote wawe wamelipwa malipo yao ili kuondoa adha wanazokumbana nazo" alikaririwa Mhe Hasunga

Alisema pamoja na kwamba malipo ni mchakato unaohitaji kupitia katika hatua nyingi za mchakato ikiwemo uhakiki lakini kila jambo lenye mwanzo ni lazima kuwa na ukomo.

Alisema mpaka sasa Tani 222,684 zimekwisha kusanywa huku hadi kufikia tarehe 14 Machi 2019 tayari jumla ya Shilingi Bilioni 596.9 zimekwishalipwa kwa wakulima kati ya Shilingi Bilioni 723

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amewahakikishia wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuwa pamoja na mchakato huo wa malipo ya Korosho kuendelea lakini pia Wizara imepitia katika michakato mbalimbali ya kumpata Mkurugenzi mpya wa Bodi ya Korosho ili kuendelea na majukumu ya Bodi hiyo.

Kuhusu wanaofanya biashara ya zao hilo kinyume na sheria maarufu kama Kangomba Waziri Hasunga alisema kuwa tayari serikali imewabaini na wote watachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumzia Pembejeo feki Mhe Hasunga alisema kuwa tayari hatua zimeanza kuchukuliwa kwa wafanyabiashara wote waliofanya hujuma kwa kuwauzia wakulima Mbegu na mbolea feki ambapo hatua kali zimeanza kuchukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kutolipwa fedha wanazodai kwa kusambaza Pembejeo hizo.

Katika hatua nyingine Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameuagiza uongozi wa Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu Vya Tropiki (TPRI) kutuma wataalamu Mkoani Lindi ili kuchukua sampuli za viuatilifu kwa wakulima na kuvipima ili kubaini kadhia ya usambazaji wa viuatilifu feki kwa wakulima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Dkt Christine Ishengoma (Mb) amemuagiza Waziri wa Kilimo kuhakikisha kuwa taarifa ya malipo ya wakulima wote wa Korosho inafika bungeni tarehe 2 Aprili 2019.
 
Wote! Ina maanisha hadi wale wa Kangomba? Kama wale hawatalipwa, basi warudishiwe korosho zao. Serikali inatakiwa iwe kioo cha kutenda haki na sio dhulma wala uonevu.
Cha mlevi huliwa na mgema lakini pia mlevi hula cha mgema. Thats an equation of value exchange...
Hao wa Kangomba hawakuiba korosho. Walizinunua kwa wananchi kwa malipo halali ya fedha ya kitanzania- taslim.
 
Wote! Ina maanisha hadi wale wa Kangomba? Kama wale hawatalipwa, basi warudishiwe korosho zao. Serikali inatakiwa iwe kioo cha kutenda haki na sio dhulma wala uonevu.
Cha mlevi huliwa na mgema lakini pia mlevi hula cha mgema. Thats an equation of value exchange...
Hao wa Kangomba hawakuiba korosho. Walizinunua kwa wananchi kwa malipo halali ya fedha ya kitanzania.
fact
 
Serikali imewahakikishia wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya kilimo,mifungo na maji kuwa kufikia tarehe 31 machi 2019, wakulima wote watakuwa wamelipwa fedha zao kwani uhakiki umekamilika kwa kiasi kikubwa.
 
Miaka ya nyuma muda kama huu wakulima walishafanyabiashara yao na wameanza kuhudumia mikorosho yao.
Nawashauri watani zangu,mwaka huu achaneni kuhudumia,limeni mazao mengine mtakayouza ndani ya nchi na chakula. Kiasi cha korosho kikipatikana bila huduma mtawauzia wabanguaji kwa mikono watuuzie tutafune.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Lindi

Back
Top Bottom