Serikali yasema hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa na utaratibu wa kukagua magari yanayoagizwa nje ya nchi

Ni wakati sasa hizo kampuni za uagizaji magari zifikirie kuhamishia hizo stock hapa hapa. Sio mi naagiza gari halafu nishalipa pesa yangu nakuja kuambiwa gari ina shida, hivyo lazima itengenezwe.

Hizo gharama anafaa azibebe muuzaji, maake alinihakikishia kuwa gari iko sawa kabla sijanunua. Pre-purchase inspection inaleta maana sana kuliko hii baada
 
Hii nchi tunarudi miaka mingi sana nyuma kwa speed ya light.
Miaka ya nyuma mzee tulikuwa tunatumia brand new cars kitu nyukwaaa unachana nylon mwenyewe ndani ya gari.

Huoni kama tumefeli sahivi.

Je, tatizo ni uchumi wa watu sahv kuweza miliki magari mapya au

Ova
 
boresheni magari ya nyumbu tuyanunue

1611737963612.png
1611737963612.png
 
Miaka ya nyuma mzee tulikuwa tunatumia brand new cars kitu nyukwaaa unachana nylon mwenyewe ndani ya gari.

Huoni kama tumefeli sahivi.

Je, tatizo ni uchumi wa watu sahv kuweza miliki magari mapya au

Ova
Kimsingi uchumi umeyumba kinoma hasa kwa mwananchi wa kawaida lakini tuko uchumi wa kati! Watakaomudu brand new cars ninhao hao walioko kwa circle ya meza kuu na wateule wachache.
 
Kimsingi uchumi umeyumba kinoma hasa kwa mwananchi wa kawaida lakini tuko uchumi wa kati! Watakaomudu brand new cars ninhao hao walioko kwa circle ya meza kuu na wateule wachache.
Kweli kabisa

Ova
 
Reference Number:20211092951
Make:TOYOTA
Model:FJ CRUISER
Body Type:SUV
Year of Manufacture:2016
Country:JAPAN
Fuel Type:PETROL
Engine Capacity:2501 CC & ABOVE
Customs Value CIF (USD):17,635.00
Import Duty (USD):4,408.75
Excise Duty (USD):2,204.38
Excise Duty due to Age (USD):0.00
VAT (USD):4,474.20
Custom Processing Fee (USD):105.81
Railway Dev Levy (USD):264.53
Total Import Taxes (USD):11,457.66
Total Import Taxes (TSHS):26,456,418.37
Vehicle Registration Fee (TSHS):550,000.00
TOTAL TAXES (TSHS):27,006,418.37

COST YA GARI MPAKA BANDARINI BILA KODI

Toyota FJ Cruiser 2010 for sale -
Car Price US$ 24,436>>56,202,800 tsh

tukiwa tunaugulia maumivu hayo ya kodi maumivu mengine yakaribiA tafakari chukua hatua
Hatari kubwa! Kwa hiyo sasa hivi wameongeza kodi ya maendeleo na kodi ya ujenzi wa reli? Hii miaka 5, ni kuendelea kutumia kwa uangalifu magari tuliyo nayo, siyo kipindi cha kuagiza magari toka nje ya nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa utaratibu wa sasa wa gari kukaguliwa huko linakonunuliwa, inakuhusu kupokea gari bandari ya Mombasa na kisha kuingiza gari kupitia mpaka kokote utakakako mfano Mutukula, Sirari, Horohoro nk.
Kwa utaratibu hui mpya, hao tulioko huku tunafanyaje?

Nashauri utaratibu huu wa sasa wa ukaguzi wa gari kusimamiwa na muuzaji k.v. Beforward, SBT, Tradecarview uendelee.
Mteja apokee gari lake baada ya kukaguliwa kama ilivyokuwa awali.
 
Kwani ukiagiza gari, likafanyiwa inspection Japan, likawa na tatizo, huwa linaletwa hivyohivyo bila kurekebishwa au huwa wanarekebisha kule kule kabla ya kulileta bongo?
 
Ngoja tusubili kwanza tuone utratibu utakuwaje na tupate uzoefu. Ukaguzi wa gari huko nje ulikuwa ni utaratibu mzuri zaid kwani gari likishafika bandarini na pengine kodi zote ushalipia TRA ilikuwa ni kuchukua gari yako kupitia Clearing and Forwarding agent ndani ya siku moja au mbili kutoka bandarini na kuondoka.
Wasi wasi wangu ni muda utaakaouchukua kupata gari yako kwa utaratibu huu mpya. Tatizo wa Tz hatupo smart, tuna urasimu , kuzungushana na kujenga mazingira ya kula kwanza kabla ya kutoa huduma stahili. Utaratibu huu unaweza kuwa chanzo cha mapato binafsi ya watu. Utaambiwa gari yako mbovu usipotoa kitu halitasajiliwa Mara lipeleke gereji mara spea flan inahitajika hata kama gari ni nzima kabisa ili utoe pesa wale. Vipuri vyenyewe bei juu
Wazungu wapo smart sana hawapendi kulaumiwa au kuharibu soko lao.
Mara zote ambazo nimeagiza magari sijawahi kuagiza gari bovu. Kabla ya kulinunua likiwa na ubovu wanakwambia shida yake na hapo halijakaguliwa huko. ukilipenda kulichukua likiwa na ubovu huo ni wewe mwenyewe. Na likikaguliwa huko unatumiwa inspection certificate kabla gari halijafika na ukiona certificate imeonyesha kuwa ni zima kabisa hamna fault popote ujue ni kweli 100%.
Sisi wabongo tuna udanganyifu na uhaminifu hakuna.
 
Nchi yetu chochote kinachoanzishwa ujue kinaenda kunufaisha watu binafsi na si nchi, hatuna utendaji kazi wa kusimamia maadili, fikiria polisi usalama barabarani baada ya kuanza kulipisha faini kwa njia ya mfumo wa kieletroniki, watu wa usalama barabarani wanasumbua madreva lazima kila kituo utoe hela usipotoa utasumbuliwa hatari hata kama gari yako haina tatizo.

Kama unasafari ya umbali wa kilomita 100 tena wewe ni dreva wa hiace jiandae kwenda na kurudi utoa angalau 50,000 na ole wako ukatae kwa kuwa gari yako haina shida utaanza kupigwa faini ambazo utajuta kuwa na gari.

Kwa hiyo hata suala ukaguzi kufanyika nchini, tegemea magari mengi kuambiwa ni mabovu ili ukanunue spea kwenye maduka ambayo baadhi ya wakaguzi wana maslahi nayo au uwape kidogo ili wakuandikie hiyo certificate ya ukaguzi.
 
Wanasema yakiwa na tatizo yatapelekwa kwenye gereji zao

Tafakari chukua hatua :rolleyes: :rolleyes:
Nina nusa harufu ya yale yale ya Bakhresa na ngano yake mwaka 1995; yaani niagize gari say from Japan, lifike hapa na lionekane ni bovu, wakati linapelekwa kwenye "garage zao" mimi nawasiliana na walioniuzia gari kwa kuawaambia, "hi guys, mmeniuzia gari bovu" mengine watajuana na serikali wakati mi naramba zangu ice cream za Azam
 
Huyu jamaa haelewi hata hoja za wadau ni zipi.

Je, hizo garage zao zitakuwa zinatengeneza hayo magari mabovu bure?

Nani atabeba hizo gharama za matengeneza?

Isitoshe wabongo tunajuana huo ukaguzi lazima utagubikwa na urasimu kibao na wizi wa vifaa tu.

Shida wala siyo mitambo yao waliyoagiza ujerumani!
Huu ndio ukweli haswa kwenye urasimu na wizi, je wamejiuliza kuwa mwanzoni waliamua kukagulia nje kwa sababu gani?
 
Back
Top Bottom