Serikali yaruhusu utafiti wa mafuta Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yaruhusu utafiti wa mafuta Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]
  [/h]IJUMAA, JUNI 29, 2012 05:56 NA BAKARI KIMWANGA, DODOMA

  SERIKALI imeruhusu kuanza mchakato wa utafiti wa mafuta na gesi Visiwani Zanzabar, ili kwenda sambamba na maendeleo ya ulimwenguni.

  Kauli hiyo, ilitolewa jana bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Micheweni, Haji Khatib Kai (CUF), aliyetaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu suala la mafuta kuendelea kuwepo katika masuala ya Muungano, hali inayochangia kuchelewesha utafiti wa mafuta visiwani humo.

  Alisema Serikali haina sababu ya kuzuia suala la kuanza utafiti, kwani hivi sasa inaandaa utaratibu maalum ambao utapelekwa katika kikao cha baraza la mawaziri kwa ajili ya kutengeneza sheria ya suala hilo.

  “Binafsi sina shaka hata kidogo kuhusu kuanza utafiti na ikiwa mafuta yatapatikana Zanzibar, litakuwa jambo jema kwa nchi yetu. Lakini suala la kuwepo katika Muungano au la hili litajadiliwa na kikao cha baraza la mawaziri kwa kushirikiana na wenzetu wa Zanzibar.

  “Hili unaloniuliza lisiwepo katika Muungano sina shaka nalo, ila ndugu yangu nakuomba vuta subira katika hilo na kupitia hii Katiba mpya, linaweza likapata ufumbuzi ndani ya Katiba hiyo.

  “Ni vema sasa tutumie kutoa maoni yetu katika Katiba mpya ili kuweza kujadili mafuta kwa maslahi ya taifa letu, yaani upande wa bara na Zanzibar,” alisema Pinda.

  Akichangia mjadala wa bajeti wiki hii, Naibu Kiongozi wa kambi ya Upinzani bungeni, Zitto Kabwe, alisema suala la mafuta la Zanzibar ni vema wakaachiwa Wazanzibari wenyewe.

  Hata hivyo, alitumia nafasi hiyo kutoa maelezo kuhusu umuhimu wa mbio za Mwenge kwa kusema kuwa ni msingi muhimu ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwa kuagiza upandishwe katika kilele cha Mlima Kilimanjaro, ili kumulika maadui wa ndani na nje ya nchi

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanini Pinda na tamaa ya Wananchi wa Zanzibar? Kwanini asiwaache Wajiamulie Wenyewe?

  Waaaache Tamaa; Watanganyika Wanawatosha kwanini kukimbilia Wazanzibari na Mali zao?
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wazanzibari wameshasema mafuta ni yao. Sasa Pinda ana mamlaka gani kuyazungumzia bungeni?
   
Loading...