Serikali yaruhusu mchanga wa madini kuuzwa nje ya nchi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Serikali wilayani Same mkoani Kilimanjaro imeruhusu usafirishwaji wa mchanga wa madini aina ya Boxide kwenye machimbo yaliyopo katika tarafa ya Chome kusafirishwa nje ya nchi.
MCHANGA-WA-DHAHABU.jpg


Mchanga huo ulizuiliwa kwa muda kusafirishwa kwenda nchi za Kenya na Uganda kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli la kutaka kufanyika ukaguzi wa kutosha wa mchanga wa madini ili kile kinachosafirishwa kilingane na kile kilichopo kwenye makubaliano.

Hatua hiyo ya wilaya ya Same imefikiwa baada ya kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa mchanga huo ya Willy Interprises kuruhusiwa kuendelea na uchimbaji baada ya kusimamishwa kufuatia agizo la Raisi Magufuli la kutaka utambuzi wa makinikia zote nchini ambapo ofisi ya madini ya kanda ya kaskazini ilichukua sampuli ambazo zimeonesha kuwa kinachosafirishwa ni kile ambacho Kampuni hiyo imepatiwa kibali.

Hata hivyo baada ya kampuni hiyo kuruhusiwa kuendelea na uchimbaji, kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Same imetembelea machimbo hayo ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo, Mkuu wa Wilaya Bi. Rosemary Senyamula ameelezea kuridhishwa na mazingira waliyoyakuta mgodini hapo.

Kwa upande wa Wananchi wanaoishi jirani na machimbo hayo wamekiri kunufaika kwa kupata huduma mbalimbali za kijamii zinaotokana na mchango wa kampuni unaotolewa kwa vijiji vilivyoingia mkataba na Kampuni hiyo.

Chanzo:ITV
 
Back
Top Bottom