SNAP J
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 7,106
- 8,044
Serikali imetengua amri ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki chini ili kulinda viwanda vilivyoajiri mamia ya watanzania na kuongeza uwekezaji.
Uamuzi huo ulitolewa na Ofisi ya Makamu wa Raisi wakati Naibu Waziri wa mazingira, Luhanga Mpina na Mkurugenzi wa Mazingira, Dr. Julius Ningu walipozungumza na waandishi wa habari wiki iliyopita.
"Tunazo kampuni 26 zinazozalisha mifuko hiyo . Hatuwezi kuwaambia wasitishe uzalishaji wakati Serikali yenyewe inasisitiza uwekezaji na wao tayari wameajiri watu kadhaa mpaka sasa," alisema Dr. Ningu.
Dr. Ningu alifafanua zaidi kuwa mifuko itakayozalishwa itapaswa kuwa ya zaidi ya maikroni 30 ambayo itaweza kutumika zaidi ya mara moja, hivyo kupunguza inayotupwa na kuzagaa mitaani.
Ikumbukwe kuwa Agosti mwaka juzi' aliyekuwa waziri wa Mazingira ,Dr. Theresia Huvisa alipiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo na kutangaza mifuko iliyokuwapo iwe imeshatumika na kusiwapo na uzalishaji au uagizaji mwingine.
Wakati aliyekuwa Dr. Huvisa akisema kuwa mifuko hiyo ni hatari kwa afya za binadamu na mazingiram Dr. Ningu alisema haina matatizo na kubainisha kuwa tatizo lipo kwa watumiaji kuitupa hovyo.
Chanzo: Mwananchi newspaper
Nami nikajaribu kuchimbua adhari za hii mifuko ya plastiki, ndipo nikakutana na hii..
Hatari:Uchomaji mifuko ya plastiki hushusha kinga za mwili, huathiri akili- Mwananchi June 13, 2014.