Serikali yarudisha kifaru kutoka Jamhuri ya Czech

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,532
Hili ni lazima lisemwe na kuingia kwenye kumbukumbu.

Mnyama adimu aina ya kifaru aliyepelekwa ughaibuni arudishwa Tanzania.

Mtakumbuka sana tulishangaa juu ya twiga kupandishwa ndege na kupelekwa ughaibuni kimya kimya sasa naona muelekeo wa nchi ni kurudisha wanyama walioondolewa nchini.

Chanzo: ITV

========

faru28.jpg

Wadau wa uhifadhi kutoka Jamhuri ya watu wa CZECH kushirikiana na shirika la hifadhi za taifa TANAPA wamefanikisha kumrudisha nchini Faru mweusi anayejulikana kwa jina la Eliska’s ikiwa ni mikakati ya kuongeza wanyama hao waliyo hatarini kutoweka kutokana na matukio ya ujangili yanayo tishia uhifadhi wa Tanzania.

Faru Eliska's aliwasiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa kilimanjaro majira ya saa mbili asubuhi.

Akizungumza wakati wa kumpokea Faru huyo jike mkurugenzi wa shirika la hifadhi za taifa Tanapa Alan Kijazi amesema mnyama huyo ni sehemu ya Faru waliyochukuliwa nchini miaka mingi iliyopita ambapo sasa wadau wa uhifadhi wameona pengo lillopo baada ya wanyama hao kutoweka kwa kasi kwa matendo ya ujangili wameamua kurudisha sehemu ya Faru ili kuimalisha uhifadhi wa Tanzania.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick amesema serikali inasikitishwa na hatua ya watu wachache kufanya ujangili wa rasirimali za taifa na vitu vianvyo semekana kutengenezwa baada ya kuawa kwa Faru havilingani na thamani ya mnyama huyo ambaye ni uridhi wa dunia.

Mhifadhi mkuu wa hifadhi taifa ya Mkomazi alipo pelekwa Faru huyo Bwana Marko Meoli amesema wamejipanga kuwalinda wanyama hao adhimu ili kuhakikisha kuwa hakuna jangili atakaye ingia kwenye eneo ilo.

Chanzo: ITV
 
Hili ni lazima lisemwe na kuingia kwenye kumbukumbu.

Mnyama adimu aina ya kifaru aliyepelekwa ughaibuni arudishwa Tanzania.

Mtakumbuka sana tulishangaa juu ya twiga kupandishwa ndege na kupelekwa ughaibuni kimya kimya sasa naona muelekeo wa nchi ni kurudisha wanyama walioondolewa nchini.

Source:ITV HABARI
:confused::confused::confused::confused::confused::confused::confused::confused::confused::confused::confused:
 
Hili ni lazima lisemwe na kuingia kwenye kumbukumbu.

Mnyama adimu aina ya kifaru aliyepelekwa ughaibuni arudishwa Tanzania.

Mtakumbuka sana tulishangaa juu ya twiga kupandishwa ndege na kupelekwa ughaibuni kimya kimya sasa naona muelekeo wa nchi ni kurudisha wanyama walioondolewa nchini.

Chanzo: ITV
Vipi walioshiriki kuwatorosha hao wanyama kama twiga walishawajibishwa?
 
Nimeona hii habari ITV huyu mnyama kaletwa na ndege kubwa ya kampuni ya DHL nikakumbuka lile lidege kubwa lililotea mitambo feki ya Richmond.

Tunaomba tujulishwe gharama ya kumleta huyu mnyama kwa ndege hiyo ya DHL.
 
Naona umekuwa mpole baada ya udc kuota mbawa
Hata kwenye U-RC ulisema haya haya...siishi kwa ulaji kama unavyoshi...mimi ni mzalendo na niko sehemu najenga nchi lakini kikija suala la ukigeugeu wa kisiasa lazima niongee!

Inawezekana mimi ni sehemu ya wanaoteua...teh teh teh!
 
Hili ni zuri na linapendeza. Heko kwa hilo.

Penye zuri tutasifia sana tu. Panapohitaji marekebisho patasemwa pia. Hakuna maendeleo bila kukubali changamoto...
 
Back
Top Bottom