Serikali ya Tanzania yaridhia utoaji mimba

Susuviri, Heshima yako mkuu;

But in one note; we have to not that there is no freedom without a limit. Suala la utoaji mimba ni nyeti katika mila za kitanzania na kiafrika kwa ujumla. Si kila kitu kinachotoka Ulimwengu 'ulioendelea' ni kizuri. Kuhusu uhuru wa wamama wamepewa na ile sheria ya kujaamiana. Sasa na hili la utoaji wa mimba kumbuka it takes two to tangle. Sasa na haki ya mwanaume katika kiumbe hicho itawekwa wapi? Je haki ya huyo mtoto as a human being italindwa vipi?
Umaskini tabu sana, unakuta nchi imeadiwa pesa na wafadhiri kuridhia maazimio kama haya ya ajabu ajabu.

Shadow.

Shadow asante. Njaa ndo imemfanya hata waziri akawa anasema wameridhia tu mkataba lakini haijatungwa sheria. Mikataba mingi tunaridhia kinyume na dhamira zetu kwa maslahi yasiyo wazi na hili ni mojawapo. Ndio nikasema ukoloni mamboleo sikueleweka. Basi tuyaite utumwa mamboleo Ingekuwa kuua ni jibu zamani vilema wengi waliuawa wachanga. Je ni vilema wangapi tena waliotoka familia fukara kupindukia tunawaona leo wakihudumia jamii kwa mengi?
 
Jambotemuv, mkuu nashukuru sana kwa response yako throughout.
Shadow, mkuu kama utaruhusu naomba niunganishe hapa maoni yangu na kuwa jibu kwa pamoja kwani naona kuna baadhi ya points zime-overlap.

1. The role of God in creation and in raising children:
JAMBOTEMUVAll children are born uneducated, poor, etc. Doing the best, with the help of GOD, to provide for the helpless child is what is expected of parents.

..... The fate of any child is never certain to anybody other than GOD. I doubt whether your mother would say she honestly knew where you would end up in life.
Nadhani nitaanza kwa kuleta angle ambayo ni ngumu kwa wengi kuuona lakini ni fact, wapo watu na si wachache ambao hawaamini kuwa Mungu ana role yoyote katika maisha ya binadamu. They are atheists. Wao wanaamini kuwa kuumbwa kwa binadamu ni chemical and biological. Wao je, utawaweka wapi? Kama haamini, huwezi kumlazimisha, na anaona hana uwezo wa kulea mtoto. It is their right.
Pia katika hili mimi nasema tunakuwa tunamsingizia vitu vingi Mungu. Hivi kweli katika dunia ya leo mtu unaweza kusema kila mtoto anazaliwa na riziki yake? Alafu unamtuma mtoto aende kwa mjomba, mama mdogo ec kuomba school fees? Unaweza kweli ukajizalia tu mtoto na ukamwacha to the mercy of God and the society? Mi naona tumeshapita na kuvuka that stage. My mother could not say 100% where I will be but she knew that the upbringing and education she gave me will enable me to survive anywhere in the world! Na kwa hilo namshukuru sana. Pia namshukuru Mungu (kwa sababu namwamini) kwa kunipa nguvu na bahati lakini naamini you have to help yourself in order for God to be able to help you.

2. Taking away Life
Control over ones body has never been extended to the right to endanger or take away life. Ndio maana ikithibitika umefanya jaribio la kutoa maisha yako mwenyewe unatiwa hatiani.
Again mudering a helpless child is not having control over ones body but over the child's life and unfairly so.
Hapo hatukubaliani kwamba mtu akitaka kujiua eti unatiwa hatiani and that is right! No it is not right! It is your body and your life. The only one who can judge a person (if you beleive) in this case is God alone, siyo sheria ya nchi. Kwa nini nasema hivyo? If you have intense suffering and you willingly want to end your life, why should anyone deny this from you?
Getting back to the unborn babies, uliuliza nani atawatetea, mama zao just like when they are born. The other point of contention, when does an embryo constitute a human being. That is also up for debate as religious people say at conception, scientists have varying answers. This problem comes up in the case of cell harvesting etc.

3. Ukoloni/utumwa mamboleo
SHADOW: But in one note; we have to not that there is no freedom without a limit. Suala la utoaji mimba ni nyeti katika mila za kitanzania na kiafrika kwa ujumla. Si kila kitu kinachotoka Ulimwengu 'ulioendelea' ni kizuri. Kuhusu uhuru wa wamama wamepewa na ile sheria ya kujaamiana. Sasa na hili la utoaji wa mimba kumbuka it takes two to tangle. Sasa na haki ya mwanaume katika kiumbe hicho itawekwa wapi? Je haki ya huyo mtoto as a human being italindwa vipi? Penal Code yetu imebainisha vizuri kabisa kwamba kama mimba inahatarisha maisha ya mama basi hapo mwanamke anahaki ya kuitoa na mengine kama hayo.

Umaskini tabu sana, unakuta nchi imeadiwa pesa na wafadhiri kuridhia maazimio kama haya ya ajabu ajabu.

JAMBOTEMUV:Shadow asante. Njaa ndo imemfanya hata waziri akawa anasema wameridhia tu mkataba lakini haijatungwa sheria. Mikataba mingi tunaridhia kinyume na dhamira zetu kwa maslahi yasiyo wazi na hili ni mojawapo. Ndio nikasema ukoloni mamboleo sikueleweka. Basi tuyaite utumwa mamboleo Ingekuwa kuua ni jibu zamani vilema wengi waliuawa wachanga. Je ni vilema wangapi tena waliotoka familia fukara kupindukia tunawaona leo wakihudumia jamii kwa mengi?
I continue to disagree that this is a Western or Eastern, African, Asian, European initiative. I call it Enlightment. Tukichunguza hata jamii za Marekani, Ulaya etc tutaona ya kuwa walikuwa na mfumodume, iliyofanya wanawake wanyimwe haki zao hivyo utoaji mimba ilifanyika kwa siri, ukichangia na dini (ambazo zote ziko based mpaka leo kwenye mfumodume) basi unaweza kuona ya kuwa everything goes back to male dominance over female. System ilikuwa (na bado ni katika mfumo huu) Wanaume wanataka kuwaeleza wanawake wafanye nini. Lakini baada ya wanaharakati (siyo akina mama tu, bali hata wanaume walioendelea kifikra) kujaribu kuhakikisha akina mama wanapewa haki zao, ndipo tunaweza kuona mabadiliko katika jamii za Marekani na Ulaya. Lakini hii haina maana kwamba wote katika jamii hizi wanakubali na wapo wanaharakati wanaopinga (pro Life) na wanaotetea (Pro Choice) utoaji mimba.
tukija kwa ukoloni huu na wafadhili let us be honest for once. Enyi watetezi wa ProLife, ni wangapi mnakuwa active katika charity na kusaidia mamilioni ya watoto ambao ni maskini, wametelekzwa (yatima) au wanateswa (abused). Because if you advocate such policies that is the least you can do. And BTW naomba nitoe analogy: hata mimi kama ni mfadhili na familia ninayoisaidia naiona inazaliana tu na kusema eti Mungu atampa kila mtoto riziki yake, lakini wanaishi kwa pesa zangu, lazima nitawa-change-ia na kuwashauri wajaribu family planning. Ama sivyo naacha kuisaidia familia hiyo, maana inaonekana msaada wangu hautakuwa na mwisho. It's fair isn't it?
At the end of the day, mimi binfasi siwezi kumshauri mwanamke atoe mimba akija kwangu kwa ushauri, lakini niko tayari kumpa options zake na nita-respect her decision.
Wakuu nashukuru kwa debate nzuri na ninaendeleakusubiri maoni yenu, shukrani!
 
Kama serikali imesharidhia mkataka huo, hiyo ni ishara tosha kwamba inakusudia kutunga sheria ya kuruhusu wanawake watoe mimba.Anacho ongea Marmo si lolote ila ni danganya toto tu.Serikali itatunga sheria ya kuruhusu uotaji wa mimba,hakuna kinachoweza kuzuia.Nchi yetu imeshaingia kwenye mtandao wa kishetani.Tunaomba Mungu awalinde wale wote wenye nia ya kweli ya kuwatetea wananchi maskini wa Tanzania.

Serikali yaridhia utoaji mimba
* PRO-LIFE yapinga, yamwandikia Kikwete

na Joseph Sabinus

Tanzania Daima~Sauti ya watu

SERIKALI imetia saini kuridhia itifaki za haki za wanawake, ikiwemo ya kuruhusu utoaji mimba nchini.

Tanzania imeridhia mkataba huo, huku madhehebu mbalimbali ya dini yakipiga marufuku utoaji mimba, kwani ni kinyume cha mafundisho ya dini.

Itifaki hiyo ambayo inasubiri kutungiwa sheria bungeni ili ianze kutekelezwa, imo katika Mkataba wa Haki za Binadamu na Haki za Wanawake barani Afrika na Itifaki ya Maputo.

Itifaki ya Maputo inazipa wajibu nchi wanachama kuhakikisha kuwa, zinalinda na kuboresha afya za wanawake, hususan afya ya uzazi.

Itifaki hiyo kwa mujibu wa uchunguzi, inaainisha haki mbalimbali za mwanamke, ikiwa pamoja na haki ya kuamua kuzaa au kutozaa, haki ya kuamua kupata watoto na nafasi ya mtoto mmoja hadi mwingine, pamoja na haki ya kuchagua njia ya uzazi wa mpango, ikiwemo kutoa mimba.

Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge, Philip Marmo, alithibitisha kuridhia kwa itifaki hiyo katika barua yake yenye Kumb. Na. I/CFC.188/444/01 ya Januari 30 mwaka huu, kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutetea Uhai (PRO-LIFE), Tanzania, Emil Hagamu, aliyeiandikia barua serikali kuhoji uhalali wa Tanzania kuridhia itifaki hiyo.

Katika barua hiyo, Hagamu alimwomba Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuingilia kati na kuzuia haraka mauaji ya watoto yanayoweza kutokea endapo Bunge litapitisha sheria ya utoaji mimba.

Akifafanua kuhusu kuridhia kwa itifaki hiyo, Waziri Marmo katika barua yake ya majibu kwa PRO-LIFE ambayo Tanzania Daima ina nakala yake, alisema Itifaki ya Haki za watu na Haki za Wanawake Barani Afrika, Ibara ya 14, kipengele cha (2) C, kinasema:

“Kwa kuangalia maudhui ya vipengele hivi kwa ujumla ni kweli inatoa tafsiri sahihi ya kuridhia utoaji mimba ili kukidhi vigezo kama inavyojieleza, ambavyo ni kwa mimba iliyosababishwa na shambulio la aibu kama vile kubakwa au kwa mimba inayohatarisha afya ya mwili na akili ya mama au uhai wa mtoto.”

Akirejea barua ya PRO-LIFE, Tanzania yenye kumbukumbu namba PLT/C-A/2009 ya Januari 5, mwaka huu, Waziri Marmo alikiri kuwa kweli Tanzania imeridhia itifaki hizo, lakini bado hazijatungiwa sheria.

“Ni kweli Tanzania iliziwekea sahihi na kuridhia itifaki za Haki za Wanawake katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Haki za Wanawake barani Afrika na Itifaki ya Maputo,” alisema.

Waziri Marmo katika barua hiyo kwa Mkurugenzi wa PRO-LIFE, ambaye pia ni Mratibu wa Human Life International (HLI) Kanda ya Tanzania, alisema japo Tanzania imeridhia itifaki hizo mbili, bado hakuna sheria iliyotungwa kusimamia au kuruhusu utoaji mimba.

“Taratibu nchini Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine ni kwamba, itifaki na mikataba ya kimataifa, haiwezi kuwa sheria ya nchi hadi zitakapotungiwa sheria za Bunge.

“Isitoshe, lugha zinazotumika katika itifaki mbalimbali zinakuwa za jumla sana na tafsiri yake inaweza kupotoshwa kwa urahisi ikifanywa bila kufuata tafsiri ya vyombo husika vilivyopewa mamlaka ya kutoa tafsiri ya maana ya miandiko katika sheria ambayo hapa kwetu ni Mahakama,” inasema sehemu ya barua hiyo.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Waziri Marmo alifafanua kuwa Tanzania imeridhia itifaki hiyo kama ilivyo kwa nchi nyingine.

Hata hivyo alisema mchakato wa kutungia sheria bado unafanyiwa kazi ili kujua kama sheria hiyo ni muhimu kwa sasa nchini.

“Kuridhia ni suala jingine, lakini tujiulize tuna mahitaji hayo kwa sasa? Ni sawa na kuwa na msitu wa miti mingi, halafu unajiuliza, je, nahitaji kupanda miti mipya kwa sasa?

“Kwa hiyo niseme tu kwamba ni kweli serikali imeridhia kuingia na imesaini mkataba huo, lakini mchakato wa kupitisha sheria bado unafanyiwa kazi,” alisema Waziri Marmo.

Akizungumza na Tanzania Daima baada ya kupata barua ya ufafanuzi kutoka kwa Waziri Marmo, Hagamu alisema PRO-LIFE, Tanzania iliwaomba Waziri Mkuu na Spika wa Bunge, kumshauri Rais na wabunge kuwa makini ili wasiruhusu kupitishwa kwa sheria hiyo inayolenga kutekeleza maamuzi ya Itifaki ya Maputo (Maputo Protocol) yaliyopitishwa miaka miwili iliyopita.

Akifurahia tamko hilo la serikali kuhusu kutoruhusu au kutunga sheria ya kuhalalisha utoaji mimba, Hagamu alisema utekelezaji wa Makubaliano ya Maputo yanayozilazimisha nchi zilizosaini kuridhia kuwapo kwa sheria hiyo, kunamaanisha kuruhusu umwagaji damu kwa kuwafanyia mauaji watoto ambao hawajazaliwa.

Alisema endapo sheria hiyo itapitishwa, Watanzania wajiandae kushuhudia watoto ambao ni taifa la kesho, wakiangamizwa bila sababu za msingi huku wanawake wakiteseka kutokana na madhara ya utoaji mimba.

“Utoaji mimba haujawahi kuleta manufaa yoyote katika nchi zilizowahi kupitisha sheria hiyo... Inabidi serikali na viongozi wote watambue wajibu mkubwa walio nao katika kulinda maisha ya watu wao tangu wakiwa tumboni, wakizaliwa, wakiwa vijana na hata wanapozeeka,” alisema Hagamu.

“Kwa kuwa haki ya mwanamke haipatikani kwa kumuua mtoto wake aliye tumboni, bali kwa kulinda hadhi yake ya umama, tunaitaka serikali kuachana kabisa na wazo la kutaka kuleta sheria hii ya mauaji kwa watu wasio na hatia wala uwezo wa kujitetea,” alisema Hagamu.

Tanzania ilisaini itifaki hiyo Novemba 5, 2003; Bunge likaridhia Machi 3, 2007 na rais kutia saini Mei 7, mwaka huohuo.

Kati ya nchi 53 za Umoja wa Afrika, nchi 45 zimesaini itifaki hiyo na 25 tayari zimeridhia kupitia mabunge na Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo 25.
 
Ukisikia ukoloni ndio huu,maada ya kiswahili unaleta kingereza ili iwaje,na sisi tukileta kichina,na yule wa poland akileta kipolish tutafika,hii ndio kuwa brain washed na hatutoendelea kama hatutojua wapi tunatakiwa kutumia kingereza na wapi tunatakiwa kutumia lugha yetu ya taifa.
Wadhungu kweli wametupata waafrica.
Kweli mtu wangu,hivi hao wenye Kiingereza chao na wao huwa wanapagawa na Kiswahili kama sisi!?Hii aibu kwelikweli,kama sehemu ni lugha ya Kiingereza inatumika basi na wewe tumia na kama ni Kiswahili kitumike panapostahili.
Binafsi,ningeweza kuamurisha ulimwengu na ukanisikiliza ni Kiswahili tu kwa kwenda mbele.
Kutoa mimba ningependa kuwe kwa masharti ambayo yana lazimika katika kuokoa uhai wa mtu.
 
Hivi mimba zinazotokana na kubakwa katika Tanzania ni nyingi kiasi cha kutungiwa sheria ya kuziondoa?. Je umeshafanyika utafiti kugundua ni wangapi walibakwa na wanataka kuzitoa hizo mimba?. Marmo, kama huna kazi ya kufanya mwoombe Rais akupumzishe.
 
Control over ones body has never been extended to the right to endanger or take away life. Ndio maana ikithibitika umefanya jaribio la kutoa maisha yako mwenyewe unatiwa hatiani.
Again mudering a helpless child is not having control over ones body but over the child's life and unfairly so.

Vile vile ukimuua mwanamke mwenye mimba mara nyingi si wanaku charge na double homicide?
 
Hakuna cha kuhalalisha wala nini.....hakuna haja ya sheria...sheria za nini? Ndio maana Pinda alikuwa sawa tu na ni sawa tu mafisadi waendelee kuiba. Chukua chako mapema....mmesahahu hiyo?
 
Susuviri asante kwa changamoto. Kutetea uhai wa wachanga ambao hawajazaliwa hakutegemei tu imani kwa Mungu wetu. Uuaji kwa ksitisha uhai wa kitoto kichanga ni kosa kubwa uwe unamwamini Mungu au humuamini. Ndio maana hata wanyama - mbwa, paka, simba, chui, kuku nk ni wakali sana katika kutetea maisha ya vichanga vyao. Awali niligusia kuwa wengi wanaotoa mimba japo kwa siri hutumia gharama kubwa na mara nyingi ni ili kujirudishia uhuru wao wa kuendelea kustarehe na kufurahia maisha bila kuwajibika kulea. Na wengi wametoa mimba zaidi ya mara moja kwa sababu zilezile. Wale maskini unaowarejea kwenye hoja zako huwa hawamudu hizi gharama na ndo huzaa na kulea na siamini watoto wao wote huishia kuwalaani mama hawa kwa kunusuru uhai wao.

Kwamba mtoto ambaye uhakika wa kumtunza haupo ni haki auawe itatupelekea siku moja kupendekeza watoto wote wanaoonekana hawana matunzo na vilema wakusanywe na kuteketezwa ili kuwaondolea mateso. Yaemekana Idi Amini aliwahiusanya vilema na kuwamwaga ziwa Nyanza. Tuyabariki hayo?

Nashukuru umetambua kazi alofanya mama yako akakupatia msingi wa maisha. Naamini bado ukimuuliza hatakuambia alikuwa na mahitaji yako yote tayari ndipo akaamua kukuzaa bali nia na utayari wa kukutafutia mahitaji alikuwa navyo. Haya yanakosekana kwa wamama wengi wanaoridhia kutoa mimba moja baada ya nyingine.

Jiulize. Iweje wapo wamama wengi wanaojuta hadharani na kuulaani uamuzi wao wa kukubali kutoa mimba?. Kama ulikuwa uamuzi sahihi na wa busara vipi leo uwanyime usingizi? Something seriously wrong here.
 
Wadau watofautiana utoaji wa mimba

na Nasra Abdallah na Lucy Ngowi

SERIKALI imetakiwa kuwaomba wananchi radhi kwa kuridhia kusaini itifaki ya haki za wanawake, ikiwemo kuruhusu utoaji mimba.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Ofisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), David Kafulila, alisema kutokana na kitendo cha serikali kuridhia itifaki hiyo haina budi kuwaomba wananchi radhi.

Kafulila alisema, CHADEMA inapinga uamuzi huo kwani inaamini kuwa uhai wa binadamu ambao unaanza katika mimba, mamlaka pekee ya kuuondoa ni Mungu wala si binadamu.

“Katika misingi ya itikadi yetu, ibara ya 3.1.8 CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu ya jamii. Utoaji mimba unahatarisha nafasi ya uhai wa mtoto kama nguzo mojawapo ya familia,” alisema.

Aliongeza kuwa haki ya mama haipaswi kuvunja haki ya mtoto, kwani itifaki hiyo ya utoaji mimba inahujumu haki ya maisha ya watoto.

Akizungumzia hilo, Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema, suala la utoaji mimba linatakiwa liwe chaguo la mwisho baada ya njia nyingine kushindikana.

Nkya alisema, kwa sasa, matukio ya ubakaji yameongezeka kwani hata mabinti wadogo wanabakwa na hivyo kupata mimba ambazo hawakuzitarajia; na ambazo si sahihi kutokana na umri na matakwa yao.

Alisema kama sheria zamani ilikuwa inazuia suala hilo, katika zama hizi za sasa ambapo kuna tatizo kubwa la ubakaji, taifa linahitaji mjadala mkubwa.

Wakati huo huo, baadhi ya wanawake jijini Dar es Salaam, wametoa maoni mbalimbali kuhusu kitendo cha serikali kuridhia mkataba wa haki hizo, ikiwemo kutoa mimba.

Fatuma Hassan, mmoja wa wanawake hao alisema kitendo hicho ni sawa na kuhalalisha dhambi ndani ya jamii, kwani hakuna dini yoyote inayoruhusu kuua.

Alisema endapo sheria hiyo itapitishwa na Bunge, ni wazi vifo vya akina mama wanaotoa mimba vitaongezeka, kutokana na ukweli kwamba hata hospitali za kufanya hayo mambo ndio zitaongezeka kwani watu wanakuwa wamehalalishiwa kufanya biashara ya kutoa watu mimba.

Kwa upande wake mkazi wa Buguruni, Adela Rhani, alikubaliana na kupitishwa kwa sheria hiyo kwa maelezo kuwa sheria inavyobana watu kutoa mimba, kunawafanya wazitoe kwa njia isiyo sahihi.

"Mfano utakuta mtu anaambiwa anywe majani ya chai au anaenda kwenye hospitali za uchochoroni na kuharibiwa njia yake ya uzazai, lakini kama sheria itapishwa watu watakuwa huru kwenda katika hospitali zinazoeleweka.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Susuviri asante kwa changamoto. Kutetea uhai wa wachanga ambao hawajazaliwa hakutegemei tu imani kwa Mungu wetu. Uuaji kwa ksitisha uhai wa kitoto kichanga ni kosa kubwa uwe unamwamini Mungu au humuamini. Ndio maana hata wanyama - mbwa, paka, simba, chui, kuku nk ni wakali sana katika kutetea maisha ya vichanga vyao. Awali niligusia kuwa wengi wanaotoa mimba japo kwa siri hutumia gharama kubwa na mara nyingi ni ili kujirudishia uhuru wao wa kuendelea kustarehe na kufurahia maisha bila kuwajibika kulea. Na wengi wametoa mimba zaidi ya mara moja kwa sababu zilezile. Wale maskini unaowarejea kwenye hoja zako huwa hawamudu hizi gharama na ndo huzaa na kulea na siamini watoto wao wote huishia kuwalaani mama hawa kwa kunusuru uhai wao.

Kwamba mtoto ambaye uhakika wa kumtunza haupo ni haki auawe itatupelekea siku moja kupendekeza watoto wote wanaoonekana hawana matunzo na vilema wakusanywe na kuteketezwa ili kuwaondolea mateso. Yaemekana Idi Amini aliwahiusanya vilema na kuwamwaga ziwa Nyanza. Tuyabariki hayo?

Nashukuru umetambua kazi alofanya mama yako akakupatia msingi wa maisha. Naamini bado ukimuuliza hatakuambia alikuwa na mahitaji yako yote tayari ndipo akaamua kukuzaa bali nia na utayari wa kukutafutia mahitaji alikuwa navyo. Haya yanakosekana kwa wamama wengi wanaoridhia kutoa mimba moja baada ya nyingine.

Jiulize. Iweje wapo wamama wengi wanaojuta hadharani na kuulaani uamuzi wao wa kukubali kutoa mimba?. Kama ulikuwa uamuzi sahihi na wa busara vipi leo uwanyime usingizi? Something seriously wrong here.

Jambotemuv: Nadhani unafikiri ya kuwa mimi ni mshauri mkuu wa utoaji mimba, la hasha, lakini hatuwezi kukataza sheria isipitishwe itakayompa mwanamke haki ya kuchagua.
Unasema wanawake wanaotoa mimba hujuta, ndiyo ni kweli wapo, lakini pia wapo ambao wanasema ilikuwa ni chaguo sahihi na wanakuja kuzaa mtoto mwingine baadaye wakiwa tayari.
Lakini pia ieleweke ya kuwa maamuzi haya ni mazito na ni magumu, lakini ni lazima choice iwepo.
Mi naona kama ni ku-exaggerate na kusema hii ni sawa na kuua mtoto mchanga, kwa nini? kwa sababu sheria inaweza kuweka wazi mimba inakuwa consdiered lini kama uhai wa binadamu (full life). After that, nadhani hata utoaji wake ni hatari. Pia kusema eti taifa itafikia hatua ya kuhalalisha mauaji ya watoto, walemavu etc kwa kweli sikubali hoja hii.
Ni kweli hakuna mzazi ambaye ni 100% ready material wise to take care of the child lakini kisaikolojia wapo wa tu ambao hawakotayari, wanajuta na kuon amtoto ni mzigo, wanawanyanyasa watoto wao kutokana na mawazo potofu, wengine huwafungia majumbani wanapotoka na kuwaacha bila chakula... there is enough horror stories, let me not even talk about post partum depression.
Unfortunately, we human beings are very complicated and that is what makes us unique and interesting! I hope that despite we are not on the same side of the debate, we can agree on this last statement!
 
Jambotemuv: Nadhani unafikiri ya kuwa mimi ni mshauri mkuu wa utoaji mimba, la hasha, lakini hatuwezi kukataza sheria isipitishwe itakayompa mwanamke haki ya kuchagua.

Tatizo kubwa ni kumpa mama uamuzi juu ya maisha ya mtoto. Ni sawa ilivyokuwa enzi za utumwa 'slave master' akiamua kumuuza mtumwa akaishi mazingira hatari zaidi kwa afya yake ilionekana sawa enzi hizo. Yadaiwa wamama watumwa wajawazito waliwahikupasuliwa matumbo yao wakiwa hai ili kuwaonyesha wamama waakiarabu mtoto hukaaje tumboni. Mbele ya jamii hizo hayalikuwa maamuzi sahihi na halali kwa mwenye mtumwa wake. Je yalikuwa halali kwa walengwa wakuu wa maamuzi hayo (watumwa)?

Unasema wanawake wanaotoa mimba hujuta, ndiyo ni kweli wapo, lakini pia wapo ambao wanasema ilikuwa ni chaguo sahihi na wanakuja kuzaa mtoto mwingine baadaye wakiwa tayari.

Hata majambazi waliotumia silaha wakawaua wenye mali zao hujisifu na kufurahia maisha kwa walichoiba wengine wakatoa sadaka makanisani, misikitini, misibani, harusini nk Kwa misingi hiyo tuhalalishe ujambazi?

Lakini pia ieleweke ya kuwa maamuzi haya ni mazito na ni magumu, lakini ni lazima choice iwepo.
Mi naona kama ni ku-exaggerate na kusema hii ni sawa na kuua mtoto mchanga, kwa nini? kwa sababu sheria inaweza kuweka wazi mimba inakuwa consdiered lini kama uhai wa binadamu (full life).

Mimba ikishatungwa huyo ni mtu kamili anakuwa afikie umri wa kujitegemea kwa hatua. Uwezo na busara za kutawala maisha yake wakomaa kadiri akuavyo. Dhamana ya maisha yao imekabidhiwa kimaumbile kwa mama na wanajamii tunapaswa tu kumsaidia kwa kila hali mama huyu kubeba jukumu hilo kiaminifu

After that, nadhani hata utoaji wake ni hatari.

Waonekana sasa hatari kwa mama lakini ulikuwa tayari hatari na batili kwa mtoto

Pia kusema eti taifa itafikia hatua ya kuhalalisha mauaji ya watoto, walemavu etc kwa kweli sikubali hoja hii.

Hukubali tufikie hapo au wadhani haiwezekani? Kwa taarifa zipo mila ambazo mtoto anyewafuata mapacha ni nuksi na anapaswa kutupwa porini ajifie. Kadhalika yasemekana kwenye makabila fulani mtoto alozaliwa kilema aliuawa kwa siri na wakunga.

Ni kweli hakuna mzazi ambaye ni 100% ready material wise to take care of the child lakini kisaikolojia wapo wa tu ambao hawakotayari, wanajuta na kuon amtoto ni mzigo, wanawanyanyasa watoto wao kutokana na mawazo potofu, wengine huwafungia majumbani wanapotoka na kuwaacha bila chakula... there is enough horror stories, let me not even talk about post partum depression.
Unfortunately, we human beings are very complicated and that is what makes us unique and interesting! I hope that despite we are not on the same side of the debate, we can agree on this last statement!

In deed we are complex beings and that's what we were meant to be. Our problems in life are even more complecated such that short cut choices only end up creating more problems for us. Complicated as they are, we often fail to associate such problems with our past wrong choices. Abortion is just one of them
 
Jambotemuv: Nadhani unafikiri ya kuwa mimi ni mshauri mkuu wa utoaji mimba, la hasha, lakini hatuwezi kukataza sheria isipitishwe itakayompa mwanamke haki ya kuchagua.

Kuchagua kuua kwa kutoa mimba unaona ni haki ya msingi? You need a prayer my friend. Haki gani hiyo ya kuchagua kuondoa uhai wa mwanadamu asiyenauwezo wa kufanya maamuzi yake mwenyewe na asiye na makosa yoyote. It's just wrong.

Unasema wanawake wanaotoa mimba hujuta, ndiyo ni kweli wapo, lakini pia wapo ambao wanasema ilikuwa ni chaguo sahihi na wanakuja kuzaa mtoto mwingine baadaye wakiwa tayari.

Huh!? Those who say it was the right choice don't have a heart. They have a stone instead! Unbelievable!

Lakini pia ieleweke ya kuwa maamuzi haya ni mazito na ni magumu, lakini ni lazima choice iwepo.

..And that choice should be life. That's the bottom line.

Mi naona kama ni ku-exaggerate na kusema hii ni sawa na kuua mtoto mchanga, kwa nini? kwa sababu sheria inaweza kuweka wazi mimba inakuwa consdiered lini kama uhai wa binadamu (full life). After that, nadhani hata utoaji wake ni hatari. Pia kusema eti taifa itafikia hatua ya kuhalalisha mauaji ya watoto, walemavu etc kwa kweli sikubali hoja hii.
Ni kweli hakuna mzazi ambaye ni 100% ready material wise to take care of the child lakini kisaikolojia wapo wa tu ambao hawakotayari, wanajuta na kuon amtoto ni mzigo, wanawanyanyasa watoto wao kutokana na mawazo potofu, wengine huwafungia majumbani wanapotoka na kuwaacha bila chakula... there is enough horror stories, let me not even talk about post partum depression.
Unfortunately, we human beings are very complicated and that is what makes us unique and interesting! I hope that despite we are not on the same side of the debate, we can agree on this last statement!

I get the feeling you are not even in support of abortion, or do you Susu?
 
The Didache (also known as "The Teaching of the Twelve Apostles") dates from the first half of the second century CE. It states: "Thou shalt not murder a child by abortion." (2:2) It also says that "The Way of Death is filled with people who are...murderers of children and abortionists of God's creatures." (5:1-2)
 
Pope Stephen V (served 885-891) wrote in 887 CE: "If he who destroys what is conceived in the womb by abortion is a murderer, how much more is he unable to excuse himself of murder who kills a child even one day old." "Epistle to Archbishop of Mainz."
 
Pope Sixtus V (1471-1484) issued a Papal bull "Effraenatam" in 1588 which threatened those who carried out abortions at any stage of gestation with excommunication and the death penalty.
 
When a delivery goes terribly wrong, and the attending physicians have no choice of Killing the fetus, and saving the life of the woman, let doing nothing, allowing nature to take its course, and watching both the woman and fetus die.
 
Barnabas: "You shall not kill either the fetus by abortion or the new born" (Letter of Barnabas, circa 125)
 
"...we are not permitted, since murder has been prohibited to us once and for all, even to destroy ...the fetus in the womb. It makes no difference whether one destroys a life that has already been born or one that is in the process of birth."
 
Ukatembelea China na kuona kwa jicho lako jinsi watu wengi inavyoweza kua kikwazo kikubwa kwa miundombinu, ardhi, nk ni dhahiri wanaopinga abortion wange badilika. Mimi naunga mkono abortion, na aliyeamua kuzaa na basi azae wakati mwafaka.
Visihusishwe dini/utu na uhalali wa abortion bali tuhusishe uzazi na uchumi/hali halisi pamoja na afya.
Tumeshuhudia kitoto na mama wanakufa kwa kukosa chakula, Dar, abortion ingemsaidia sana mama/mtoto maana mama alipata mimba katika jitihada ya kujipatia mlo wa siku kwa kutumia mwili wake. Ikisaidiwa na condom, night pill(a month contraseptive pills)/morning pill(after sex)? pia ni vema zikapatikana kwa wingi na kwa bei poa.
 
Back
Top Bottom