Serikali yaridhia umeme kupanda Kuanzia January 2014!

Status
Not open for further replies.
Wakati wa kipindi cha uongozi wa Mh. Mkapa sekta ya umma ili undergo mabadiliko makubwa. Makapa alianzisha programu maalumu aliyoiita Public Service Reform Programme. Programme hii ilikuwa na mambo mengi mazuri ambayo yalilenga kutransform utumishi wa umma kuwa more effective na efficient. Baadhi ya mambo yaliyoanzishwa kwa kipindi hiki ni kamaifuatavyo;

1. Kuanzisha mpango wa ku-outsource baadhi ya huduma zisizo za msingi (Outsourcing of non-core activities). Katika mpango huu shughuli za ulinzi na usafi zikaanza kuwa outsourced. Zamani mawizara yalikuwa na walinzi walioajiriwa na wafanya usafi. Hali ya usalama na usafi katika mawizara ilikuwa inatisha. Kuoutsorce shughuli hizi kulilenga kuboresha huduma za usafi na ulinzi na pia kupunguzia watendaji jukumu la kusimamia moja kwa moja HR wanaohusika na kazi hizo. Ulinzi na Usafi ilikuwa ni kwa kuanzia. Ila shughuli nyingi zaidi zilitegemewa kuwa outsorced kulingana na mahitaji na mafaniko. Hata hivyo baada ya mkapa kumaliza kipindi chake hakuna tena kilichoendelea kuhusiana na hilo swala na hali imebaki palepale mkapa alipopacha.

2.Eneo la pili ambalo lililengwa ni kuondoa urasimu na ukiritimba wa shughuli za usimamizi wa sheria mbalimbali na utoaji lesenina vibali mbalimbali. kabla ya hapo shughuli zote hizo zilikuwa zinafanywa na idara mbalimbali za Wizara husika. Likaja wazo la kuunda vyombo ambavyo ni semi-autonomous, ambavyo vitafanya shughuli hizi. Hasa ukizingatia uchumi ulikuwa unakua kwa haraka na mazingira ya biashara yalihitaji kuboreshwa. Hapo ndo vyombo kama TRA, TCRA, EWURA, SUMATRA, TEMESA n.k vilianzishwa. uanzishwaji wa wakala na mamlaka mbambali mbali ulitakiwa uende sambamba na upunguzwaji wa Idadi ya Wizara. Kwa kuwa kazi hizi za usimamizi wa sheria zilikuwa zinahamishwa kutoka katika wizara kwenda ama kwa mamlaka au wakala, wizara zisingeendelea kuwa kama zilivyo. Baadhi ya watumishi walihamishiwa kwenye taasisi hizo mpya na vile vile wizara zilitakiwa kupungua hadi kubaki 15 tu. Baada ya Mkapa kuondoka JK siyo tu akaongeza idadi ya Wizara lakini hata ukubwa wa mawizara ukaongezeka. Wakaanzisha kurugenzi mpya na wakurugenzi wasaidizi kibao ambao hata kazi hawana, wanaishia kusoma magazeti tu. Kitu kingine ambacho hakikwenda sawa ni katika kuangalia vyanzo vya mapato vya hizo taasisi mpya. Ila tukubali tu zimesaidia katika kuratibu na kusimamia biashara mbalimbali, kuweka uwanja sawa wa biashara n.k.

3. Eneo lingine ambal mkapa alilifanyia marekebishao ni upelekaji wa madara Wilayani. Hata hivyo aliacha kazi hii iko nusu na Hadi leo haikuendelea tena. Bado serikali kuu imeng'ang'ania madaraka kibao. Huwenda kama hili lingefanikiwa, hata CHADEMA wasingekuwa na haja ya kuwa na sera ya majimbo. Maana wilaya zingekuwa na uhuru wa kukusanya mapato mengi na kutumia katika miradi ya maendeleo mbalimbali.

Hiyo ndo historia ya hivi vyombo kwa ufupi. Kutokana na kutokuwa na vision, utawala wa sasa haufanyi au kuendeleza mabadilko ya msingi ya uchumi unaokua.
 
inatia huzuni sana kila mara kwa nchi yetu gharama za umeme zinapanda na tena kwa kiwango kikubwa tu ukilinganisha na hali halisi ya maisha ya watanzania, lakini mara zote EWURA ambayo inasimamiwa na watanzania hao hao waliotoka katika mikono ya kimaskini kupita kiasi imekuwa kimya ikiwaruhusu Tanesco kupandisha bei ya umeme bila hata kufikiri mara mbili.

Na hakika kama mamlaka ya nishati na maji EWURA, wangekuwa na uzalendo wa taifa hili na hasa kwa kuzingatia tamthini za kitaalamu dhidi ya hali ya umaskini wa kipato walionao watanzania, wasingewaruhusu TANESCO kupandisha bei ya umeme kila mara.

Nina mashaka pia kama tathmini inayofanya inazingatia utafiti wa kweli wa hali halisi ya kipato cha wananchi watumiaji wa umeme, kila siku watanzania wanabebeshwa mzigo wa gharama hizi za umeme.

nina mashaka pia na hata na uwezo wa watendaji wa hiki chombo, na pengine hata kisiwepo hapa nchini.

maana haina maana ya nchi kuwa na chombo kama hiki, ambacho hakithamini watanzania walipa kodi wanaoteseka na ugumu huo wa maisha.
 
ewura imekaa kiulaji zaidi, pengine wana pasenti inayopanda pale umeme unapopanda
 
Ewura sio chanzo cha tatizo.Tatizo ni mfumo wa uzalishaji wa nishati ya umeme.Ewura anatumia formula alizopewa na wafuaji umeme,amboa ni makampuni yenye uwezo mdogo wa kufua umeme kwa gharama halisi au ni milango ya kifisadi.Wakulaumiwa ni serikali iliotia mikataba na vikampuni uchwara bila kuzingatia maslahi ya mtumiaji.
 
Brazil watu wameandamana kwa nauli ya mabasi tu kupanda,.. Sisi tunalalamika pembeni tu.
 
Kwa kweli inasikitisha sana. Nilinunua umeme wa 30,000/= na baadhi ya taarifa zilizopo kwenye risiti ni hizi (ningeweza kui-scan na ku-upload lakini kwa sababu zilizo wazi sitafanya hivyo):-

NYONGEZA: TZS30,000.00
AMOUNT (VAT+1%): 19070.16 (4195.44)
ENERGY RECEIVED: 62.30KWHR
RECEIPT NUM: *SIRI*
METER NUM: *SIRI*
.......
SRV CHGR (VAT): 5520.0 (1214.4)

Piga hesabu uone kiuhalisia uniti moja ni shilingi ngapi?
 
Hii maana yake nini? Mlaji anakatwa VAT mara mbili kwa manunuzi yale yale; anakatwa kwenye manunuzi ya umeme wenyewe na anakatwa kwenye service charge. Sijaelewa, naomba wataalamu wa uchumi watusaidie kwenye hili.
 
inatia huzuni sana kila mara kwa nchi yetu gharama za umeme zinapanda na tena kwa kiwango kikubwa tu ukilinganisha na hali halisi ya maisha ya watanzania, lakini mara zote EWURA ambayo inasimamiwa na watanzania hao hao waliotoka katika mikono ya kimaskini kupita kiasi imekuwa kimya ikiwaruhusu Tanesco kupandisha bei ya umeme bila hata kufikiri mara mbili.
Na hakika kama mamlaka ya nishati na maji EWURA, wangekuwa na uzalendo wa taifa hili na hasa kwa kuzingatia tamthini za kitaalamu dhidi ya hali ya umaskini wa kipato walionao watanzania, wasingewaruhusu TANESCO kupandisha bei ya umeme kila mara.
Nina mashaka pia kama tathmini inayofanya inazingatia utafiti wa kweli wa hali halisi ya kipato cha wananchi watumiaji wa umeme, kila siku watanzania wanabebeshwa mzigo wa gharama hizi za umeme.
nina mashaka pia na hata na uwezo wa watendaji wa hiki chombo, na pengine hata kisiwepo hapa nchini.
maana haina maana ya nchi kuwa na chombo kama hiki, ambacho hakithamini watanzania walipa kodi wanaoteseka na ugumu huo wa maisha.
Hao EWURA sisi wananchi tunapaswa kuwauliza maswali machache ili watujibu tujiridhishe kama kweli chombo hicho kipo kwa maslahi ya TANESCO kwa upande mmoja na watumiaji umeme kwa upande wa pili.

Swali la kwanza, ni kwa nini EWURA inaitisha vikao ambavyo huwa inadai, ni vya kusikiliza maoni ya watumiaji umeme, sasa huwa inatumia kigezo gani kupandisha bei hiyo ya umeme, wakati zaidi ya asilimia 95 ya watoaji maoni hayo huwa wanapinga nyongeza, sisi wananchi tukiwaambia kuwa vikao hivyo, huwa wanviitisha kama danganya toto, tutakuwa tumekusea?!

Swali la pili, iwapo EWURA walimsikia Mkurugenzi mkuu wa TANESCO, Falchsemi Mramba, akikiri kwa kinywa chake mwenyewe, na kukaririwa na vyombo vya habari kuwa wanawadai wadeni wao sugu, wengi wao zikiwa Idara na Taasisi za serikali, zaidi ya shilinfgi bilioni 233, sasa ni kwa nini EWURA haiwaulizi TANESCO sababu zao za kushindwa kuwakatia umeme Idara hizo na Taasisi hizo, wakati ianaeleweka wazi kuwa kila mwaka Idara hizo na Taasisi hizo zinatengewa mafungu maalum katika bajeti ya nchi hii, zikiwa ni pesa zetu walipa kodi?!

Swali la tatu, ni kwa nini EWURA inaendelea kubariki mtindo wa TANESCO wa kuwapa umeme wa "dezo" wafanyakazi wake zaidi ya elfu 5 nchi nzima, kila mmoja uniti 750 kwa mwezi, wakati wakijua fika kuwa, gharama hizo za umeme wa dezo wa "staff" wa TANESCO unafidiwa na sisi wananchi wengine, tuliopandishiwa umeme?!

Swali la nne, ni kwa nini TANESCO haitoi kipaumbele kwa vyanzo vingine vya umeme wa bei rahisi, kama vile vya mtambo wa Kiwira, unaotumia makaa ya mawe, wenye uwezo wa kuzalisha kuzalisha megawati 400, badala yake inang'ang'ania umeme aghali wa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia mafuta ya akina Symbion, Aggreko na IPTL?!

Ni vyema EWURA wakajitokeza na kutujibia maswali haya, ili tujiridhishe kuwa kweli chombo hicho kipo kwa ajili ya maslahi ya pande mbili ambazo ni upande mmoja ni wa wazalishaji wa umeme na upande wa pili ni watumiaji wa umeme huo
 
inatia huzuni sana kila mara kwa nchi yetu gharama za umeme zinapanda na tena kwa kiwango kikubwa tu ukilinganisha na hali halisi ya maisha ya watanzania, lakini mara zote EWURA ambayo inasimamiwa na watanzania hao hao waliotoka katika mikono ya kimaskini kupita kiasi imekuwa kimya ikiwaruhusu Tanesco kupandisha bei ya umeme bila hata kufikiri mara mbili.
Na hakika kama mamlaka ya nishati na maji EWURA, wangekuwa na uzalendo wa taifa hili na hasa kwa kuzingatia tamthini za kitaalamu dhidi ya hali ya umaskini wa kipato walionao watanzania, wasingewaruhusu TANESCO kupandisha bei ya umeme kila mara.
Nina mashaka pia kama tathmini inayofanya inazingatia utafiti wa kweli wa hali halisi ya kipato cha wananchi watumiaji wa umeme, kila siku watanzania wanabebeshwa mzigo wa gharama hizi za umeme.
nina mashaka pia na hata na uwezo wa watendaji wa hiki chombo, na pengine hata kisiwepo hapa nchini.
maana haina maana ya nchi kuwa na chombo kama hiki, ambacho hakithamini watanzania walipa kodi wanaoteseka na ugumu huo wa maisha.

Tatizo ni sisi WATANZANIA. Hivyo vingine vyooooooote ni mbaazi kusingizia jua. Walishaona sisi ni kama minyumbu ya Manyara national park huwa tunaafuta na kukubali kila tunachoambiwa bila ku-react! Hukusikia kuna nchi serikali zinaondololewa kwa kupandika bei hata ya mkate tu? Lakini hapa kwetu unakuta mtu kakaa anasema ''movie ndio imeanza yangu macho'' au ''mimi natumia kibatari hivyo inawahusu wenye umeme'' (asijue hata yeye ataathirika)
 
Mkuu hiyo siyo jokes! Huo ndo mpango mzima! Hata Prof Muhongo kuwekwa pale haikuwa zali lake! Ule ulikuwa mpango mkakati uliosukwa na sasa unatekelezwa via EHM wao Muhongo et al...Symbion are here to stay kama CCM itaendelea kukaa madarakani...tegemea kifo cha TANESCO soon...

Sala zetu Mungu amazisikia!
 
Mkuu naomba niongezee kwenye mapendekezo yako kwamba ili kuondoa hali hii
rasimu ya katiba iliyopendekezwa na mzee warioba na wenzake ndo mpango mzima
yaani madaraka ya rais yapunguzwe hasa kwenye uteuzi wa wakuu wa taasisi za kiufundi kama EWURA
kama tukicheka na nyani mahindi tutaishia kuyaangalia kwenye TV,tusahau kuvuna ya kwetu.
Watanzania lazima tuchukue hatua kwa kutumia nguvu ya kura zetu,hapo tutaweza kujikomboa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom