Serikali yaridhia umeme kupanda Kuanzia January 2014!

Status
Not open for further replies.

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
199,440
2,000
Previously:
Serikali kupitia EWURA imebariki umeme kupanda bei, ambapo ghrama za umeme zitapanda kuanzia januari moja, wateja wanaotumia umeme unit 60 kwa mwezi wataanza kununua unit moja shilingi mia badala ya shilingi 75

Kwanini EWURA haimlindi mlaji katika suala zima la Nishati?

Katika kutetea maamuzi yake ya kwanini bei za nishati ya umeme ziilizopendekezwa na TANESCO zipande maradufu kwa watumiaji wa kati huku watumiaji wakubwa wakipewa haueni, EWURA walitumia maelekezo ya barua ya Waziri wa Nishati kutekeleza maamuzi yao. Haya ni mashinikizo ya kisiasa kwa masuala ya kitaalamu.

Nilichojifunza kwa haraka-haraka ni kuwa pamoja na lengo la kuundwa EWURA kilikuwa chombo kinachopaswa kutekeleza majukumu yake kwa kujitegemea na na bila ya kuingiliwa na wanasiasa sasa inavyoonekana kuwa wataalamu walioajiriwa hapo ni picha tu na taasisi hiyo nyeti inaendeshwa na wanasiasa tu.

Hii ndiyo inasababisha maamuzi yake kulenga kuwanusuru wanasiasa ambao uchu wao wa madaraka na mali ndiyo hutubebesha mizigo mizito raia ambao hatia yetu aidha ni kuwachagua kishabiki au kuvumilia bila ya kulalamika wakati kura zetu wanaziiba na kuhalalisha kuendelea kutudhulumu.

Ukiangalia muundo mzima wa EWURA utaona haina ubavu wa kufanya maamuzi ya kitaalamu kwa sababu zifuatazo:-

a) Bodi yao ya wakurugenzi huteuliwa kwa sababu za kisiasa na mara nyingi huwa Raisi huteua Mwenyekiti kama zawadi au kumziba mdomo mwanasiasa au mtendaji serikalini asilete chokochoko na matunda yake ni kuwa mwenyekiti huyo anapokutana na wajumbe wa Bodi yake ambao nao ni matunda ya kujuana huwa ni kutoa takrima kwa waziri/Raisi ili aendelee kuwateua nao wale! Katika mazingira ya namna hii kamwe tusitegemee Bodi inayotekeleza majukumu yake kitaalamu bali tutegemee Bodi ambayo inatekeleza majukumu yake kisiasa tu.

b) Sifa za uteuzi wa wajumbe wa Bodi huwa ni siri ya mteuzi na kamwe mchakato husika hauwahusishi watanzania wote katika kutafuta wenye sifa ya kuisimamia taasisi ya umma na hivyo kugeuza uongozi na ushiriki katika uongozi kuwa ni miliki ya viongozi wa juu serikalini badala ya mabosi ambao ni wapigakura! Katika khali hii, tunaishia kuwakilishwa na makapi ambayo hayawajibiki moja kwa moja kwa umma.

c) Kutokana na mapungufu ya kimuundo taasisi nyingi za umma zimeshindwa kukidhi mahitaji ya wananchi wa kawaida na EWURA haiwezi kuwa vinginevyo kwa sababu hata uteuzi wa watendaji wa ngazi za juu ndani ya taasisi za umma huzingatia utashi wa kisiasa na hivyo siyo wa kitaalamu na hivyo kuwa ni mzigo mkubwa wa kiuendeshaji.

d) Gharama kubwa za kiuendeshaji wa mashirika ya umma kama ya TANESCO na EWURA hutupiwa walaji huku walaji wakiwa hawanufaiki ipasavyo na taasisi hizo. Matokeo yake ni kuwa maamuzi mengi huwa ni kuwanufaisha viongozi badala ya wananchi wa kawaida na hii ni baadhi tu ya mifano:-

1) Katika maamuzi ya kuingiza mafuta kutoka nje EWURA ilipigia debe uagizaji wa jumla ambao sasa upo mikononi mwa wafanyabiashara wakubwa wachache na hivyo kuua kabisa ushindani. EWURA walidai ya kuwa kwa kuua ushindani kungeleta ufanisi , ubora wa bidhaa na punguzo la bei ingawaje tangia mfumo huu wa “bulk suppliers” uanzishwe bei zimekuwa zikipanda kiholela na hata ilifikia EWURA wenyewe kuwekwa kibindoni na wafanyabiashara hao!

2) Kutokana na bei ya mafuta kushindwa kuthibitiwa na EWURA gharama za uzalishaji wa umeme pia zimepanda na kuwa mzigo kwa wanannchi wasio na hatia. Zipo hisia kali kuwa “bulk supply” ni utaratibu unashinikizwa ili kujaza mifuko ya wakubwa ambao wamejijengea mazingira mazuri ya kukusanya ulaji tu na wala siyo kwa sababu ambazo tumekuwa tukielezewa.

3) TANESCO imekuwa na gharama kubwa za kiuendeshaji kwa sababu ya wizi na ubadhirifu unaoendelea ndani ya shirika hilo. Gharama hizi husababishwa na mikataba ambayo ni ya kiulaji na mara nyingi ni mashinikizo ya wakubwa serikalini na hivyo kuchangia mashinikizo ya kupandisha bei za umeme na hivyo mzigo kwa mlaji.

4) EWURA katika kuhalalisha bei mpya wameshindwa kujibu maswali ya kimsingi yakiwemo ni nani awajibike kwa gharama za mikataba mibovu na utoaji zabuni usiozingatia mahitaji halisi ya soko. EWURA walikimbilia kutukumbusha madeni ya TANESCO bila ya kutuelezea yamesababishwa na nini na kwanini hayalipiki kama kweli TANESCO inafanya biashara kulingana na nguvu za soko.

5) EWURA wamekwepa kujibu maswali ya kimsingi ya kwanini wanasema mlaji mdogo matumizi yake kwa mwezi ni units sabini na tano tu ambazo hazizingatii kabisa mahitaji halisi ya matumizi ya mwanadamu. Familia ya kawaida ya watu wanne hutumia units 450 kwa mwezi sasa wao hizo units sabini na tano wanazitoa wapi? Kwa siku familia moja huhitaji units 15 kwa kupikia na kuwasha taa 6 kwa masaa manne kwa siku. Units sabini na tano ambazo ni wastani wa units 2.5 kwa siku hazitoshi kupikia achilia mbali kuwashaa taa usiku. Huyo mlaji wa chini kabisa anapikia kuni na kuharibu mazingira au yukoje? Tena wasivyo na adabu, EWURA wanadai viwango vyao vipya vimemjali mlaji mdogo vijijini na mjini kwa kupewa ahueni ya units 2.5 wakati matumizi halisi ni units 15 kwa siku. Hivi kwa utani-utani wa kiwango hiki mradi wa umeme vijijini ni kusambaza nguzo tu zionekane au kweli lengo ni wanavijiji walengwa kweli wazitumie?

6) Ikumbukwe Mkapa wakati wa enzi zake aliwahi kuwaleta
wasauzi na alitumia khoja za madeni ya TANESCO bila ya kujibu khoja ya msingi ni nani anayasababisha na EWURA inaendeleza nyimbo zilezile kuhalalisha wananchi kuumizwa na bei ambazo zitapanda kila mwaka hadi itakapofikia hatua watumiaji wadogo watakapojitoa na kutafuta mibadala mingine. Madeni ya TANESCO yamezwe na serikali kuu kwa sababu ndiyo chanzo cha kushindwa kuyalipa, period!

7) Katika hali inayoleta ubaguzi ambao misingi yake haina maelezo, EWURA imemkandamiza mtumiaji anayehitaji nishati kwaajili ya kupikia na hivyo kutopunguza kasi umalizaji wa miti kwa matumizi ya kuni za kupikia! Sielewi sababu za watumiaji wa kati kuwapatia ruzuku watumiaji wakubwa. Kilichotakiwa kufanyika ni bei iwe moja na kama ni upendeleo utolewe kwa wote.

8) Wakati majuzi nishati ya umeme ilipopotea tulielezwa walikuwa wanasafisha visima vya gesi na ya kuwa sehemu kubwa ya uzalishaji wa umeme ulikuwa unafanywa na gesi badala ya maji au mafuta lakini hadi leo inapokuja sababu za kupandisha gharama za umeme khoja hizo hutupiwa virago vyake na
khoja za mwaka arobaini na saba kutumiwa kudai gharama za ununuzi wa mafuta zimepanda na hivyo kusababisha umuhimu wa kupandisha bei za umeme. Ukweli uko wapi sehemu kubwa ya uzalishaji ni gesi au mafuta? Tumevumilia uwongo wa kila aina kuhusiana na hii sekta ya nishati na hata ukweli haujulikani ulipo!

MAPENDEKEZO

1) Ili kuongeza uwajibikaji kwa wananchi taasisi zote za umma zinapaswa kubadilisha muundo wa Bodi zao za wakurugenzi ili kupunguza siasa katika uendeshaji wa Bodi hizo na kuzifanya ziwe huru zaidi katika kufanya maamuzi yao.

2) Mfano EWURA Bodi ya wakurugenzi iwe na uwakilishi wa moja kwa moja wa theluthi moja ya walaji na theluthi moja ya wazalishaji wa nishati na theluthi moja wa warasimu ambao waziri atawateua kulingana na umuhimu wao kwenye sekta hii. Walaji na wazalishaji kupitia vyama vyao wawachague wawakilishi wao moja kwa moja na hivyo kupunguza Bodi yenye kukidhi mahitaji ya muda mfupi ya waziri na Raisi husika na hivyo kuwa na msisitizo kwenye mahitaji endelevu ya sekta ya nishati. Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ufanywe na wajumbe wa Bodi badala ya Raisi. Wajumbe wa Bodi waongozwe na mjumbe ambao wao wanaona anasifa za kuwaongoza badala ya kuongozwa na mashinikizo ya kisiasa ambayo madhara yake ndiyo kubebeshwa mizigo ya wanasiasa.

3) Pamoja na jitihada za kisera za kulivunja TANESCO kama mapungufu ya kimuundo wa Bodi hayatashughulikiwa kama ninavyopendekeza basi tutegemee uozo na gharama za kiuendeshaji kupanda mara tatu ili kuwapa ruzuku viwavi jeshi ambao watakuwa wamejipanga kwenye taasisi hizo mpya.

4) Huko tuendako tusitarajie bei za umeme kushuka bali kupanda kwa sababu mtazamo wa kisera wa uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa umeme unatilia mkazo wazalishaji wakubwa. Sera ambayo italeta ahueni kwa walaji wa aina zote siyo kuisambaratisha TANESCO tu bali kuweka sera za muuzaji wa nishati ya umeme kununua umeme kwa wazalishaji wadogo wadogo ambao watauzalisha kwa kutumia jua na upepo ambazo ni nishati endelevu. Kwa mfano kama sera hii ingelikuwepo ungeona wawekezaji wengi wadogo-wadogo badala ya kuwekeza katika ujenzi wa nyumba za kupanga wangeliwekeza kwenye uvunaji wa nishati endelevu tajwa na hivyo kujihudumia wao na naksi ya ziada kuwauuzia TANESCO.

 

ha ha ha

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
638
195
Ngoma inogile, nchihii kume sio maskini tena.

Watu wake watatoa wapi ela za huo umeme kama sio washaona ela zipo na hazina kazi????:lock1:
 

tusichoke

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
1,313
1,250
Kodi Simu juu, umeme juu haya ndio maisha bora Kwa kila mtanzania na tutashuudia mengi kabla ya 2015 lazima tuwachangie watu
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,042
2,000
Na mishahara itapanda lini!? ili kuwawezesha Watanzania kukidhi gharama za juu za maisha!? Bila mshikamano wa dhati wa Watanzania kupinga gharama kubwa za maisha zinazosababishwa na ufisadi wao na mishahara midogo Serikali hii dhalimu itaendelea kuwaumiza Watanzania kwa kila namna.
 

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,280
2,000
EWURA imebariki umeme kupanda bei,ambapo ghrama za umeme zitapanda kuanzia januari moja,wateja wanaotumia umeme unit 60 kwa mwezi wataanza kununua unit moja shilingi mia badala ya shilingi 75
sosi:ukurasa wa fb wa eatv

Acha upande kwa nini upande tu!!
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Serikali imeridhia TANESCO kupandish bei ya umeme kwa watumiaji wadogo vijijini kwa 40%, na kwa watumiaji wa kati bei imepanda kwa 85% kuanzia Januari 2014, hali hii inatisha sana, Je EL hauhusiki na hili sakata la bei ya umeme??

Maana tangu Richmond bei imekuwa ikipanda kumudu matumizi ambayo yanatokana na kulipa mikataba mibaya ulioshinikiza TANESCO na Serikali kuingia, Unatuua MZEE kwa michango yako ya harambeee, pesa si ndo hizi tunawalipa???

Nawasilisha
 

realleonia

JF-Expert Member
May 25, 2013
364
250
Hivi kweli hawa viongozi wetu wanajua ugumu wa kupandisha umeme na simu yaani mizigo yote unabeba mwananchi hii noma.
 

samora10

JF-Expert Member
Jul 21, 2010
7,533
2,000
Uzuri wanaoumia ndio hao hao wanaodanganywa na khanga na kofia za rangi ya kijani... Nasema wapandishe tu
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom