Serikali yaridhia sekta binafsi kuzalisha na kusambaza umeme!


nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
81
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 81 145
na Grace Macha, Arusha

KATIKA kukabiliana na tatizo la ukosefu wa umeme wa uhakika nchini, serikali imekusudia kufanyia marekebisho sheria ili kuwaruhusu watu na taasisi binafsi kuzalisha na kuzambaza umeme bila kuupitishia Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO).

Hayo yalisemwa jana jijini Arusha na Waziri wa Fedha na Uchumi , Mustafa Mkulo, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Bilali, kufungua mkutano wa 20 wa magavana wa nchi za Afrika, unaojadili tatizo la ajira kwa vijana na matumizi ya fedha za maendeleo zinazotolewa na wafadhili.

Alisema kuwa sheria hiyo itapelekwa bungeni kwenye kikao cha Novemba ambapo kama wabunge wataridhia mabadiliko hayo, yatawezesha umeme kusambazwa maeneo mengi hasa ya vijijini jambo litakalosaidia kupunguza wimbi la vijana kukimbilia mijini kutafuta ajira kwani wataweza kuendesha shughuli za kujiajiri.

"Kuna taasisi na kampuni ambazo zinazalisha umeme wao na mwingine mwingi wa ziada unabaki lakini wanashindwa kuusambaza hata kwa majirani zao kutokana na sheria ya sasa hairuhusu lakini tukibadilisha sheria ya sasa, wengine watajitokeza kuzalisha na kusambaza kwa wananchi hivyo kupunguza tatizo, " alisema Waziri Mkulo.

Alisema kuwa tatizo la ajira kwa vijana lililopo barani Afrika na hapa nchini linaweza kutatuliwa endapo kutakuwa na mkakati wa pamoja kuhakikisha kuwa vijana hao wanapatiwa elimu ya kuwawezesha kujiajiri mara baada ya kumaliza masomo, badala ya kusubiri kuajiriwa, hivyo alivitaka vyuo vikuu kuhakikisha vinabadili mtazamo na kutoa elimu itakayowawezesha vijana kujiajiri mara baada ya kuhitimu mafunzo.

"Kwenye bajeti ya mwaka huu tumeitengea fedha nyingi Wizara ya Elimu na Mafunzo ili iweze kuboresha vyuo vya ufundi stadi (VETA) pamoja na SIDO (Shirika la Viwanda Vidogo) ili kutoa mafunzo ya ufundi kwa vijana yatakayowawezesha kujiajiri," alisema Waziri Mkulo.

Katika kuwahakikishia soko la bidhaa zinazozalishwa na vijana kupitia ufundi, alisema kuwa serikali ilishapiga marufuku watendaji wake kuagiza samani kutoka nje ya nchi na badala yake wanunue zile zinazotengenezwa hapa nchini lakini wanunue zilizo na ubora unaokubalika.

Aidha aliwataka wananchi wenye uwezo kujitokeza kuliendesha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ubia na serikali katika kutekeleza sera ya ushirikiano wa sekta binafsi na umma (PPP) ili kuongeza ajira hasa kwa vijana, huku akisisitiza kuwa jina halitabadilishwa.
 
S

superfisadi

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2009
Messages
553
Likes
3
Points
35
S

superfisadi

JF-Expert Member
Joined May 22, 2009
553 3 35
itakuwa nafuu jamani wawekezaji jitokezeni , wa kuzalisha kwa upepo haya wa kuzalisha kwa maji haya yaani kila mwenye teknolojia , welcome
 
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,559
Likes
5,068
Points
280
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,559 5,068 280
Wamebana mwisho wameachia!
 
Rweye

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Messages
16,175
Likes
3,952
Points
280
Rweye

Rweye

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2011
16,175 3,952 280
Hii ikianza itasaidia kuwaamsha tanesco kutoka kwenye usingizini
 

Forum statistics

Threads 1,237,166
Members 475,465
Posts 29,280,118