Serikali yarejesha uwanja wa KIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yarejesha uwanja wa KIA

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Democrasia, Sep 15, 2009.

 1. Democrasia

  Democrasia Member

  #1
  Sep 15, 2009
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 80
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wakuu poleni na kazi, kuna habari ambazo naamini kuwa ni rasmi ni kuwa uwanja wa ndege wa KIA umerudi serekalini.

  Hii nadhani ni baada ya watu kushikilia bangu kodi kidunchu iliyokuwa ikilipwa serekalini yaani US$ 1,000 KWA MWAKA wakati income per day was is around TSH 20,000,000
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Je hela zetu anaondoka nazo? ie the difference between what he was paying and what he was getting assuming the lease was for ten years in maana anaondoka na zaidi ya shs 71,200,000,000/=.

  aliyenegotiate na kuapprove mkatabaa naachiwa tu hivihivi,mbona liyumba aliyejenga Twin Towe ambacho ni na kitu tangible kinaonekana kinatumika anasota rumande na huyu anaachiwa tuu.

  Msokoto wa bangi jela miezi 12, kuiba kuku mmoja kwa ajili ya kuganga njaa kupigwa hadi kufa, karani kuchukua rushwa ya shs 50,000/= kosa litaandikwa kwenye magazeti yote tanzania huyu bwana anaondoka na hela zetu tunamuangalia tu.

  je mitanzania ( ikiwa ni sehemu ya miafrika) ndivyo tulivyo au wantanzania tuna laana?????

  Dawa yake nini??????


  Lini tutaamka toka usinginzi mzito unaotukabili????
   
 3. Johas

  Johas Senior Member

  #3
  Sep 15, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa! Sio usingizi Mzito tuu, umbumbu,uhoga na kutojiamini katika mchakato mzima wa kusimamia na kupigania haki zetu.
  Ebu! fikilia ingekuwa kwa watani wetu wa jadi (kenya), ingekuwaje?

  Huu, uhuru tuliopata chini ya kivuli ndio matokeo yake haya ya kutokuwa ngangali katika Maslai yetu. Wanatushinda ata wazanzibar!!
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Si kweli uwanja umerudi serikalini. Ila imenunua hisa na kuwa 95% na inatafuta mwekezaji mwingine imuuzie hizo hisa. Uwanja wa KIA ni mzuri sana na pengine baadhi ya sehemu imeuzidi hata wa Nyerere......
   
 5. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizi habari kama ni za kweli basi nitakuwa nafuraha ya muda wa umri wangu. Sijawahi kuona kitu cha kijinga na cha ajabu kama kuukodishia uwanja wa KIA. Tunaofahamu hasara tunayopata kutokana na mkataba huo ni wachache sana. Mimi sitoisha kumpongeza aliyeufikisha huo mkataba mwisho, na ningekuwa na mamlaka ningemsamehi makosa yake yote hata kama anatuhumiwa ufisadi ningemsamehe mara moja.
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Naenda kulala, kiwanja cha ndege chetu, amekaa nacho miaka 10, amepewa bei ya kutupa halafu tunanunua hisa asilimia 95 hisa zipi tena mimi sielewimaumivu ya kichwa yanaanza polepole hedex haifanyi kazi wala diclopar dawa ni kwenda kulala kupunguza hasira.

  Mwekezaji anakuja kufanya kitu gani ambacho sisi hatuwezi, jamani kuendesha uwanja wa ndege tunahitaji wawekezaji, those trolleys, vigari vya mizigo, gari za kubeba kinyesi toka kwenye ndege tunatafuta wazungu. Nyerere alitupeleka shule ili tufanye nini?, tuwe werevu na wenye elimu au wajinga????
   
 7. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Aliyetuingiza katika mktaba huu mbovu ni moja kati ya wana mtandao, hakuna atakachofanywa.
  Lipumba hakuwa mwana mtandao na mbaya zaidi alikuwa anachukua mabibi wa wana mtandao kwani chenji ya wizi alikuwa nayo, hakuona shida kuwanunulia akina dada vitara nyekundu. Ndiyo maana anasota keko.

  Angalia akina Mkapa, Yona, Mramba, Lowasa mpaka leo wanapeta mitaani kama hakuna mabaya waliyotenda.

  Tanzania ni nchi ya watu wachache, akina sisi tupo tupo tu.
   
 8. E

  Eric Yunusu New Member

  #8
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 21, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kidatu nafikiri anayesota Keko siyo Lipumba ni Liyumba
   
 9. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kwamba $ 1000 ni kidogo sana, lakini si ni afadhali analipa hiyo hela serikalini ? Mbona kabla ya hapo serikali ndo ilikuwa inatumia pesa za kodi zetu kuiendesha, na walikuwa wanatengeneza hasara tu.
   
 10. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Tena uwanja ulikuwa unanukaaa! sasa nashindwa kuelewa hii ni laana gani tunayo watz, angalia uwanja wa dar nilipita pale juzi juzi nikapishana na panya. Ngoja tuone utaanza kuonekana vipi baada ya srikali kuuchukua/kununua hizo hisa. Ni miaka miwili tu, wenzetu mlioko karibu pigeni picha za kumbukumbu tuje kulinganisha baada ya muda huo.
  Nadhani kuna mkubwa serikalini anataka kuuchukua kama kile kituo cha mabasi Ubungo. Sehemu za kupatia chenji za kampeni za uchaguzi zimezidi kupungua kwahiyo hiyo si ajabu ni EPA-Kagoda mpya. Lini kituo cha Ubungo kitachukuliwa pia.
   
 11. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Uwanja wa ndege wa kamataifa wa Kilimanjaro,umebinafsisha kwa mwekezaji mmoja;ambaye anailipa serikali kodi ya dola za kimarekani 1000 kwa mwezi.Na mwekezaji huyo analipwa na shirika moja tu la ndege kama KLM dola za kimarekani 5000 kwa mwezi.

  Unaweza kujiuliza tu swali rahisi,je kuna mashirika mangapi ambayo ndege zake zinatua Kilimanjaro International Airport(KIA)?Mimi naamini ni mengi,lakini serikali imekubali kudhulumiwa huku nikiamini wanalijua hilo.Kwasababu,mbunge(Zitto Kabwe) aliomba mkataba huo upelekwe bungeni;cha ajabu waziri mwenye dhamana husika(Zakia Meghji)akamjibu mbunge,haitawezakana kwa madai kwamba mkataba ni siri.

  Lakini ukweli uliopo kwa mujibu wa sheria mkataba unaohusu mali ya umma siyo siri
   
 12. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu!!!!!, tatizo si watanzania wote, bali hao waliopewa dhamana. Katika nchi hii ukitaka usichukuliwe hatua, basi fanya dili kubwakubwa za mabilioni, lakini ikiwa ni dili za visilingi kumi, tegemea miaka 30.
  Mimi naona huku kurudishwa kwa uwanja Mafisadi wameona hizo pesa walizokuwa wanapata hazitushi kwa ajili ya uchaguzi 2010. Wanasema serikali umeuchukua, na baadaye utasikia unahitaji ukarabati, pesa za ukarabati zitachukuliwa serikalini - matumizi ya dharura lakini hazitatumika kwa ajili ya ukarabati bali zitaelekezwa kwenye kampeni.
  Ili kuamini nisemayo, vipi pesa zilizorudishwa toka EPA uliziona au ulisikia tu zimerudishwa na baadaye zikapelekwa Kwa jamaa anaitwa Kilimo kwanza.
  wote waliotajwa hakuna hatammoja aliyetwajwa kuwa ndiye aliyerudisha na amerudisha kiasi gani. "Follow the river and you will find the sea"
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Haya mawazo haya ndo yanatupeleka huko ingawa ni kidogo afadhali kulipwa dola 1,000, sababu kabla erikali ndo ilikuwa inatumia pesazetu za kodi kuiendesha.

  Premise in that sense ingekuea ni nani aliyekuwa anafaidika na hela wakati huo na amefanyiwa nini kama njia ya kumuadabisha kuliko kusema afadhali kidogo.

  Rasilimali zinakwenda na sisi tunaangalia tu hakuna answerabiliky or whatever.

  my GOD
   
 14. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mawazo haya ni mazuri tu (rejea kwa nini socialist economic principles/gvt. takeovers zilivyofeli flat). Tatizo letu watu wanaosimamia mali zetu wanatumia nafasi hizi kuingia mikataba ya ajabu ajabu kwa faida yao - kama huu wa kukodisha $ 1000 kwa mwaka.
   
 15. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Bongo bwana, kila siku kunachomoka mchezo wa kuigiza serikalini. Sasa madhali twaingia 2010 maigizo yatakuja mengi sana kutupofusha macho ili tuamini viongozi wetu sasa wako makini zaidi kustahili kukalia vigoda vyao mara nyingine, hadi wafie kwenye kwenye vigoda hivyo, wakidhani hakuna mwingine kama wao.
   
 16. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ila tunashukuru nyepesi hizo, iwe ni kweli au mchezo wa kuigiza hatujali. Sio lazima tuwape kula tena maana hawashibi watu hawa, hebu wajaribu na wengine.
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
   
Loading...