Serikali yapoteza zaidi ya shilingi bilioni 5.1 kwa uchimbaji haramu wa madini wilayani Handeni

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,604
2,000
mgodi%286%29.jpg


Serikali wilayani Handeni katika kipindi miaka mitatu imepoteza zaidi ya shilingi bilioni 5.1 kufuatia wachimbaji haramu wasiokuwa na leseni kuchimba baadhi ya migodi bila kuwa na leseni hatua ambayo imesababisha kiasi kikubwa cha fedha zitokanazo na sekta ya madini kupotea.

Akizungumza na ITV kuhusu zoezi la makusanyo ya kodi kupitia sekta ya madini,mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amesema serikali imeanza mchakato wa kuwapatia leseni haraka wachimbaji hao kwa sababu baadhi yao wamekuwa wakiingia katika migodi ya wawekezaji wanaolipa fedha nyingi kwa serikali hatua ambayo pia imekuwa ikisababisha migogoro baina ya pande hizo mbili.

Kwa upande wake afisa madini mkazi wilayani Handeni Frank Makyao amesema tayari serikai imetenga eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 32.91 lililopo eneo la Manga wilayani Handeni hivyo amewataka wachimbaji wadogo kujitokeza kuchukua leseni ili kuepuka migogoro baina ya wawekezaji wenye migodi inayolipiwa kodi kwa serikali .

Kufuatia hatua hiyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amewaagiza watendaji wa halmashauri kuhakikisha kuwa wanawadhibiti wachimbaji wadogo wanaofanya kazi hiyo bila kuwa na leseni kisha wakamatwe ili sheria iweze kuchukua mkondo wake huku baadhi ya wachimbaji haramu wakiiomba serikali iwaache katika maeneo ya migodi mikubwa waendelee kujitafutia riziki kwa sababu hawana ajira.

Chanzo: ITV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom