Serikali yapoteza bil. 4/- kwa mwezi kusamehe wawekezaji

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Serikali yapoteza bil. 4/- kwa mwezi kusamehe wawekezaji

na Sheilla Sezzy, Mwanza
Tanzania Daima

HATUA ya serikali kuwafutia wawekezaji wa migodi kodi ya mafuta ya dizeli inaikosesha sh bilioni 4 kila mwezi.
Chanzo chetu cha habari, kinaeleza kuwa mafuta hayo ambayo yanaingia nchini bila ya ushuru yamekuwa yakionekana katika baadhi ya vituo vya mafuta na yanajulikana kutokana na kuwa na utofauti wa rangi.

Njia ya magendo ambayo inatumiwa na wahusika wa migodi hiyo ni kuwa wanaingiza mafuta hayo migodini kwa kuwafumba wananchi macho na kisha yanatolewa kupitia magari makubwa ya mafuta na kuanza kusambazwa kwa wateja ambao wapo katika mikoa ya Mwanza, Kagera, Kigoma, Mara na Shinyanga katika sehemu za vijijini na mijini.

Katika Mkoa wa Mwanza sehemu ambazo mafuta hayo yanapatikana ni Misungwi, Usagara, Busisi Feli, Mkomba, Nyampande, Sengerema, Sima, Igaka, Kasamwa, Geita, Karato, Nyahunge, Bupandwa, Mkome, Nzera, Nyarugusu, Bukori na Kakola wakati katika Mkoa wa Kigoma ni Kakonko, Kibondo na Kasulu.

Mkoani Shinyanga mafuta hayo yanapatikana Kishapu, Maganzo, Isaka, Tinde, Nata, Chuma, Chankora, Kahama, Segese, Bukombe, Runzewe, Ushirombo, Bariadi na Maswa wakati mkoani Bukoba yanapatikana Ngara, Biharamulo, na Katoro.

Katika Mkoa wa Mara mafuta hayo yanapatikana katika maeneo ya Makutano, Sirari na Utegi.

Inaelezwa kuwa baadhi ya maofisa wa TRA, Polisi na EWURA wanazo taarifa hizo, lakini katika kipindi cha miaka zaidi ya mitani hawajafutatilia suala hilo.

Inadaiwa kuwa mgodi mmoja uliopo mkoani Mwanza unatoa zaidi ya lita 100,000 kwa siku ambayo yanasambazwa katika maeneo tofauti nchini kwa kupitishiwa Katoma na kuuzwa kwa tofauti ya sh 500 ya mafuta ya yanayouzwa vituoni.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa wauzaji ambao wanaishi katika Kijiji cha Nyahunge wanaifadhi mafuta hayo ndani zaidi ya lita 100,000 bila kujua kama ni hatari kwa maisha yao.
 
Back
Top Bottom