Serikali yapokea msaada wa shilingi bilioni 14.9 ili kupambana na Corona

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Serikali imepokea msaada wa shilingi bilioni 14.9 kutoka Global Fund, Airtel Tanzania, Rotary Club Tanzania ambazo sehemu kubwa zitatumika kununua vifaa kinga kwa watumishi wa afya na vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye maambukizi ya COVID-19.

1587992669920.png

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo wakati akipokea msaada wa fedha na lita 1,250 za vitakasa mikono ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Waziri Ummy amefafanua kwamba Global Fund imetoa shilingi bilioni 14, Airtel Tanzania shilingi milioni 700 na Rotary Club Tanzania shilingi milioni 250.

“Tumepokea shilingi bilioni 14 kutoka Global Fund, shilingi bilioni 9.6 tumezitoa kwa ajili ya kununua vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa Afya, lakini pia fedha zilizotolewa na Airtel na Rotary Club Tanzania tutazielekeza huko. Kipaumbele chetu ni kuwalinda watumishi wa afya,” amesema Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

“Natumia fursa hii kuwashukuru watumishi wa afya ambao wamekuwa wakijitoa usiku na mchana katika kutoa huduma kwa watu waliopata maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19) pamoja na wale wahisiwa.

"Kipaumbele cha Serikali ni kuwalinda watumishi wa Afya kwa kununua vifaa kinga kwani fedha tulizozipata hapa tutazielekeza kwenye ununuzi wa vifaa kinga. Niendelee kuwaisistiza Watumishi wa Afya wazingatie miongozo ya magonjwa ya kuambukiza,” Amesema Waziri Ummy .

Amesema watumishi wa afya ambao wamepatiwa mafunzo katika vituo vya kutoa huduma kwa wenyr maambukizi ya ugonjwa huo, hakuna aliyepata maambukizi kwa kuwa wanazingatia miongozo ya Serikali ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Covid-19 pamoja na miongozo ya magonjwa ya kuambukiza.

Waziri amesema ushiriki wa kila mdau katika mapambano dhidi ya maambikizi ya virusi vya Corona ni muhimu na kwamba msaada uliotolewa na kampuni hizo ni mkubwa katika mapambano ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

1587992706968.png

“Napenda kurudia tena kwa niaba Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, nawashukuru Airtel Tanzania, Serengenti Breweries na Rotary Club kwa hiki mlichotupatia. Asanteni sana,” amesema Waziri Ummy.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Airtel Tanzania, Bw. Gabriel Malata amesema Airtel Tanzania imetoa shilingi milioni 700 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na janga la Corona.

“Sisi bodi ya wakurugenzi wa Airtel na kwa niaba ya Airtel Tanzania, tunatambua juhudi za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Corona, lakini pia tumejitathimini na kutambua kuwa sisi kama

Airtel hatuwezi kuendelea bila kuwepo watu wanaotumia huduma zetu. Watu hawa ndio mtaji wa Kampuni,” amesema Bw. Gabriel.

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengenti, Bw. John Wanyancha amesema kuwa kampuni hiyo imetoa lita 1,250 ya vitakasa mikono nyenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na maambukiza ya virusi.

Mwenyekiti wa Rotary Club, Bi. Agnes Batenga amesema Rotary imetoa shilingi milioni 250 kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID-19).

1587992735340.png

“Shilingi milioni 183 zitatumika kutoa msaada wa vifaa vya kujikinga (PPE), vifaa vya maji safi ambavyo vitasambazwa katika vituo maalumu vya kuhudumia wagonjwa wa Corona jijini Dar es Salaam, Hospitali ya Amana, Zanzibar, Hospitali ya Mawenzi na Hospitali ya Mount Meru,” amesema Bi. Agnes.

Amesema shilingi milioni 67 zitatumika katika kutekeleza miradi ya kudhibiti ugonjwa wa Corona nchini kupitia Club za Rotary.
 
Mh.....
Mungu awabariki waliotoa kwa Moyo, ila serikali nayenyewe isipende kupokea tu na yenyewe ijue kutoa.

Mfano, Serikali inaweza kabisa kupunguza makali ya maisha kwa wananchi wake kipindi hiki ambacho shuhuli nyingi za uzalishaji zimesimama ikiwa ni pamoja na ajira kusitihwa, serikali ikiamua inaweza kupunguza gharama za umeme, Maji, kodi mbalimbali nk.
 
Kabudi lazima apige simu Canada kabombadia kengine kaleeee kanaenda kupokelewa.
 
Jiwe alivyo Na roho mbaya anatamani hata aongeze kodi na bei ili mtaabike. Ndio maana kwengine ameacha mfe ila chato ameifunga yote.

Mh.....
Mungu awabariki waliotoa kwa Moyo, ila serikali nayenyewe isipende kupokea tu na yenyewe ijue kutoa.

Mfano, Serikali inaweza kabisa kupunguza makali ya maisha kwa wananchi wake kipindi hiki ambacho shuhuli nyingi za uzalishaji zimesimama ikiwa ni pamoja na ajira kusitihwa, serikali ikiamua inaweza kupunguza gharama za umeme, Maji, kodi mbalimbali nk.
 
Kadema wanajisikia vibaya kwa habari hii utadhani wanaishi Mars! Kwao habari nzuri ni ile ya Benki ya dunia yainima Tanzania mkopo wa kupambana na corona! AIBU YENU!
Una kinyongo hadi unakosea kuandika. Hebu soma tena uliyoyaandika mkuu alafu upunguze chuki kwa waTanzania wenzako

Mungu atakubariki.
 
Back
Top Bottom