mamayoyo1
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 1,011
- 1,019
- Hafla ya makabidhiano ya Hundi kifani ya gawio la shilingi Bilioni moja imefanyika jijini Dodoma, kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ambaye alipokea kwa niaba ya Serikali, na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo Dkt. Edmund Mndolwa.
- Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Mpango aliipongeza Benki hiyo kwa kutoa gawio kwa Serikali, na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.
- “Utoaji huu wa gawio ni kiashiria tosha kwa Serikali kuwa Benki inazidi kukua na kuwapa moyo watanzania na wawekezaji kuwa TPB inatoa huduma bora katika jamii”, alisema Dkt. Mpango.