Serikali yapokea gawio Bilioni 21.8 kutoka NMB

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,116
2,000
Na. Farida Ramadhani na Saidina Msangi, WFM, Dodoma

Serikali imepokea gawio la kiasi cha shilingi bilioni 21.8 kutoka Benki ya NMB, ikiwa ni sehemu ya faida ya shilingi bilioni 206 baada ya kodi iliyopatikana katika benki hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.

Akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango, alisema Serikali inathamini mchango wa Benki ya NMB katika maendeleo ya nchi na kuupongeza uongozi wa benki hiyo kwa jitihada mbalimbali za kuchangia uchumi wa nchi.

“Nimefurahi kusikia kwamba fedha hizo zimeshaingizwa katika akaunti ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha na Mipango mhakikishe fedha hizo zinatumika katika miradi ya kipaumbele ili kutatua changamoto za wananchi,” alisema Mhe. Dkt. Mpango.

Aidha, Dkt. Mpango ameelekeza mabenki pamoja na taasisi nyingine za fedha nchini kutumia utaalamu na uzoefu walionao katika Sekta ya Fedha kutafuta suluhisho la riba kubwa ili wananchi waweze kupata mikopo na kuweka amana katika taasisi hizo.

Vilevile, Mhe. Dkt. Mpango amezielekeza taasisi nyingine ambazo Serikali ina hisa kuhakikisha zinajiendesha kwa ufanisi na kutoa gawio Serikalini ili kuiwezesha kutekeleza miradi ya maendeleo na kuonya kuwa Taasisi hizo kushindwa kutoa gawio ina maanisha viongozi wanaoongoza taasisi hizo hawatoshi katika nafasi hizo.

Aidha, Dkt. Mpango amempongeza Msajilli wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka kwa usimamizi wa mashirika ya umma, taasisi pamoja na kampuni 287 na kuwezesha Serikali kupata gawio kulingana na uwekezaji wa hisa na umiliki wa moja kwa moja wa Serikali.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dkt. Edwin Mhede alisema mwaka 2019 Benki yake iliipatia Serikali gawio la shilingi bilioni 15.2 lakini kutokana na maelekezo ya Mhe. Makamu wa Rais wakati huo akiwa Waziri wa Fedha na Mipango aliiagiza Benki hiyo kuongeza gawio kwa kuboresha huduma zake hatua iliyochangia kupata faida kubwa na kuiwezsha kutoa gawio hilo la shilingi bilioni 21.8 sawa na ongezeko la asilimia 43.

“Tunaahidi kuwa mwaka ujao tutaongeza ubunifu na uwajibikaji zaidi na kuongeza gawio kubwa zaidi Serikalini” Aliongeza Dkt. Mhede

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara ambayo yamechochea mafanikio ya benki hiyo na kuweza kufikisha mtaji wa Sh. trilioni 1.1.

Bi. Zaipuna alibainisha kuwa pamoja na kutoa gawio hilo, Benki yake pia imelipa kodi mbalimbali serikalini zenye thamani ya shilingi bilioni 245 na kiasi cha Sh. bilioni 1.4 kimetumika katika kuwezesha sekta za elimu, afya, elimu kupitia mpango wao wa kutoa huduma kwa jamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameupongeza uongozi wa benki ya NMB kwa kusimamia utendaji wa benki hiyo na kufanikisha kupatikana kwa faida kubwa na kuwaagiza kuendelea kudhibiti matumizi, kuongeza mapato na kusimamia vyema mikopo ili mwakani waweze kutoa gawio kubwa zaidi.

Mhe. Dkt. Nchemba aliiagiza Ofisi ya Msajili wa Hazina kuendelea na juhudi za kusimamia taasisi na mashirika ya umma kwa kuwa ufanisi wa mashirika hayo una faida kwa Serikali na wananchi kwa ujumla.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka amesema kuwa kutokana na usimamizi mzuri ofisi hiyo imeendelea kushuhudia maduhuli ya Serikali yakipanda kutoka shilingi bilioni 225.467 mwaka 2015/16 hadi shilingi bilioni 753.95 mwaka 2019/20, ikiwa ni ongezeko la asilimia 77 na fedha hizo ziliingizwa moja kwa moja katika akaunti ya Ofisi hiyo.
 

Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
40,956
2,000
Sijui haterz wa muheshimiwa hayati Jiwe watasemaje, nasubiri kusikia jinsi wanavyojamba jamba, halafu tuone kama huko miaka ya usoni haya magawio yataendelea kuwepo. RIP 🪦 JPM
Lini ulisikia NMB imepata hasara?
 

RMC

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
716
1,000
Nakumbuka Mranba alisimama kidete huko nyuma kutaka benki hii iuzwe kabisa lakini wazalendo walipiga mno kelele kupinga na hizo kelele zilisaidia sana. Kama ingeuzwa yote leo hii serikali isingekuwa inavuna gawio kila mwaka.

Ilifika hatua Mkurugenzi wake raia. wa Marekani wakati huo alilazimika kujiuzulu baada ya kukataa shinikizo lililokuwa linamtaka adanganye kuwa benki inapata hasara ili kuwarahisishia waliokuwa wanataka kuiuza . Uzalendo wake mmarekani yule uliisaidia benki isiingie mikononi mwa mafisadi.

Nakumbuka alisema kuwa Marekani kudanganya ni kosa la jinai linaloadhibiwa na sheria kisha akajiuzulu.
 

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,624
2,000
Nakumbuka Mranba alisimama kidete huko nyuma kutaka benki hii iuzwe kabisa lakini wazalendo walipiga mno kelele kupinga na hizo kelele zilisaidia sana. Kama ingeuzwa yote leo hii serikali isingekuwa inavuna gawio kila mwaka. Ilifika hatua Mkurugenzi wake raia. wa Marekani wakati huo alilazimika kujiuzulu baada ya kukataa shinikizo lililokuwa linamtaka adanganye kuwa benki inapata hasara ili kuwarahisishia waliokuwa wanataka kuiuza . Uzalendo wake mmarekani yule uliisaidia benki isiingie mikononi mwa mafisadi. Nakumbuka alisema kuwa Marekani kudanganya ni kosa la jinai linaloadhibiwa na sheria kisha akajiuzulu.
Akipatikana Mtanzania wa aina hii, Hawezi kuishi miaka yake aliyopangiwa
 

Gobole

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
1,044
2,000
Akipatikana Mtanzania wa aina hii, Hawezi kuishi miaka yake aliyopangiwa
Ila Basil Mramba yupo tu mtaani anakula good time...now ana miaka 81...keshavuka ht ile standard ya miaka 70...vp unalisemeaje hilo?
 

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,624
2,000
Ila Bazil mramba yupo tu mtaani anakula good time...now ana miaka 81...keshavuka ht ile standard ya miaka 70...vp unalisemeaje hilo?
Uko nje ya mada,

Inasadikiwa kwamba, huyo bwana mramba wakati akiwa waziri, alitaka bank ya NMB iuzwe kwa lengo la kifisadi, akidai eti inatia hasara,alyekuwa mkurugenzi wa bank hiyo wakati huo alikuwa mzungu Muamerica, Mramba alimfuata akimwambia akubali haraka kwamba bank hiyo inatia hasara Serikali,

Yule mzungu hakukubali ombi la waziri Mramba kwa kuwa haikuwa kweli kwamba bank ilikuwa haitoi faida, basi yule mzungu ikabidi ajihudhuru kulinda heshima yake na ya nchi yake, kwakuwa nchini kwao, kitu kinaitwa uwongo ni mwiko kwao

Ndipo nikasemaa...! Aikitokea mbongo wa aina ya mzungu huyo, hawezi kuishi kwa miaka yake alopangiwa!!

wewe tena hukuelewa unaleta habari za Mramba kuishi miaka mingi, sio mbaya lkn
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom