Serikali yapigilia msumari msimamo wake kuhusu mapenzi ya jinsia moja

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
1.JPG


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Amon Mpanju amesema kuwa mapenzi ya jinsia moja hayakubaliki na Serikali ilishaweka msimamo wake katika hilo.

Akizungumza mapema leo katika mkutano wa wadau wa haki za binadamu uliofanyika katika hoteli ya Blue Pearl wa kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu (Universal Periodic Review), Mhe. Mpanju ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo alisema mapendekezo yaliyowasilishwa Mwezi Mei mwaka huu katika mkutano wa Baraza la haki za binadamu uliofanyika Geneva, serikali ilikubali mapendekezo Mia thelathini (130) na mengine 72 iliyakataa.

“Sehemu ya mapendekezo hayo serikali iliyakataa kwa sababu kuna mengine yapo kinyume na katiba, sheria, mila na desturi zetu, kwani katika mapendekezo hayo yapo yanayotaka mapenzi ya jinsia moja jambo ambalo haliwezi kukubalika”, Mhe. Mpanju alisema

“Hivyo wakati mkijadili namna ya kupanga mikakati ya utekelezaji ili serikali ione umuhimu wa kukubali sehemu ya mapendekezo hayo naomba msijielekeze kwenye yale yaliyo kinyume na imani”, Mhe. Mpanju alisisitiza

Aidha, Mhe. Naibu Katibu huyo alisema serikali imefungua milango kwa kushirikiano na tume, wadau wa haki za binadamu wapeleke serikalini sababu zenye mantiki ili kuona ni mambo gani ambayo serikali inaweza kuyashugulikia na kuyatekeleza.

Akizungumza katika Mkutano huo, Bwana Onesmo Olengurumwa kutoka taasisi ya watetezi wa haki za binadamu (THRDC) alisema kuwa wadau wamekutana katika mkutano huo kujadili ni kwa namna gani wataishawishi serikali ili iweze kuyakubali mapendekezo yaliyobakia na kuyaweka katika utekelezaji.

Akifungua mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Iddi Mapuri alisema kuwa mkutano huo umelenga katika kuweka mikakati ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo hayo na alipongeza mchango mkubwa unaotolewa na wadau wa haki za binadamu katika kuhakikisha masuala ya haki za binadamu yanapata msukumo mkubwa hapa nchini.

2.jpg


Bwana Onesmo Olengurumwa (aliyevaa koti la Drafti) kutoka taasisi ya watetezi wa haki za binadamu (THRDC) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za sheria wa Tume ya Haki za Binadamu, Bwana Nabor Assey( aliyevaa shati la bluu). Nyuma yao ni Bwana Laurent Burilo burilo, Mratibu wa Mpango kazi wa Haki za Binadamu(katikati) na Bwana Deugratius Bwire kutoka (THRDC)

3.jpg


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Amon Mpanju (aliyevaa miwani) akiteta jambo na Bwana Onesmo Olengurumwa (aliyevaa koti la Drafti) kutoka taasisi ya watetezi wa haki za binadamu (THRDC) katika mkutano huo wa kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu na kuweka mikakati ya kuishawishi serikali kukubali mapendekezo mengine ambayo iliyakataa.

4.jpg


Sehemu ya wadau wa haki za binadamu wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo wa kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu.

Chanzo: Mpekuzi


My Take: Haya matamko yanakuja siku chache tuu baada ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon kutangaza kujiuzulu ambaye anaunga mkono sana suala hili la mapenzi ya jinsia moja. Pia Obama naye anakaribia ukomo wa uongozi wake, ikiwa hii ilikuwa sera aliyoiunga mkono sana na kushawishi mataifa mengi ya Afrika kuikubali. Waafrika tuwe makini tusijekuuza utu wetu wetu!
 
NAIBU%20Katibu%20Mkuu%20wa%20Wizara%20ya%20Katiba%20na%20Sheria%2C%20Amon%20Mpanju.jpg


NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju, ametoa msimamo wa serikali na kusema mapenzi ya jinsia moja hayakubaliki Tanzania na serikali ilishaweka msimamo wake katika hilo.

Mpanju Mpanju alisema hayo jana katika mkutano wa wadau wa haki za binadamu uliofanyika jijini Dar es Salaam, kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu, na kuweka mikakati ya kuishawishi serikali kukubali mapendekezo mengine ambayo iliyakataa.

Mpanju ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, alisema mapendekezo yaliyowasilishwa Mei, mwaka huu, katika mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu uliofanyika Geneva, serikali ilikubali mapendekezo 130 na mengine 72 iliyakataa.

"Sehemu ya mapendekezo hayo serikali iliyakataa kwa sababu kuna mengine yako kinyume cha katiba, sheria, mila na desturi zetu, kwani katika mapendekezo hayo yapo yanayotaka mapenzi ya jinsia moja, jambo ambalo haliwezi kukubalika," alisema.

Aliongeza kuwa:

"Wakati mkijadili namna ya kupanga mikakati ya utekelezaji ili serikali ione umuhimu wa kukubali sehemu ya mapendekezo hayo, katika mkutano huu, naomba msijielekeze kwenye yale yaliyo kinyume cha Imani."

Alisema serikali imefungua milango kwa kushirikiana na tume, hivyo wadau wa haki za binadamu wapeleke serikalini sababu zenye mantiki ili kuona ni mambo gani ambayo serikali inaweza kuyashugulikia na kuyatekeleza.

Naye Onesmo Olengurumwa kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), alisema wadau wamekutana katika mkutano huo kujadili ni kwa namna gani wataishawishi serikali ili kuyakubali mapendekezo yaliyobakia na kuyaweka katika utekelezaji.

Awali, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Iddi Mapuri, alisema mkutano huo umelenga katika kuweka mikakati ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo hayo.

Mapuri alipongeza mchango mkubwa unaotolewa na wadau wa haki za binadamu katika kuhakikisha masuala ya haki za binadamu yanapata msukumo mkubwa nchini.

Source: Nipashe
 
Back
Top Bottom