Serikali yapiga marufuku wanunuzi kukopa pamba za wakulima

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Mnunuzi yeyote anapochukua Pamba katika Chama cha Msingi, ni lazima Mkulima awe amelipwa ndani ya muda usiozidi saa 48, na watakaoenda kinyume watafutiwa Leseni.

Kauli yake imekuja baada ya Mbunge Robert Maboto kuhoji ni kwa namna gani Wizara imejipanga kuwasimamia wenye Viwanda wasiende kukopa kwa zao hilo kwa Wakulima.
 
Masaa 48 ya nini?

Tunataka hela baada ya kuuza pamba, dk 20 tu.

Mnalazimisha amcos sijui ushirika au ushirikina.

Magufuli aliharibu sana mfumo wa biashara, alitaka ujamaa ambao ulishakufa na nyerere.

Ruhusu makampuni ya kibepari yanunue pamba wakulima wapate pesa.

Binafsi nilishaapa kutolima pamba hadi serikali ya ccm iondoe hao wachawi waitwao amcos
 
Dakika 20 za nini?
Kwanza alipe ndio achukue pamba?
 
Back
Top Bottom