Serikali yapiga marufuku ulaji wa nyama ya Nguruwe Kahama kwa muda usiojulikana

Biashara ya nguruwe yapigwa marufuku Tanzania Homa ya nguruwe yabainika Tanzania
Mkuu wa Wilaya ya kahama Annamringi Macha amepiga marufuku biashara ya nyama ya nguruwe na usafirishaji wa nguruwe wenyewe baada ya wanyama hao kubainika kwa homa ya nguruwe, Gazeti la serikali ya Tanzania, Habari leo limeandika.

Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu huyo wa wilaya alisema amechukua uamuzi huo ili kukinga wananchi na watumiaji wa nyama hiyo dhidi ya ugonjwa huo.

‘’Maeneo yanayofanya biashara ya nyama ya nguruwe, vichinjio, wapishi na sehemu za starehe haziruhusiwi kufanya biashara hiyo kwa sasa mpaka itakapotangazwa tena,’’ Macha alisema.

Bwana Macha alisema dalili za mlipuko wa ugonjwa huo zilianza Desemba mwaka jana na sasa ni kama unasambaa.

Bwana Macha pia alipiga marufuku usafirishaji wa wanyama hao kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kibali cha daktari na atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Daktari wa Mifugo Halmashauri ya Mji wa Kahama, Dkt. Damian Kilyenyi amethibitisha kuwa zaidi ya nguruwe 500 wamekufa kwasababu ya ugonjwa huo.

Homa ya nguruwe ni nini?

Ni ugonjwa wa kupumua unaosababishwa na virusi ya influenza aina A, vinavyofahamika kama H1N1
Chanzo chake ni kwenye nguruwe, lakini sasa huambukiza binadamu na huenezwa kwa kupiga chafya au kukohoa.

Dalili za ugonjwa huo zinakaribiana na za homa ya msimu - homa kali, kukohoa, maumivu kooni, maumivu mwilini na mzizimo. Wanaoathirika zaidi huwa wajawazito, watoto wa chini ya miaka mitano, wazee wa zaidi ya miaka 65 na wale wenye matatizo mengine ya kiafya.

Virusi hiyo vilitambuliwa mara ya kwanza nchini mexico mwaka 2009 na vikaenea upesi maeneo mengine duniani.
 
Pork mpenda watu lakini watu hawampendi pork.
Siyo kweli watu hawampendi pork, lakini inategemea na mapenzi yako kwake. Katazo la kutokula nguruwe siyo sababu ya kumchukia mnyama huyo, kwani ameumbwa na Muumbaji huyo huyo aliyekuumba wewe, lakini kutokana na utaratibu na hekima aliyokuwa nayo Muumba akatukataza kutomtumia nguruwe kwa kitu chochote, hivyo kumfanya kuwa "special animal" ambaye atakuwa huru bila ya kuudhiwa kwa kuliwa na kutumiwa kwa jambo lolote kama wanyama wengine mbuzi, ng'ombe, kondoo n.k.

Kutochinjwa au kuuliwa kwa nguruwe hakujamfanya kuwa mwenye kuchukiwa, bali ndiyo mapenzi ya kumpenda mnyama huyo. Chukulia mume na kaka, hawa wote ni wanaume lakini mume ndiye unaweza kufanya naye tendo la ndoa lakini kwa kaka ni haramu kufanya naye tendo la ndoa lakini wote utakuwa unawapenda kwa mipaka yao.
 
Siyo kweli watu hawampendi pork, lakini inategemea na mapenzi yako kwake. Katazo la kutokula nguruwe siyo sababu ya kumchukia mnyama huyo, kwani ameumbwa na Muumbaji huyo huyo aliyekuumba wewe, lakini kutokana na utaratibu na hekima aliyokuwa nayo Muumba akatukataza kutomtumia nguruwe kwa kitu chochote,
Shukran kwa maelezo mazuri.
 
Nimepitia uzi mzima najukuta najawa mate mdomoni hichi kiumbe bana,anyway ngoja nikachukue kilo na ndizi tatu kachumbari nyiiingii, nianze nank vant mdogo mdogo nikiendelea kuisubiri
 
Huyo alietangaza anajua hasara za kiuchumi ambazo nchi itapata kutokana na kukulupuka Ivo ? Achukuliwe Sheria . Na kazi afukuzwe kwa maana yeye Hana hayo mamlaka.
 
Kama ni ugonjwa kuwepo basi ni jukumu la wizara na sio wilaya. Pia Hali hii Kama itaachwa basi kiuchumi itatugalimu pakubwa Sana. Maadui zetu wataweza tumia mwanya huo kusema nchi yote ina mafua ya nguruwe.

Na sio tu kwa nguruwe waweza sema hata ngombe, mbuzi, na kuku wanamafua. Nimwona BBC wanasema Tanzania Kuna mafua ya nguruwe. Wahusika wawajibishwe mara moja maana Ni sawa na kuhujumu uchumi.

Hiyo sio kazi yao Bali ni kazi ya wizala.
 
Wewe ndio utakuwa na huo ugonjwa na wala sio hao nguruwe...
Au ndio uroho umekushika mpaka kwenye mikono kiasi cha kushindwa kuandika?.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom