Serikali yapiga marufuku tuzo za muziki na mashindano ya Miss Tanzania

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287


Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amesema amepiga marufuku mashindano ya miss Tanzania na Tuzo za muziki

Amesema mashindano ya Miss Tanzania yamegubikwa na ubabaishaji kwenye utoaji wa tuzo na wamekuwa wakiwasotesha watoto wetu kwa mwaka mzima wakijiandaa na tuzo hizo lakini mwisho kuwapa zawadi inakuwa ni usumbufu

Ameongezea kwa watakaotaka kuandaa mashindano hayo zawadi wanazoahidi kuwapa washindi ziwekwe ofisini kwake

Kwa sasa wanakaa chini na wadau wa burudani juu ya mashindano hayo ila wanataka ziwe na (guaranteed sustainability) muendelezo wa uhakika na sio kufanyika kwa kubahatisha

Kwenye tuzo za muziki waziri amesema tuzo za muziki zilikuwa zikitegemea watu wakinuna basi hakuna tuzo hizo na pia zinahitaji marekebisho

Chanzo: Times FM
 
Back
Top Bottom