Serikali yapiga marufuku Posho kwenye Halmashauri!

Waanzie Bungeni kwanza then wizara zoote baadae washuke chini halmashauri zote!na tamko litoke kwa JK au Pinda ku cover kila sekta
 
Huyu Naoni katibu mkuu ni mpumbavu kama wapumbavu wengine wa CCM. Anajua kabisa serikali haifanyi kazi kwa kufuata matamko ya wanasiasa majukwaani bali inafanya kazi kwa kufuata secular.

Kama anataka kuondoa hizo posho lazima itoke secular inayozuia kutoa posho za aina hiyo na secular hizo hupitishwa na baraza la mawaziri. Lakini kama ipo SECULAR inayoruhusu wakurugenzi kutoa pOSHO za aina hiyo basi atakuwa anat twanga majini kwenye kinu.
 
hivi mshahara wake huyo ni shilingi ngapi???


mnyonge mnyongeni lakini haki
yake mpeni,nadhani tumsifu na kumuunga mkono huyu naibu katibu mkuu kwa
msimamo wake na hatua anazochukua na kabla hajaenda mikoani labda
ameshasafisha wizarani kwake,ma ps wengine waige mfano huu
 
Yes huu ni upuuzi na ndio maana watu hawafanyi kazi wakisubiri posho ni ugonjwa hatari kuliko ukimwi nchini. Sote tupige vita tabia hii ya kutaka posho katika kila unachofanya hata kama ni sehemu ya kazi yako ya kila siku.
 
Unajua saa hizi mafisadi wanatafuta viinimacho kuwadanganya watizedi uchaguzi 2015.Natoa wito:TUWE MAKINI TUSIDANGANYWE!
 
PM alpga marufuku semina,wakangeuza jina ssa wanaita mafunzo,na hiyo posho wataipatia jina lngne muda c mrefu,na maisha yataendelea kama kawa!
 
huyu katibu aliyetamka haya ni juakalulu
na muandishi aliyeandika haya ni juakalulu

hebu watutajie ni watumishi gani wanalipwa posho wakiwa vituo vya kazi.

WEWE NDIO JUAKALULU!

Anaposema kwenye kituo cha kazi ana maana ya kuwa ndani ya Wilaya husika, mfano mtumishi anayefanyia kazi makao makuu ya wilaya anapoenda Vijijini kufanya kazi fulani. Hakuna watumishi wanaolipwa posho kwa kwenda vijijini kutimiza majukumu yao?

Juakalulu mkubwa wee!
 
jamani mm nazijua halmashauri mno! kule cha mtoto sana mambo yote wizarani! Wizarani ndio source ya yote! narudia tena hii ni sawa na maneno maarufu ya polisi ya kitu cha ncha kali ili kufunika kombe! halmashauri ndio dampo la lawala asilimia kubwa imekuwa kichaka cha maovu cha serikali kuu!
 
Kadata kutembelea halmashauri ni moja ya majukumu kwa mujibu wa kazi zake, lakini hebu tumuulize amejilipa posho kiasi gani ya kwenda kutembelea hizi halmashauri? Akisema hajajilipa basi akataze watumishi wengine kulipwa posho. Akisema ndiyo, ajitafakari kwanza kabla ya kuzungumza.
 
Cheki mambo mawili kwa haraka:-
1) Mahudhurio ya wajumbe yakoje
2) Idadi ya vikao (no. and frequency) kulinganisha na siku za nyuma

Lakini pamoja na changa hili la macho yote tisa ila fedha hizo hizo zitafisadiwa kwa njia nyingine lukuki! CCM hawana uwezo, nia wala utashi wa kupambana na ubadhirifu serikalini. Kama ilivyo rushwa na ufisadi ubadhirifu nao uko kwenye vinasaba vyao, ndio uhai wa CCM!
 
Matamshi! Matamshi!. Government business moves on paper. Si atoe waraka wa kufuta nyaraka zilizopo? Si kweli kwamba kila posho anayolipwa mtumishi awapo kituoni kwake ni wizi. Halafu kwa nini asubiri kuyasema haya kwenye majukwaa, wakati ofisi anayo.? Au hii ndiyo njia ya yeye kusikika! Poor him, cheap popularity.
OR-Utumishi ndiyo hutoa nyaraka za posho watumishi wawapo katika vituo vyao vya kazi. Yeye kapata wapi madaraka haya? Au ndio kama kambale kila moja na ndevu zake.
 
WEWE NDIO JUAKALULU!

Anaposema kwenye kituo cha kazi ana maana ya kuwa ndani ya Wilaya husika, mfano mtumishi anayefanyia kazi makao makuu ya wilaya anapoenda Vijijini kufanya kazi fulani. Hakuna watumishi wanaolipwa posho kwa kwenda vijijini kutimiza majukumu yao?

Juakalulu mkubwa wee!

hiyo maana unaiweka wewe!kikawaida ukiajiriwa huwa unapewa barua ya ajira na pia barua hupelekwa kwa mkuu wa idara husika mfano afya,elimu au maji ili upangiwe kituo cha kazi.kituo cha kazi chaweza kuwa makao makuu ya wilaya au vijijini.nakushauri urudie kusoma kanuni za kudumu za utumishi wa umma ili ujiondoe kwenye group la majuha kalulu.
 
Back
Top Bottom