Serikali yapiga marufuku Posho kwenye Halmashauri!

Informer

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Messages
1,323
Likes
3,200
Points
280
Informer

Informer

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2006
1,323 3,200 280
Imeandikwa tarehe 30 Novemba 2012 na Christopher Maregesi, Bunda | HabariLeo

SAKATA la posho kwa watendaji wanaolipwa mshahara baada ya kupoa kwa wabunge, limehamia katika halmashauri nchini kote baada ya Serikali kupiga marufuku posho za watumishi wa halmashauri hizo zinazotolewa wakati wakitimiza majukumu yao ndani ya vituo vya kazi.

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mathayo Kadata alitoa kauli ya kuzuia posho hizo jana mjini hapa, akiwa katika ziara yake ambapo pia alikutana na wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Alifafanua, kuwa malipo ya posho yanapaswa kutolewa kwa mtumishi aliyetumwa kikazi nje ya kituo chake cha kazi na si vinginevyo na kumtaka kila mtumishi wa halmashauri nchini kuzingatia hilo ili kudumisha nidhamu katika matumizi ya fedha za Serikali.

Kadata alionya watumishi wa halmashauri nchini wenye tabia ya kuomba wakurugenzi wao posho kila mara hata wawapo ofisini mwao na kuongeza kuwa kudai posho ni sawa na kuiibia Serikali.

Mbali na kuonya watumishi hao, Kadata pia alionya wakurugenzi wa halmashauri kwamba hatasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na ikibidi kuwaondoa kazini mara moja, wakibainika kulipa posho watumishi wao kwa mambo yaliyo ndani ya majukumu yao ya kila siku.

Alisema watendaji hao wanapaswa kutambua, kuwa wameajiriwa kwa lengo la kutumikia Watanzania wanaowalipa mishahara kupitia kodi wanazotoa.

Alitaka watumishi watumikie wananchi maana wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi kutokana na walichokifanya kwa mwezi na kusisitiza, kwamba kudai posho ni wizi.

“Wananchi hawa wanaelewa sana. Hatuwezi kuwafanya wajinga siku zote. Tunawazidi utaalamu tu lakini si kingine; hivyo tunapaswa tuwatumikie kwa ubunifu na uadilifu wenye uzalendo mwingi ndani yake,” alisema Kadata.

Aliongeza kuwa Watanzania wanatarajia kuona mabadiliko ya maisha yao yatokanayo na ubunifu, uadilifu, uwajibikaji na uzalendo wa watumishi wao.

Sakata la posho limekuwa likiibuka mara kwa mara katika ngazi ya wanasiasa na hasa wabunge ambapo wananchi na wadau wamekuwa wakihoji mantiki ya posho kwa mtu anayelipwa mshahara.
 
Jackbauer

Jackbauer

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
5,920
Likes
98
Points
145
Jackbauer

Jackbauer

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
5,920 98 145
huyu katibu aliyetamka haya ni juakalulu
na muandishi aliyeandika haya ni juakalulu

hebu watutajie ni watumishi gani wanalipwa posho wakiwa vituo vya kazi.
 
M

MR.LEO

Senior Member
Joined
Jun 10, 2012
Messages
129
Likes
3
Points
0
M

MR.LEO

Senior Member
Joined Jun 10, 2012
129 3 0
Iweje aseme watumishi wa halmashauri tu wakati huo ujinga upo mpaka ngazi ya wizara,,,?
AANZE KUPIGA MARUFUKU OFISINI KWAKE KWANZA!
 
Mr. Bigman

Mr. Bigman

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2011
Messages
2,492
Likes
1,050
Points
280
Mr. Bigman

Mr. Bigman

JF-Expert Member
Joined May 7, 2011
2,492 1,050 280
Baada ya ninyi wenyewe kushiba na kukinai posho, leo mnawageuzia wenzenu wasilipane posho. Nani atakubali? Labda na ninyi mrudishe posho zote mlizo zimega kwa angalau miaka 10 iliyopita! I mean kila mwaka ten years!
 
M

Mgaya D.W

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
966
Likes
201
Points
60
M

Mgaya D.W

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
966 201 60
Atoe waraka wa namna posho zinavyotakiwa kutolewa na aseme atakabiliana vipi na wanaopeana poshi pasi kufuata taratibu,vinginevyo maneno matupu hayavunji mfupa na kama kauli tuna mafurushi ya kauli zisizo na meno zilizo tolewa na mawaziri,waziri mikuu na hata rais na hatujaona zikifanyiwa kazi.

Hatuhitaji kujenga nchi kwa maneno tu bali vitendo so Busara kwa ndg.Kadata ni kuja na wakurugenzi pamoja na watumishi wao aliowakamata wakipeana poshi bila kuzingatia sheria na kutueleza hatua mathubuti zilizochukuliwa dhidi yao na si haya matamko maana kwa sasa hatuna kwa kuhifadhi kila tamko.
 
SG8

SG8

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2009
Messages
3,501
Likes
558
Points
280
SG8

SG8

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2009
3,501 558 280
Huyu alitaka tu coverage ya vyombo vya habari. Posho zipi anazozizuia? Posho zipo Wizarani kwake Tamisemi aanze na hizo kwanza. Vinginevyo asituletee unafiki wake hapa
 
UJANJAUJANJA

UJANJAUJANJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2012
Messages
217
Likes
16
Points
35
UJANJAUJANJA

UJANJAUJANJA

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2012
217 16 35
Imeandikwa tarehe 30 Novemba 2012 na Christopher Maregesi, Bunda | HabariLeo

SAKATA la posho kwa watendaji wanaolipwa mshahara baada ya kupoa kwa wabunge, limehamia katika halmashauri nchini kote baada ya Serikali kupiga marufuku posho za watumishi wa halmashauri hizo zinazotolewa wakati wakitimiza majukumu yao ndani ya vituo vya kazi.

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mathayo Kadata alitoa kauli ya kuzuia posho hizo jana mjini hapa, akiwa katika ziara yake ambapo pia alikutana na wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Alifafanua, kuwa malipo ya posho yanapaswa kutolewa kwa mtumishi aliyetumwa kikazi nje ya kituo chake cha kazi na si vinginevyo na kumtaka kila mtumishi wa halmashauri nchini kuzingatia hilo ili kudumisha nidhamu katika matumizi ya fedha za Serikali.

Kadata alionya watumishi wa halmashauri nchini wenye tabia ya kuomba wakurugenzi wao posho kila mara hata wawapo ofisini mwao na kuongeza kuwa kudai posho ni sawa na kuiibia Serikali.

Mbali na kuonya watumishi hao, Kadata pia alionya wakurugenzi wa halmashauri kwamba hatasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na ikibidi kuwaondoa kazini mara moja, wakibainika kulipa posho watumishi wao kwa mambo yaliyo ndani ya majukumu yao ya kila siku.

Alisema watendaji hao wanapaswa kutambua, kuwa wameajiriwa kwa lengo la kutumikia Watanzania wanaowalipa mishahara kupitia kodi wanazotoa.

Alitaka watumishi watumikie wananchi maana wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi kutokana na walichokifanya kwa mwezi na kusisitiza, kwamba kudai posho ni wizi.

“Wananchi hawa wanaelewa sana. Hatuwezi kuwafanya wajinga siku zote. Tunawazidi utaalamu tu lakini si kingine; hivyo tunapaswa tuwatumikie kwa ubunifu na uadilifu wenye uzalendo mwingi ndani yake,” alisema Kadata.

Aliongeza kuwa Watanzania wanatarajia kuona mabadiliko ya maisha yao yatokanayo na ubunifu, uadilifu, uwajibikaji na uzalendo wa watumishi wao.

Sakata la posho limekuwa likiibuka mara kwa mara katika ngazi ya wanasiasa na hasa wabunge ambapo wananchi na wadau wamekuwa wakihoji mantiki ya posho kwa mtu anayelipwa mshahara.
Wana JF,

Naona kama yote yanayoendelea kutokea ndani ya serikali yetu "is a copy and paste of Chadema's 2010 election manifesto". Still more to bee heard and seen
 
E

emike

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2011
Messages
346
Likes
6
Points
35
Age
48
E

emike

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2011
346 6 35
mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,nadhani tumsifu na kumuunga mkono huyu naibu katibu mkuu kwa msimamo wake na hatua anazochukua na kabla hajaenda mikoani labda ameshasafisha wizarani kwake,ma ps wengine waige mfano huu
 
Bob Lee Swagger

Bob Lee Swagger

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Messages
1,366
Likes
6
Points
135
Bob Lee Swagger

Bob Lee Swagger

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2011
1,366 6 135
Wangefanikiwa kuzikataza posho kwenye ngazi za juu kwanza, bungeni, wizarani nk ingeweza kuwa rahisi zaidi kwenye halmashauri. Kinyume na hapo wategemee upinzani mkubwa sana maana kusema ambacho hawatendi ni unafiki tu!
 
kibogo

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Messages
9,696
Likes
1,196
Points
280
Age
28
kibogo

kibogo

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2012
9,696 1,196 280
Huu ni umbumbu wa Fikra tuesikia wamewaongezea mishahara wakubwa tofauti ni watumishi wa ngazi za chini ambao ni wengi na kwa njia moja ama nyingine hizo posho zilikuwa kama motivation kiutendaji, kwa kauli hii wasitegemee kama TZ utendaji utaimarika wakubwa wamewaongezea posho zao kwenye mishahara yao wanyonge wanasema wasipewe posho na kama tunavyojua wakuu wa Idara wa serikali karibu wote wanalinda maslahi ya CCM wakiwemo wakurugenzi na ndo maana tunaona upendeleo wa wazi unavyofanyika kwao.
 
kibogo

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Messages
9,696
Likes
1,196
Points
280
Age
28
kibogo

kibogo

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2012
9,696 1,196 280
Baada ya ninyi wenyewe kushiba na kukinai posho, leo mnawageuzia wenzenu wasilipane posho. Nani atakubali? Labda na ninyi mrudishe posho zote mlizo zimega kwa angalau miaka 10 iliyopita! I mean kila mwaka ten years!
Hawa jamaa naona wamepewa muongozo ili kukusanya fedha za uchaguzi 2015 kama si hivyo itakuwa wafadhiri wamegoma kutoa fedha na serikali haina fedha ndo maana tunasikia matamko kama haya.
 
Mtumishi Wetu

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
5,145
Likes
523
Points
280
Age
66
Mtumishi Wetu

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
5,145 523 280
mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,nadhani tumsifu na kumuunga mkono huyu naibu katibu mkuu kwa msimamo wake na hatua anazochukua na kabla hajaenda mikoani labda ameshasafisha wizarani kwake,ma ps wengine waige mfano huu
Hana lolote huyo waziri angefaa aanzie kwenye wizara yake na yeye mwenyewe asichukue posho aonyeshe mfano!!! Mwakyembe alisafiri na treini toka Dar hadi Dodoma atoe mfano halisi!!! Hitawezekana wizara zingine wapeane posho na ofisi za wakuu wa mikoa eti halimashauri hakuna utakuwa uonezi!!! Atoe secular kiserikali sio kwenye majukwaa kuwa Tanzania posho basi!!!

Kimagege

Kimagege

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
283
Likes
1
Points
35
Kimagege

Kimagege

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
283 1 35
huo ni unafki wa hali y juu kwani hata huyo aliyetoa hilo tamko naamini opia alipewa posho ya kutoa tamko kana kwamba hio sio kazi yake.serikali ingeanza na posho za wabunge na mawaziri kabla ya kugusa hizi nyingine.haopo ingeeleweka kuliko kuwadanganya watu kama wanavyofanya.
 
Malafyale

Malafyale

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Messages
12,323
Likes
5,086
Points
280
Malafyale

Malafyale

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2008
12,323 5,086 280
Rais,VP,PM,Mawaziri,wabunge,Vigogo wa wizara na WAKUU wa vyombo vya dola,Ma RC na Ma DC,na wakurugenzi wa taasisi za UMMA NDIYO wawe wa kwanza kunyang'wanywa POSHO kwa maana wao ndiyo wanaotumia pesa nyingi mno!

Kuwanyang'anya posho hawa watumishi walala hoi ni kuwaonea tu!
 
Mtanzania1

Mtanzania1

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2010
Messages
1,169
Likes
0
Points
133
Mtanzania1

Mtanzania1

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2010
1,169 0 133
......Pyramid life
 
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
13,476
Likes
2,416
Points
280
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined Oct 4, 2007
13,476 2,416 280
Posho zitatugawa watanzania
 
Forum statistics

Threads 1,251,863
Members 481,917
Posts 29,788,064