Serikali yapiga marufuku matumizi ya dawa za aina tatu kwa wenye kiungulia na vidonda vya tumbo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
40cc60ce53eeaf36d9b0e8f9c4e20b5c

Afisa Habari Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), Gaudencia Semwanza

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) imewataka watu wote waliokuwa wanatumia dawa za Raniplex 150 mg, Rantac 500mg/mL na Aciloc 150mg, ambazo hutumika kwa kiungulia na vidonda vya tumbo kuacha mara moja na kuripoti kituo chochote cha Afya kilicho karibu.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili kuhusiana na katazo hilo ambalo taarifa zake zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Afisa habari wa Mamaka hiyo, Gaudencia Semwanza, alikiri kuwa taarifa hizo ni za kweli na kwamba wamefanya hivyo kwa ajili ya usalama

“Ni kweli taarifa hizo zinazosambaa ni za kweli na tumefanya hivyo kwa ajili ya usalama tu, lakini pia taarifa kamili ipo kwenye tovuti yetu,” alisema Semwanza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyoko kwenye tovuti ya mamlaka hiyo, TMDA imefanya tathmini kamili ya dawa zote za binadamu zilizo na ‘ranitidine’ kama kingo hai ya dawa (API).

Ranitidine ni dawa inayotumiwa kwa dalili nyingi ikiwamo ya matibabu na kuzuia vidonda vya tumbo na matumbo, kudhibiti uzalishaji wa asidi ya tumbo kwenye utando wa moyo na vile vile matibabu ya ugonjwa wa gluro-esophageal Reflux (GERD).

“Mapitio ya bidhaa zilizo na ranitidine ililenga kutambua yale ambayo yana N-nitrosodimethylamine (NDMA) – uchafu ambao umethibitishwa hivi karibuni kuwa ugonjwa wa kansa unaoweza kusababisha mfano na saratani kwa binadamu.

“Hivyo kufuatia ukaguzi, bidhaa za dawa zilizoorodheshwa hapo chini zimezingatiwa ili kuangalia hali ya uzalishaji, lakini tulibaini kuwa zinazalisha uchafu,” ilieleza taarifa hiyo na kuziorodhesha dawa hizo kuwa ni.

Raniplex 150 mg inayozalishwa Cyprus, Rantac 500 mg/mL na Aciloc 150 mg zinazozalishwa nchini India.

TMDA ilisema kuwa kutokana na uchunguzi wake, imeamua kuzuia dawa hizo ili kulinda afya ya watumiaji.

“Kuhusiana na hili na kulinda afya ya umma, TMDA imesimamisha utumiaji wa bidhaa hizi za dawa kuanzia Novemba 15, 2019, pia watengenezaji wote wameelimishwa na kuamriwa kubadili muundo wao ikiwa ni pamoja na michakato ya utengenezaji ili kutengeneza bidhaa ambazo hazizalishi uchafu.

“Kama kuna bidhaa mbadala za dalili kama hizo kama Omeprazole, lansoprazole, Rabeprazole, Pantoprazole na Esomeprazole ambazo zimeidhinishwa kutumiwa na TMDA, wagonjwa wanashauriwa kushauriana na watoa huduma zao za afya kupata maagizo mapya kulingana na hali yao ya ugonjwa,” imeeleza taarifa hiyo.

Pia imesema kuwa, wauzaji wote na wasambazaji wote wameelekezwa zaidi kuacha kusambaza au kuuza bidhaa zilizotajwa hapo juu kwa mtiririko huo na kutaarifu TMDA kwa mwongozo wa kukumbuka.

“Ikumbukwe kwamba kusimamishwa ni kwa bidhaa tatu zilizoorodheshwa hapo juu na kwamba bidhaa zingine zilizo na ranitidine za viwanda vingine hazijasimamishwa na zinaweza kutumika.

“Watumiaji bado wanakumbushwa kuwaarifu TMDA kuhusu athari yoyote mbaya ya dawa (ADR) ambayo inaweza kutokea kwa sababu ya matumizi ya dawa hizi au dawa zingine zozote kama sehemu ya mfumo wake wa maduka ya dawa,” imeeleza taaifa hiyo na kuhitimisha kuwa,

“Ikumbukwe pia kwamba kusimamishwa, kupiga marufuku na kukumbuka kwa bidhaa za ranitidine zilizo na uchafu N-nitrosodimethylamine kwa sasa zinaendelea katika nchi nyingine nyingi duniani,” ilisema.

Chanzo: Mtanzania
 
Raniplex 150 mg inayozalishwa Cyprus, Rantac 500 mg/mL na Aciloc 150 mg zinazozalishwa nchini India.

TMDA ilisema kuwa kutokana na uchunguzi wake, imeamua kuzuia dawa hizo ili kulinda afya ya watumiaji.

Washenzi wakubwa mnakuja kuutangazia umma baada ya kuwa mmedhuru watu maelfu, mlikuwa wapi kuyafanya hayo kabla hamjaruhusu bidhaa kuingia sokoni, naishauri serikali kuwachukulia hatua wote waliohusika na janga hili, siku zote tunasisitiza umakini katika kulinda afya za watu lakini mnaendekeza rushwa kwanza, je ni raia wangapi wamedhurika na madawa mengine ukiacha haya mnayozungumzia?
 
Waliokufa tayari kwa kudhuriwa na dawa hizo ni wangapi? TMDA kuanzia sasa sita waamini tena.
 
Waliokufa tayari kwa kudhuriwa na dawa hizo ni wangapi? TMDA kuanzia sasa sita waamini tena.

Wanakula rushwa huko kwa wahindi, wanafanyia majaribio kwa inocent people! Hii mamlaka inatakiwa kufutwa kabisa na wahusika kuwekwa ndani haitufai, nchi zingine hawaruhusu kabisa raia wao kuchezewa hata kwa blood slide ya malaria, sisi thamani yetu imekuwa chini kuliko kinyesi!!
 
“Ikumbukwe pia kwamba kusimamishwa, kupiga marufuku na kukumbuka kwa bidhaa za ranitidine zilizo na uchafu N-nitrosodimethylamine kwa sasa zinaendelea katika nchi nyingine nyingi duniani,” ilisema.

Stupid and shut up!!
Kama wengine wameamua kula kinyesi kwa shida zao unaunatumia sababu hiyo kudhoofisha hoja!!?
 
Hapa ndipo nataka rais wetu awe mkali na hawa washenzi wanaokula rushwa kutoka viwanda vya wahindi kwa ajili ya kuleta madawa yao yaliyokataliwa hko nchi zingine. Hawa wataalamu wetu wanajali hela tu wanaweza kuwauza watanzania wote kwa ajili ya kukubali madawa ya majaribio. Yaani leo ndio mnakuja kutuambia huu utumbo? Washenzi kabisa, mnapaswa kuhukumiwa kifo kama wauaji wengine. Pumbavu zenu.
Mheshimiwa rais nakuomba utulinde na uwe mkali na hii idara ya serikali wanawaua watanzania kwa vipande vya fedha
 
Elimu kwa jamii inahitajika sana kwenye hili eneo. Tusiwalaumu TMDA, walichokifanya kinafanyika ulimwengu mzima. Dawa ikishagunduliwa inapitia kwenye majaribio tofauti/ clinical trials na ikikidhi vigezo husika husajiliwa na mamlaka husika. Baada ya kusajiliwa, huanza kufuatiliwa/ post marketing surveillance, na kama ikionyesha kuna tatizo huondolewa. Ranitidine sio ya kwanza na haitakuwa ya mwisho. Kuna madhara ambayo huchelewa kuonekana......ni bahati mbaya ila ndivyo ilivyo kwenye ulimwengu wa dawa......
Washenzi wakubwa mnakuja kuutangazia umma baada ya kuwa mmedhuru watu maelfu, mlikuwa wapi kuyafanya hayo kabla hamjaruhusu bidhaa kuingia sokoni, naishauri serikali kuwachukulia hatua wote waliohusika na janga hili, siku zote tunasisitiza umakini katika kulinda afya za watu lakini mnaendekeza rushwa kwanza, je ni raia wangapi wamedhurika na madawa mengine ukiacha haya mnayozungumzia?
 
Elimu kwa jamii inahitajika sana kwenye hili eneo. Tusiwalaumu TMDA, walichokifanya kinafanyika ulimwengu mzima. Dawa ikishagunduliwa inapitia kwenye majaribio tofauti/ clinical trials na ikikidhi vigezo husika husajiliwa na mamlaka husika.

Kwanini walijiridhisha na kuiruhusu bila kujipa muda mrefu wa kutosha kuifuatilia? Je kuna dawa ngapi mbaya tumekula kutokana na sababu kama hizo za kwamba madhara yamekuja kugundulika baadaye?
 
mm natumia Omoprozole sijui ina madhara yani Kwakweli ni bora kutumia chakula tiba tu kuliko Haya makemikali
 
Mkuu kuna madhara ya dawa ambayo huwezi kuyapredict based on the chemical group or chemical structure ya dawa husika. Kwa lugha rahisi madhara mengine hayajulikani, na huchukua muda sana kutokea hasa baada ya kutumika kwenye population kubwa.....ndio sababu ya hiyo post marketing survaillance.....na ni practice dunia nzima....ni vigumu kueleweka lakini ndio hivyo....vinginevyo tusingekuwa na dawa kabisa kama tungesema tusubiri kuthibitisha uwepo au kutokuwepo kwa hayo madhara ambayo hutujui kama yatatokea au kutotokea.....
Kwanini walijiridhisha na kuiruhusu bila kujipa muda mrefu wa kutosha kuifuatilia? Je kuna dawa ngapi mbaya tumekula kutokana na sababu kama hizo za kwamba madhara yamekuja kugundulika baadaye?
 
Mkuu Omeprazole na dawa nyingine zilizosajiliwa na TMDA zinafaa kutumika kama inavyoelekezwa na daktari. Dawa zina madhara madogo / side effects ambazo ziko documented na daktari/ mfamasia atakuwa amekueleza wakati anakupa. Ninaaamini unaitumia kwa maelekezo na chini ya uangalizi wa mtaalam wa afya. Kama utaona kuna tatizo lolote rudi kwao watajua la kufanya. Hili la Ranitidine yenye hizo brand names ni tatizo kubwa lililofanyiwa ufuatiliaji wa muda mrefu dunia nzima.
mm natumia Omoprozole sijui ina madhara yani Kwakweli ni bora kutumia chakula tiba tu kuliko Haya makemikali
 
mm natumia Omoprozole sijui ina madhara yani Kwakweli ni bora kutumia chakula tiba tu kuliko Haya makemikali

Hapo kwenye the so called “vyakula tiba” ndo wajanja washawaokota wanawapiga sawa sawa, kuna wale kina Mwaka na Fiterawa na kwa sasa Mchina hayupo nyuma.... zingatia ushauri wa kitaalamu acha hofu utapigwa kweli kweli.
 
Huku kwetu ndiyo bara la majaribio ya dawa kabla ya wao kutumia
 
Binafsi dawa za India huwa nazitilia mashaka sana; kwa bahati mbaya ndo zimejaa mahospitalini kwetu. Ishu kama hii ingetokea kule Ulaya, mbona kesi za madai zisingetosha?
 
Elimu kwa jamii inahitajika sana kwenye hili eneo. Tusiwalaumu TMDA, walichokifanya kinafanyika ulimwengu mzima. Dawa ikishagunduliwa inapitia kwenye majaribio tofauti/ clinical trials na ikikidhi vigezo husika husajiliwa na mamlaka husika. Baada ya kusajiliwa, huanza kufuatiliwa/ post marketing surveillance, na kama ikionyesha kuna tatizo huondolewa. Ranitidine sio ya kwanza na haitakuwa ya mwisho. Kuna madhara ambayo huchelewa kuonekana......ni bahati mbaya ila ndivyo ilivyo kwenye ulimwengu wa dawa......
umejibu vyema. umewahi kuwa Principle Investigator?
 
Vipi kuhusu dawa inayoitwa Cemetidine(Tagament) nayo ni vipi,maana naona kama majina yanafanana..?
 
Back
Top Bottom