Serikali yapiga marufuku kutumia karatasi kama njia ya kuidhinisha maombi ya dawa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amepiga marufuku kwa watumishi wa afya katika vituo vya kutolea huduma za afya kutumia karatasi kama njia ya kuidhinisha maombi ya dawa.

Dkt. Ndugulile ametoa marufuku hiyo maara baada ya kubaini mianya ya upotevu wa dawa za Serikali katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini alipokuwa ziarani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi)

“Ni marufuku kuanzia sasa kutumia karatasi za daftari kuomba dawa kutoka idara moja kwenda nyingine, tuandae fomu maalum za maombi” Amesema Dkt. Ndugulile

Ameagiza kuwa dawa zote zinazopatikana katika vituo vya kutolea huduma ziwekwe kwenye fomu za maombi (reiquizitaion form) huku zikionyesha jina la aliyeomba pamoja na kusaini kuthibitisha maombi yake ya dawa.

Amesepa pia mtu au idara ya famasi inayopoke maombi hsyo anatakiwa kuhakikisha maombi hayo na kusaini fomu hiyo.

“Ni marufuku kwa mtu wa famasi kujiongezea dawa kwa maneno ya mdomo au kuambiana, na atakayepokea dawa hizo pia anatakiwa aandike jina lake na kusaini.

Hatua hiyo inakuja mara baada kubaini mianya ya upotevu wa dawa za Serikali ambapo Dkt. Ndugulile amesema “Serikali imewekeza nguvu kubwa sana katika upande wa dawa, lakini pia nyie wataalam ambao mnasimamia mnatakiwa kuhakikisha mnaweka kumbukumbu zenu sahihi ili kudhibiti mianya ya upotevu wa dawa”

“Hapa nnapata mashaka kuwa kuna uptevu wa dawa za Serikali tujirekebishe na kuhakikisha tunatunza vzuri kumbukumbu zetu” Amesema Dk. Ndugulile na kuwataka kuhakikisha wanaweka mifumo ya TEHAMA katika kusimamia maombi ya dawa.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi) Dkt. Jumanne Karia amesema wamepokea maelekezo hayo na kuahidi kuyatekeleza mara moja.
 
Hilo la serikali kuwekeza nguvu nyingi kwenye madawa naungana na serikali kwa 100%, wamefanya kazi nzuri sana.

Sasa biashara ya pharmacy inaelekea kufa kwa sababu ya hatua ilizochukua serikali kuagiza yenyewe madawa kutoka kwa manufacturers.

Wahindi walikua waagiza dawa alafu wanaweza margin ya 70% faida. Sasa wanaelekea kufilisika.
 
Kwa nini hawatumii computer, ila tatizo la website za serikani ni hamna update,ukifungua unaweza kukuta mambo na tarehe ya miezi zaidi ya sita nyuma, haya mambo ya karatasi sijui kusaini hayatasaidia wizi wataiba tu, bila kwenda na tech ni kazi bure.
 
Back
Top Bottom