Serikali yapiga marufuku kusambaza mafuta ya mashoga

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,452
Serikali imepiga marufuku miradi inayohusisha utoaji wa vilainishi kwa mashoga kama njia ya kukinga kundi hilo na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera baada ya kuzindua wodi ya wazazi, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema suala hilo halikubaliki na ni kukiuka miiko na maadili ya Watanzania.

Amesema mashirika yasiyo ya Kiserikali yanaweza kutumia njia nyingine mbadala za kudhibiti maambukizi ya Ukimwi na siyo kutoa vilainishi ambavyo kwa upande wa pili vinaweza kuwa vinachochea tatizo hilo.

Awali, akizungumza katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, waziri huyo amesema kuwa Serikali iko mbioni kuandaa muswada wa sheria utakaowasilishwa bungeni ili kutunga sheria itakayomlazimisha kila mwananchi kuwa na bima ya afya.

Chanzo: Mwananchi
 
Chanzo: mwananchi
Sasa kuwanyima vilainishi vyao si kutaleta friction na hatimaye maambukizi mapya ya VVU? Hapo si tutakuwa tunaihujumu TACAIDS? Au sijaelewa kazi ya vilainishi hivyo?
 
Nchi hii kuna mambo mengi saana muhimu lakini sasa hivi tumejikita kutangaza USHOGA. Kiufupi serikali inatangaza hili suala maana kuna baadhi hata hawakujua kuna tatizo hili. Tushughulikie mambo muhimu haya mengine tuyaache
 
Jamaa walikuwa wanapatiwa mafuta kama magari ya mawaziri
86324faa7f48e00b0b4375fc51807967.jpg
 
Kwani ky si inauzwa madukani? au..

bora wangekataza isiwepo madukani ibaki ni kwa ajili ya matumizi ya hospitali tu kama dawa nusukaputi
 
Back
Top Bottom