Serikali yapiga marufuku Hospitali Binafsi kupandisha bei kwa wagonjwa wenye matatizo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,763
Prof. Mchembe amesema serikali imepiga marufuku hispital binafsi kupandisha bei kwa wagonjwa wenye matatizo ya kupumua.

Prof. Mchembe amesema ameona kwenye mitandao baadhi ya hospital zimeongeza bei na kutahadharisha kuwa siyo kila mwenye matatizo ya kupumua ana Corona.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!.

===
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Prof. Mabula Mchembe amezionya hospitali binafsi kutoza bei kubwa kwa wagonjwa wa matatizo ya kupumua

Prof. Mabula amesema sio kila tatizo la kupumua ni CoronaVirus wakati mwingine inaweza kuwa ni pumu au matatizo ya moyo

Amesema hivi karibuni kuna hospitali iliandika gharama ya Tsh. 600,000 kwa siku kwa magonjwa ya kupumua

Haoni haja ya bei kupanda kwa sababu hata kabla ya #CoronaVirus walikuwa wanatoza gharama za kawaida

Zaidi soma;


====

SIO KWELI HOSPITALI HAPA NCHINI ZIMEJAA WAGONJWA WA CORONA - PRO. MCHEMBE.

Na. Rayson Mwaisemba (WAMJW - DSM)

KATIBU MKUU Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Prof. Mabula Mchembe ameweka wazi kuwa, sio kweli Hospitali zimejaa wagonjwa wa Corona kama inavyopotoshwa na baadhi ya watu wenye nia mbaya katika mitandao ya kijamii.

Prof. Mchembe amesema hayo leo wakati alipofanya ziara katika hospitali binafsi za Agakhan na Kairuki ili kukagua hali ya utoaji huduma kwa wananchi na kuongea na viongozi wa hospitali hizo lengo ikiwa ni sehemu ya maboresho ya utoaji huduma katika Sekta ya Afya hapa nchini.

"Sio kweli kwamba Hospitali hizi zimejaa wagonjwa wa Corona kama inavyosemekana kwenye mitandao ya kijamii, hospitali zina uwezo wa vitanda zaidi ya 150 lakini sio vyote vina wagonjwa na wapo wagonjwa wa kila aina wanaohitaji huduma", amesema Prof. Mchembe.

Prof. Mchembe ameendelea kwa kupongeza ushirikiano uliopo kati ya hospitali binafsi, mashirika na zile za Serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi wenye hali zote katika jamii.

"Nashukuru pia ushirikiano uliopo kati ya Hospitali binafsi na za mashirika binafsi kwa jinsi ambavyo zinashirikiana na Serikali, kikubwa ni kuwahudumia vyema wenzetu kama kawaida", amesema Prof. Mchembe.

Aidha, Prof. Mchembe ametoa onyo kwa hospitali zinazopandisha gharama za matibabu nchini bila kufuata taratibu na miongozo ya Serikali, huku akisisitiza kwamba, kuwa na tatizo la kupumua katika mfumo wa hewa sio kuumwa Corona.

"Niziase pia Hospitali, zisitumie nafasi hii, mtu kuwa na tatizo la kupumua kwenye mfumo wa hewa sio kwamba ana Corona, mbona mwanzo walivyokuwa wanawahudumia kabla ya haya yote haikuwa na gharama hizi, niwaase kwamba twende kwenye gharama ambazo zimewekwa na Serikali", alisisitiza Prof. Mchembe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Agakhan Dkt. Ahmed Jusabani ameweka wazi kuwa sio kweli Hospitali ya Agakhan imejaa wagonjwa wa Corona, huku akisisitiza kuwa wagonjwa wapo wa kila aina wakiwemo wagonjwa wa Saratani, mama wajawazito, magonjwa ya sukari na presha.

Aliendelea kusisitiza kuwa, wananchi wasikimbie huduma katika hospitali hiyo endapo watahitaji huduma, huku akisisitiza kutowachelewesha wagonjwa wanaohitaji huduma ili kuleta tija ya tiba zitazotolewa katika hospitali hiyo.

Naye, Mkurugenzi wa Hopitali ya Kumbukumbu ya Kairuki, Dkt. Asser Mchomvu amewatoa hofu wananchi juu ya tangazo la gharama za juu za matibabu hasa kwa wenye shida za mfumo wa upumuaji katika hospitali hiyo na kusisitiza kuwa tangazo hilo sio halali na hawalifahamu kwani halina muhuri wala saini ya Mkurugenzi wa hospitali hiyo.

"Zaidi ya asilimia 80 ya wateja wetu ni wa mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, nataka kuwaondolea hofu wananchi hususan wateja wetu kwamba, lile tangazo ambalo lilitoka kwenye mitandao ya kijamii, sio kweli na hata sisi tulishangaa, na lingekuwa la kwetu, lingekuwa na muhuli wa Hospitali na lingekuwa na saini yangu ili liweze kutambulika", amesema Dkt. Asser Mchomvu.
IMG-20210203-WA0114.jpg
IMG-20210203-WA0117.jpg
IMG-20210203-WA0116.jpg
IMG-20210203-WA0118.jpg
IMG-20210203-WA0115.jpg
IMG-20210203-WA0113.jpg
 
Corona ni ugonjwa kama mafua tu, dawa yake asilia inapatikana Tanzania. Dharau kujifukiza uendelee na safari yako kaburini.
 
Muhmu sana pia nina wasiwasi kuna hospitali moja inaweza fanyia majaribio ya chanjo yao hapa kutokea india nimeona dalili me mzalendo
 
Hivi huyu Professa anajitambua kweli?

Hivi kuna mwongozo rasmi wa serikali kuhusu gharama za matibabu katika hospitali binafsi?

Kama serikali haihusiki na uwekezaji katika hospitali binafsi, ni vipi iwapangie ni lini wamiliki wa hospitali binafsi wapandishe gharama?

Yeye ameshasema hakuna Corona hapa Tanzania, ni vipi tena ahoji matatizo ya kupumua kwa watanzania kama yanahusika na Corona?
 
Hakika Corona imezidi kuwa tatizo, huu ugonjwa unazitesa sana familia nyingi.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Prof. Mabula Mchembe amezionya hospitali binafsi kutoza bei kubwa kwa wagonjwa wa matatizo ya kupumua

Prof. Mabula amesema sio kila tatizo la kupumua ni CoronaVirus wakati mwingine inaweza kuwa ni pumu au matatizo ya moyo

Amesema hivi karibuni kuna hospitali iliandika gharama ya Tsh. 600,000 kwa siku kwa magonjwa ya kupumua

Haoni haja ya bei kupanda kwa sababu hata kabla ya #CoronaVirus walikuwa wanatoza gharama za kawaida
 
Safi hii imekaa vizuri!

Wenye kutaka kupansdisha bei, walitaka watoto wachanga wenye pneumonia washindwe kulaza vichanga vyao vifie majumbani?
 
Corona ni ugonjwa kama mafua tu, dawa yake asilia inapatikana Tanzania. Dharau kujifukiza uendelee na safari yako kaburini.

Kwa washirikina wote tunajua mtatumia dawa zisizo na vipimo kama kile kikombe cha babu mlichokunywa.
 
Afya hata maradhi ya kawaida hospitali za umma garama zipo juu na bima zetu za daraja la 3C zinatufehesha tu ije mambo ya kupumua? Wengi wetu tutajiuguza majumbani nyungu nk.
 
Labda muwatege kwa kujifanya wagonjwa lakini maagizo ya kwenye tv na you tube hawasikii ng'o!
 
Back
Top Bottom