Serikali yapiga marufuku Dawa za kuuliwa Nzi na Wadudu kupulizwa Buchani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Bodi wa nyama nchini imepiga marufuku matumizi ya dawa za kuulia nzi na wadudu wengine kupulizwa kwenye mabucha wakati nyama ikiwemo ndani ,jambo ambalo linalohatarisha maisha na afya za wanunuzi wa kitoweo hicho.

Dawa hizo ni sumu hatari zinafanya kazi taratibu ndani ya mwilini mwa binadamu na mwisho wa siku zinasababisha maradhi mbalimbali yakiwemo kansa .

Rai hiyo imetolewa na Afisa wa Bodi ya Nyama kanda ya kanda ya Magaharibi ,Joseph kulwa wakati akitoa elimu kwa wadau wa nyama katika kata ya Nata wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Alisema kuwa baadhi ya mwenye mabucha wamekuwa wakitumia dawa za kuulia wadudu kuwauwa nzi maarufu (Rungu )wakati nyama ikiwemo kwenye bucha kitendo ambacho ni hatari sana kwa walaji wa nyama .

Alisema kwamba bucha nyingi mazingira sio rafiki ni machafu hivyo nzi wanavutiwa nayo ni muhimu kwa wamiliki wa mabucha hayo weka mazingira ya usafi ilikuepukana na jambo hilo.

Alisema kwamba nikosa la jina kupulizia dawa ya kuulia wadudu kwenye eneo ambalo lina vyakula vya binadamu nani hatari hata kwa muuza nyama mwenyewe.

“Tumeamua kutoa tahadhari hiyo mara kwa mara ili kuacha kabisa kutumia dawa za kuuliza wadudu kwa ajili ya kuulia nzi wakati bucha ina nyama tutakuchua hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo”alisema Kulwa .

Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa nyama kata ya Nata, Said Salum alisema kwamba wataitumia elimu hiyo kama darasa muhimu la kuweza kupunguza mapungufu ambayo walikuwa nayo kwenye mabucha yao .

Alisema elimu waliyoipata ni elimu ambayo wengi wao walikuwa hawana hivyo ni muhimu kuifanyia kazi kwenye tasni hiyo.

Hata hivyo wafugaji wa mifugo wilayani nzega wametakiwa kuhakikisha wanasajili bucha zao ili waweze kufanya biashara ya kuuza nyama na wale ambao hawataweza kufanya usajiliwa hawataweza kufanya biashara hiyo tena .

Ippmedia
 
Kwenye hili suala naunga mkono kabisa ni hatari na itakua imelinda usalama wa watumiaji.

lakini inafikirisha na kunipa wasiwasi kama mpaka leo bado kuna butcher hazima meat saw yaani zinatumia magogo na shoka.

Sasa najiuliza kama hili limeshindikana kulimaliza je hili litafanikiwa???
 
Kuhusu misumeno, ni kweli lakini kwa umeme huu, sehemu nyingi bado wanatumia magogo!!siku hizi hawatumii dawa ya Rungu bali kuna dawa, ziko kwenye vipaketi, wanachanganya na maji, wana mwaga chini tu kwenye sakafu, babaa balaaa, nzi unawaokotaa tu!!!
 
Kwenye hili suala naunga mkono kabisa ni hatari na itakua imelinda usalama wa watumiaji.

lakini inafikirisha na kunipa wasiwasi kama mpaka leo bado kuna butcher hazima meat saw yaani zinatumia magogo na shoka.

Sasa najiuliza kama hili limeshindikana kulimaliza je hili litafanikiwa???
Tulishakula nyama iliyopuliziwa insects killer tusubiri mrejesho, kuhusu magogo na mashoka kutumika katika mabucha hii ni asili yetu na umaskini wa kimkakati unaowatawala wenye dhamana ya uongozi, wavumilie tu
 
Kwenye hili suala naunga mkono kabisa ni hatari na itakua imelinda usalama wa watumiaji.

lakini inafikirisha na kunipa wasiwasi kama mpaka leo bado kuna butcher hazima meat saw yaani zinatumia magogo na shoka.

Sasa najiuliza kama hili limeshindikana kulimaliza je hili litafanikiwa???
... meat saw? Kwa nishati hii hii ya mgao? Tunazungumzia bucha za Nakapanya na maeneo dizaini hiyo ambako nyama hupimwa kwa "kukadiria".
 
Back
Top Bottom