Serikali yapendekeza ushuru wa nywele bandia uwe asilimia 35

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,902
Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwenye nywele bandia zinazotambulika kwa Heading 6704.

Dk Mwigulu amesema hayo bungeni leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha makadilio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Serikali 2022/23

Amesema “Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwenye nywele bandia zinazotambulika kwa Heading 6704.

Hatua hii inalenga kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na kuongeza mapato ya Serikali” amesema

Amesema hatua hiyo inalenga kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na kuongeza mapato ya Serikali

"Pamoja na hayo yamefanywa mabadiliko mbalimbali ya sheria kwa kufutwa kifungu cha 5 (1) (l) cha sheria ya chakula, dawa na vipodozi na. 1 ya mwaka 2003 ili jukumu la viwango vya kitaifa libaki kwenye sheria ya viwango na. 2 ya mwaka 2009. Mahitaji ya viwango ya TMDA yatawasilishwa Shirika la Viwango Tanzania.

Source: Mwananchi
 
Wangeweka 90% ingeendeza zaidi
Ndio tungeona mwanamke nywele natural yupi naunga mkono hoja

Sema watahamia kwenye vilemba kuvaa vilemba kama mama Samia kumbe wanakwepa bei za nywele bandia

Tutarajie soko la vilemba kama vile anavyovaa mama Samia na yule Mlinzi wake soko kuwa juu kisingizio kuwa mama Samia Fashion.
 
Wana wa kiume msichekelee sasa bali jiandae kisaikolojia kupitia wallet zenu.
 
Wadangaji watakuwa na mtihani mkubwa maana wanaume wenyewe siku hizi wamestuka, hawakati hela hovyo kama zamani!

Wanasema Eti ujinga huwa wakati wa kwenda kurudi werevu !

Sijui itakuwaje?!
 
Back
Top Bottom