Serikali yapanga bei tiba hospitali binafsi

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Serikali imesema itatoa bei elekezi katika sekta ya afya hivi karibuni baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kubariki bei hizo kuanza kutumika kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wa gharama wananchi.

Bei elekezi kwa vituo vya afya zimeshasainiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na baadhi ya vituo vya afya vimeshaanza kutumia bei hiyo.

Aidha, serikali imepanga kuweka utaratibu wa wagonjwa kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangalla wakati akizungumza na waaandishi wa habari baada ya kuzindua Matokeo ya Utafiti wa Kutathimini utoaji wa huduma za afya nchini kwa mwaka 2014/2015.

“Bei elekezi ziko mbioni kutoka na baadhi ya vituo wameshaanza kuzitumia kwa sababu zimeshasainiwa na Waziri, sasa hivi tunasubiri Baraka za Waziri Mkuu akiziridhia tutazitangaza rasmi,” alisema Dk Kigwangalla.
 
Naona kama serikali inampango wa kukomoa huduma ambazo co zakiserikali kama hizo hospitali na mashule, hamna sabab ya msingi kufanya hvy zaid ya kuboresha huduma za serikali ili wananchi wapate huduma serikalini. Wangependekeza tu limitation labd kwamb tozo zisivuke zaid ya kiwango flan
 
Hii issue ina madhara zaidi kuliko faida. Nchi pekee ambayo imefanikiwa katika hili ni Japan. Lakini nayo ingawa wana regulate pricing, hili huenda sambamba na ukuzaji wa mishahara ya watumishi. Waholanzi walikuwa na hii kitu. Lakini iliwashinda walipoona ubora wa huduma za afya unashuka kila mwaka.
Mtu ambaye hajui ABC za Uchumi, hususani wa afya, atafikiria kwamba hizi hospitali zinazopata faida basi wamiliki wake watakuwa akina Bill Gates karibuni!!! Wala. Faida ndogo inayopatikana inatumika kuongeza ubora wa huduma, kama kujenga majengo mapya, kununua vifaa vipya, kuanzisha huduma mpya za kisasa, off course na kumpeleka mtoto wako shule nzuri, n.k. n.k. ila mwisho wa siku jamii ndiyo inanufaika zaidi.
 
Serikali imesema itatoa bei elekezi katika sekta ya afya hivi karibuni baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kubariki bei hizo kuanza kutumika kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wa gharama wananchi.

Bei elekezi kwa vituo vya afya zimeshasainiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na baadhi ya vituo vya afya vimeshaanza kutumia bei hiyo.

Aidha, serikali imepanga kuweka utaratibu wa wagonjwa kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangalla wakati akizungumza na waaandishi wa habari baada ya kuzindua Matokeo ya Utafiti wa Kutathimini utoaji wa huduma za afya nchini kwa mwaka 2014/2015.

“Bei elekezi ziko mbioni kutoka na baadhi ya vituo wameshaanza kuzitumia kwa sababu zimeshasainiwa na Waziri, sasa hivi tunasubiri Baraka za Waziri Mkuu akiziridhia tutazitangaza rasmi,” alisema Dk Kigwangalla.
 
Ninapinga sana serikali kuweka directive pricing ktk service sector iliyo chini ya private ownership ila nitakuwa wa kwanza kuiunga mkono ikiwa wataweka viwango vya bei kwenye bidhaa zilizoko sokoni,huku ndiko tunakoibiwa hasa nyakati za sikukuu.
 
Hii issue ina madhara zaidi kuliko faida. Nchi pekee ambayo imefanikiwa katika hili ni Japan. Lakini nayo ingawa wana regulate pricing, hili huenda sambamba na ukuzaji wa mishahara ya watumishi. Waholanzi walikuwa na hii kitu. Lakini iliwashinda walipoona ubora wa huduma za afya unashuka kila mwaka.
Mtu ambaye hajui ABC za Uchumi, hususani wa afya, atafikiria kwamba hizi hospitali zinazopata faida basi wamiliki wake watakuwa akina Bill Gates karibuni!!! Wala. Faida ndogo inayopatikana inatumika kuongeza ubora wa huduma, kama kujenga majengo mapya, kununua vifaa vipya, kuanzisha huduma mpya za kisasa, off course na kumpeleka mtoto wako shule nzuri, n.k. n.k. ila mwisho wa siku jamii ndiyo inanufaika zaidi.
Kwel kabs mkuu, madawa na vifaa vya hospital za serikali huwa hazilipiwi ushuru, lakn binafs wanalipa sana tu, istoshe bei za kununulia pia lazima ni tofaut kwamba serikali inakuw na advantage, hili ni swala la serikali kuona aibu tu kwamb kwann wapitwe kihuduma na watu binafs ama taasis zisizo za kiserikal!
 
Nitaelewa km watakuja na bei elekezi kwa maduka ya akna mangi na kanji vingnevyo upuuzi shule binafs wameishia wapi?
 
Katika soko huria hiyo kidogo inanipa walakin na pia nakubaliana na mdau G.Man
ubepari bila kudhibitiwa na dola watauza hata binadamu kama bidhaa. lazima kwa biashara kama hospitali kudhibiti au wengine watakufa kwa kushindwa kununua
aspirin
 
Safiiii... maana kuna hospitali kumuona Dr tu hasa specialist ni sh. 35,000 hapo hujatibiwa... wtf..?
Pia kulala siku moja tu ktk vitanda vya private utakuta 35,000 per night... hasa hizi hosp. kubwa...imagine...!!! So, safi sanaaaa... i was waiting this day..!! Na hapo sio ICU mind you...!!

Very good... lazima kila kitu kiwe na Limits... haiwezekani huduma muhimu kama za afya bei ziwe free kama Guest house... hapana..!!! Serikali weka bei elekezi kama Shule za Private vile... shule za Private naona Wizara kama imezilegezea kamba hivi... Private schools lazima pia bei za ADA zinapangwa na serikali
 
Mkuu hatusemi hospitali ziwe zinapata faida za kutisha. Nao wanapata faida kama biashara za kawaida, ambazo mwisho wa siku zamuwezesha mmiliki kumpeleka mtoto shule, kujenga nyumba, kununua gari n.k. Lakini faida kubwa huenda kwenye investment. Mfano nina darubini moja, nikipata faida nanunua ya pili na nzuri zaidi. Nilikuwa nina vyumba viwili, nikipata faida naongeza kimoja. Nilikuwa nina wafanyakazi kumi, naongeza watano. Mwisho wa siku faida zote zinamrudia mwananchi.
Tuache soko li command. Serikali kama ina ubavu ipunguze gharama kwenye hospitali zake sambamba na kuboresha huduma. Wao watapunguza tu.
Uki regulate price, itadumaza huduma.
By the way, siku zote maskini hula kupitia mgongo wa mtu wa kipato cha kati na tajiri indirectly. Watu wa kipato cha kati na juu, ndio wanatoa kodi ambazo maskini hunufaika nazo. Ukimfanya mwenye kipato cha kati na cha juu asipate huduma nzuri ya afya, ati kwa sababu wataka kumu accomodate masikini, uzalishaji utapungua na huyo masikini atazidi kuwa masikini.
 
Tumesubiri bei elekezi kwenye shule binafsi hawajatoa, ada imelipwa iliile ya miaka ya nyuma, leo wamekuja na afya! looo huu sasa usanii jamani. kha, wakumbuke tu sukari imepanda bei.
 
Safiiii... maana kuna hospitali kumuona Dr tu hasa specialist ni sh. 35,000 hapo hujatibiwa... wtf..?
Pia kulala siku moja tu ktk vitanda vya private utakuta 35,000 per night... hasa hizi hosp. kubwa...imagine...!!! So, safi sanaaaa... i was waiting this day..!! Na hapo sio ICU mind you...!!

Very good... lazima kila kitu kiwe na Limits... haiwezekani huduma muhimu kama za afya bei ziwe free kama Guest house... hapana..!!! Serikali weka bei elekezi kama Shule za Private vile... shule za Private naona Wizara kama imezilegezea kamba hivi... Private schools lazima pia bei za ADA zinapangwa na serikali

Mkuu ulitaka umlipe kiasi gani specialist? Hiyo wanaita consultation fee. Na ndio tiba haswaa. Mkiongea na kupimwa na daktari, anakuwa amepata clue ya ugonjwa wako kwa zaidi ya 80%. Vipimo ni ku confirm. So consultation fee ni gharama za kutumia kichwa cha mwenzako aliyesoma kitu usichojua. Iko field zote. Mbona hulalamiki kutoa elfu 5 kwa kila sahihi moja ya mwanasheria?
 
Mkuu ulitaka umlipe kiasi gani specialist? Hiyo wanaita consultation fee. Iko field zote. Mbona hulalamiki kutoa elfu 5 kwa kila mhuri mmoja wa mwanasheria?

Sasa ndio mtakoma... Wizi mlikuwa mnafanya ktk AFYA ZA WANANCHI... Consultation fees kwani KUNA UJENZI AU USHAURI WA KUJENGA GHOROFA AU MELI AU KUANZISHA INTERNATIONAL COMPANY...

That was PURELY THEFT....

Mwisho wenu umefika sasa... nakuona unatetea tumbo lako hapa... SERIKALI IMESHA FINALISE BEI ELEKEZI FOR PRIVATE HOSPITALS... ww utazuia...?

Mwisho, mliharibu kupanga bei za ajabu sana..... kwa kujificha mnatoa HUDUMA... but AFYA si jambo la mchezo mchezo... so ukiona hosp. biashara hailipi FUNGA... fungua GUEST kisha panga bei unayotaka...

I love my Govnt...!!! Safiii kabisaa
 
Tanzania tuna practice mixed economy ambapo gvt inaweza kufanya intarvation
"Advantages of Mixed Economies - Most business and industry can be left to private firms. Private firms tend to be more efficient than government controlled firms because they have a profit incentive to cut costs and be innovative"

"The Advantages of a Mixed Economy. A mixed economy permits private participation in production, which in return allows healthy competition that can result in profit. It also contributes to public ownership in manufacturing, which can address social welfare needs."
 
Sasa ndio mtakoma... Wizi mlikuwa mnafanya ktk AFYA ZA WANANCHI... Consultation fees kwani KUNA UJENZI AU USHAURI WA KUJENGA GHOROFA AU MELI AU KUANZISHA INTERNATIONAL COMPANY...

That was PURELY THEFT....

Mwisho wenu umefika sasa... nakuona unatetea tumbo lako hapa... SERIKALI IMESHA FINALISE BEI ELEKEZI FOR PRIVATE HOSPITALS... ww utazuia...?

Mwisho, mliharibu kupanga bei za ajabu sana..... kwa kujificha mnatoa HUDUMA... but AFYA si jambo la mchezo mchezo... so ukiona hosp. biashara hailipi FUNGA... fungua GUEST kisha panga bei unayotaka...

I love my Govnt...!!! Safiii kabisaa

Khaaa. Nilijua naongea na great thinker kumbe napoteza muda. Kwa hiyo consultation fee ipo ujenzi tu (engineers) au kuanzisha company (lawyers)? Utachekwa kaka, walau uwe wasoma kabla ya kujibu. Usitawaliwe na mihemko. Usidhani wewe ndio uko karibu sana na serikali.
 
Safiiii... maana kuna hospitali kumuona Dr tu hasa specialist ni sh. 35,000 hapo hujatibiwa... wtf..?
Pia kulala siku moja tu ktk vitanda vya private utakuta 35,000 per night... hasa hizi hosp. kubwa...imagine...!!! So, safi sanaaaa... i was waiting this day..!! Na hapo sio ICU mind you...!!

Very good... lazima kila kitu kiwe na Limits... haiwezekani huduma muhimu kama za afya bei ziwe free kama Guest house... hapana..!!! Serikali weka bei elekezi kama Shule za Private vile... shule za Private naona Wizara kama imezilegezea kamba hivi... Private schools lazima pia bei za ADA zinapangwa na serikali
mkuu, kwani muhimbili kumuona specialist ni tsh ngapi?
 
Back
Top Bottom