Serikali yapandisha bei ya zao la Cacao mpaka Tzs 5015 kwa kilo

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
327
414
Mnada wa Cacao wenye Catalogue no 10 ya 2021/2022 umefanyika Mkoani Mbeya Wilayani Kyela, Mwambusye Amcos mnamo tarehe 06/09/2021. Jumla ya uzito ni kg 266,980, bean count 88, slate 1.9, flate 1.0, mould 0.2.

Bei tsh 5015 per kg Mzigo kwa bei hiyo Thamani yake ni Tsh.Bilion 1,338,904,700/= Ahsante Mhe Rais kwa kusimamia vyema ushirika na wananchi kupata bei nzuri kutoka 2500 Mpaka 5015 kwa kilo moja Bei ya Cacao.

Kazi iendelee na Mhe Rais wetu Mpendwa Samia Suhulu Hassan.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Zuberi Homera.
 
Kapandishaje?

Yeye binafsi amefanya kitu gani hadi bei imepanda?
Apandishe na mahindi kama anao huo uwezo.
Wakulima wa mahindi wanasaga meno kwe bei ndogo ya mahindi.

Hili la cash crops ni sawa maana wamewalalia sana na serikali kukosa fedha za kigeni

Haya mazao ya chakula tunauziana wenyewe ni sawa tu
Ila sio Cocoa, Korosho, mbaazi na dengu, Tumbaku, hayo yapande sana tu
 
Cacao ndio zao gani hilo? Isije ikawa bei za kisiasa tukaanza kuzungushana kwenye malipo
 
Kapandisha how?

Kwa kutoa Ruzuku / Subsidy au Soko la Dunia bei imepanda au walikuwa wanawaibia hapo nyuma sasa wameamua kuwapa haki yao?
 
Matumizi ya anasa ya serikali yanaumiza wanyonge..mafuta kupikia Bei juu, gesi majumbani Bei juu, vifaa vya ujenzi Bei juu, TOZO wanajinasibu kujenga vituo vya afya na barabara..usanii

Je Madini, utalii, bandari, gesi asilia?

Viwanda...

Kodi zake zinaenda wapi?
 
Bilioni ngapi? hebu rekebisha hapo.

Amepandisha sawa ni nani aliyeshusha?
 
BEI YA KAKAO ( COCOA) NI ZAIDI YA SHANGWE SASA NI TZS 5,000/Kg KUTOKA TZS 2,000/Kg FY2020|21

__________________________________

Kuna baadhi ya wazembe wache wa kufikiri wanasema kupanda ghafla kwa bei ya mazao hasa ya kibiashara nchini wakati huu wa Rais Samia Suluhu Hassan ni Matokeo ya Lock down ya CORONA,No hii si Sahihi na sikweli,Watu hawa Kwanini wasijiulize why bei hii haikupanda wakati Ule zaidi ya 3/4 ya dunia ilikuwa imejifungia ndani kwa "Lock down "wakiwa "Hawapandi wala Hawavuni " Kwanini Leo, ipande hasa kwa mazao yote ya kibiashara wakati huu ambao dunia yote iko nje na Rais ni Samia Suluhu Hassani? Ukweli ni kwamba wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania wamemuamini sana Rais Samia Suluhu Hassan hasa kwa kuondoa milolongo ya tozo|kodi zaidi 232 zilizoisababishia serikali kupoteza mapato yanayozidi Tshs 55BL na hii ndio dhana halisi ya Mzee JK "Ukitaka kula lazima uliwe",

Rais Samia Suluhu Hassan amepandisha bei ya kakao|Cocoa kwa zaidi ya 150% yaani bei imepanda marambili na nusu zaidi ya ile iliyokuwepo hadi mwanzoni mwamwaka huu wa 2021| Baadhi wanasema haya ni matokeo ya demand|Supply fine, Lakini kwanini Leo demand iwe kubwa wakati Samia Suluhu Hassan ni rais wa JMT au demand inamwogopa Rais Samia?!

Ukweli ni kwamba demand ya Vyakula nje ni kubwa toka enzi na enzi kuliko tunavyoweza kusupply nje tatizo lilikuwa ni Urasimu|Sera zetu za kibiashara yote haya Rais Samia Suluhu Hassan ameyaweka sawa ndani ya muda mfupi,Waswahili wanasema "Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake Mpeni, Hatakama Rais Samia Suluhu Hassan si wa chama Chako.

Hata kama humuungi mkono kwa sababu zozote zile lakini kazi anazozifanya kwaajili yetu na Watoto wetu,na kwa watoto wa watoto wetu zinastahili pongezi kubwa kwani zinaacha alama kwa kizazi hiki na kile kijacho,Tumuunge mkono ili tufike kwa kuwahi,

Kazi iendelee...
 
Aina hii ya Watanzania mnaturudisha nyuma sana kwakweli.

Hivi unaelewa hata ABCs za economics mkuu? Ni factor gani zinasababisha kupanda kwa bei ya bidhaa/raw materials?

Ni rais anapandisha bei?
 
Back
Top Bottom