Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Serikali imeondoa katazo la kutokuvua samaki wazazi kuanzia sentimita 85 hivyo kuanzia kesho wavuvi watavua samaki hao bila kukamatwa.
Aliyetangaza kuondoa katazo hilo katika kijiji cha Kikumbaitale wilayani Chato mkoani Geita ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, wakati akizindua ushirika wa chama wavuvi wa mwalo wa Kikumbaitale na kuwakabidhi hundi ya shilingi milioni tano ikiwa ni kuwawezesha kukuza mtaji.
Hatua hiyo imefuatia matokeo ya utafiti uliofanyika na kubaini nchi za Kenya na Uganda hazikatazi samaki wazazi kuvuliwa, kwakuwa wakipelekwa sokoni wanapata wateja, huku wafanyabiashara wa nchini wanapopeleka samaki zao katika nchi hizo hukosa wateja.
"Wavuvi Serikali imesikia kilio chenu cha muda mrefu, hivyo imeruhusu uvuaji wa samaki kuanzia sentimita 85 na kuendelea, lakini bado mchakato unaendelea wa kuangalia namna gani ya kuruhusu samaki aina ya ngele, gogogo na furu na kuwekwa kwenye utaratibu wa sheria na kanuni", alisema Ulega