Serikali yaondoa hofu ya ‘mchele wa plastiki’

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939

Wana Jf
Salaam



Dar es Salaam. Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), imewatoa hofu Watanzania kuhusu taarifa zilizozagaa kuwa kuna mchele unaotengenezwa kwa plastiki kutoka nchini China, unaodaiwa kuuzwa katika maduka mbalimbali.

Pia, imekanusha uwapo wa viwanda vya kichina vinavyotengeneza mchele huo.

Hata hivyo, wafanyabiashara wa nafaka walisema kuna mchele unaolimwa Mbeya unaoitwa ‘mchele wa plastiki kutoka Mbeya’.

Meneja Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma kutoka TFDA, Gaudensia Simwanza alisema hakuna ukweli wowote juu ya taarifa hizo bali ni uzushi wa watu waliokosa kazi na wanaotaka kuwachanganya na kuwatia hofu Watanzania.

“Kwanza naomba niulize hivi mchele wa plastiki ukiupika unaiva? Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kuununua mchele wa aina hiyo? Kama yupo tunaomba ajitokeze aseme na atupe ushahidi wa kujitosheleza,” alisema.

Kwa zaidi ya wiki moja sasa kumekuwapo na taarifa za kuwapo kwa mchele huo, unaotengenezwa kwenye viwanda vya raia wa China.

Taarifa hizo zilidai mchele huo hutengenezwa kwa kutumia chupa za plastiki na mifuko ya plastiki, nyingine zilienda mbali zaidi na kudai kuwa mchele huo unatengenezwa kwa kutumia mifuko ya sandarusi. Pia, video fupi ilizagaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha kijana akiwa ndani ya kiwanda kinachotengeneza mchele huo kwa kutumia mifuko ya plastiki akiifanya kazi hiyo.

Hata hivyo, Simwanza alisema video inayoonekana kwenye mitandao haina uhusiano wowote na kutengeneza mchele wa aina hiyo.

Alisema kuna viwanda vinavyotengeneza chupa za plastiki, kalamu na bidhaa mbalimbali za plastiki ambazo huchakata plastiki zilizotumika kwa kusagwa na kuwa katika vipande vidogo kama mchele kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zingine.

“Naomba niwatoe hofu Watanzania hakuna kitu kama hicho, kwanza Tanzania tuna mchele mwingi wa kutosha, hatujafikia hatua ya kula mchele wa plastiki, pia wananchi wasipende kuamini sana taarifa za kwenye mitandao,” alisema.

“Ukiangalia sasa hivi pia kuna video inasambaa ikimuonesha mwanamke akionyesha vidonge feki hizi zote ni uzushi, kama TFDA hatuwezi kuona kitu kikubwa kama hicho na kufumbia macho au tukakaa kimya.”

Wafanyabishara nao wakanusha

Mwananchi ilitembelea maduka mbalimbali ya nafaka na kuwahoji baadhi ya wafanyabiashara katika maeneo ya Tandika, Mbagala na Kariakoo.

“Dada (Mwandishi) mchele unaouzungumzia wewe haupo labda unataka mchele wa VIP au ule wa Mbeya kwa huu wa VIP ulishapigwa marufuku na haupo hata ukiupata unauzwa kwa kificho sana,”alisema mfanyabiashara wa mchele soko la Tandika, Japhet Jonh.

Mussa Juma, mfanyabiashara wa mchele soko la Mbagala alisema hajawahi kuuona mchele huo licha ya kuwa anasikia kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna mchele wa plastiki.

“Dada mimi sijauona mchele wa aina hiyo hata ukiangalia hapa kwangu nakuruhusu kagua hakuna dada taarifa nyingine ni za uongo mimi siamini kama kweli mchele wa aina hiyo upo, kwanza ukiupika si utaujua tu,” alisema.


Mchele wa plastiki wa Mbeya upoje?

*Wafanyabiashara hao walisema mchele unaoitwa wa plastiki wa Mbeya unalimwa eneo ambalo halina maji mengi (unamwagiliwa) tofauti na mchele wa kawaida.

*Ukishavunwa unakaushwa kiwandani au kwa kutumia mashine maalumu ya kukaushia mchele, tofauti na mchele mwingine ambao unakaushwa kwa kutumia mwanga wa jua.

*Mchele huu ukishakaushwa husagwa kawaida na kufungwa kwenye viroba vya kilo 50.

*Unaitwa mchele wa plastiki kwa sababu ya umbo lake ni nene na unapopikwa huvimba sana.

*Pia jina lingine la mchele huo huitwa Kipunga.

Chanzo: Mwananchi
 
Virusi vya Dhika tulitolewa hofu hivyo hivyo, leo kila watoto wanaozaliwa asilimi 45 wanaviruhi hivyo, huoni kuna tatizo hapo la kutoana hofu ya kuhisi?
Mimi upande wangu nina hofu basi,
 
Mimi ni mwendo wa ugali tu au mpunga anaolima bibi naenda kukoboa mwenyewe
 
Back
Top Bottom