Serikali yaombwa kuwekeza fedha katika utafiti wa mbegu za mafuta ikiwemo Alizeti na Ufuta

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Serikali imeombwa kuwekeza fedha katika utafiti wa mbegu za mafuta ikiwemo Alizeti na Ufuta, badala ya kuwategemea wafadhili ambao licha ya kugoma kuwekeza katika mazao hayo wamekuwa na masharti magumu.

Kauli hiyo imetolewa na mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele, HAPPY DAUDI ambaye amesema nchi haiwezi kuendelea bila ya kuwekeza katika utafiti.

Amesema mazao ya alizeti na ututa mara nyingi wafadhili wamekuwa wakigoma kufadhili utafiti wake, kwa madai mazao hayo ni ya biashara na hivyo watafiti kukosa bajeti ya kuyafanyia utafiti hasa pale yanapovamiwa na magonjwa.

Kufuatia hilo ameiomba serikali kuona umuhimu wa kuwekeza fedha katika mazao hayo badala ya kutegemea wafadhili pekee ambao licha ya kutoa fedha kwenye mazao mengine wanakuwa na malengo yao na hivyo wanalazimika kufuata masharti ya mfadhili.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugeunzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele, Dakta. OMAR MPONDA amesema mkutano huo uliowakutanisha maafisa kilimo na wadau wa kilimo lengo lake ni kutoa mrejesho dhidi ya tafiti zilizofanyika mwaka 2016-2017 kupitia kituo hicho.



ITV
 
Dah, Thread kama hizi hazinaga wachangiaji kabisa. Ajabu yakeThread kama za kina Doctor Shika ndio zina watu!
 
KILIMOORGANO Ltd. Dar-es-Salaam,Tanzania.

Kutana na mtaalamu wa kilimo kutoka Dar es Salaam Tanzania anayekuza miche ya migomba, mananasi na mimea mingine zaidi ya milioni moja katika maabara ili kuiuza ndani na nje ya Tanzania. Mimea hiyo ya kutoka maabara hiyo huzalisha mavuno bora marudufu na kuongeza kipato kwa mkulima .

source: DW KISWAHILI
 
Back
Top Bottom