Serikali yaombwa kuingilia mgogoro Bulyanhulu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Serikali yaombwa kuingilia mgogoro Bulyanhulu

na Hellen Ngoromera
Tanzania Daima

SIKU kadhaa baada ya Kampuni ya Barrick inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama kutangaza kuwafukuza kazi wafanyakazi wa mgodi huo, na kusimamisha uzalishaji kwa muda usiojulikana, Chama cha Wafanyakazi wa Migodi, Nishati, Ujenzi na Kazi Nyingine (TAMICO) kimeitaka serikali kuingilia kati mgogoro baina ya wafanyakazi na mwekezaji huyo.
Tamico imeitaka serikali hiyo kurekebisha sheria ambazo chama hicho kinadaiwa kuwa ni mbovu na zilizoshindwa kuwanusuru wafanyakazi hao.

Mgogoro uliosababisha wafanyakazi hao kugoma, unatokana na masuala mbalimbali yakiwamo ya kukiukwa kwa mkataba kuhusu masuala mbalimbali kati ya wafanyakazi na mwajiri huyo - malipo maalumu kwa kazi hatarishi, utoaji wa kivutio maalumu (bonus) kwa mwaka na nyongeza ya mishahara isiyo na ubaguzi.

Mwenyekiti taifa wa Taimico, Mbaraka Igangula, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa pamoja na mambo mengine, mgomo uliofanywa na wafanyakazi walio chini tawi la Tamico ulikuwa halali kwa kuwa walifuata taratibu za kufanya mgomo huo.

"Nchi hii tumeingiliwa na wawekezaji na kwa kweli wanaharibu. Katika hili serikali iingilie kati, irekebishe sheria wanazoona ni mbovu," alisema Igangula.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, wafanyakazi hawatarudi kazini hadi watakapozungumza na mwajiri na kuwa wapo tayari wakati wowote kuendelea na mazungumzo ya pamoja hadi kufikia muafaka.

Alisema makubaliano ya pamoja juu ya ajira yalitiwa saini chini ya usimamizi wa Ofisa Kazi wa Wilaya ya Kahama, Februari 16, mwaka huu, na yalikuwa baina ya viongozi wa chama na uongozi wa mgodi huo.

"Ukiukwaji ulianza mwanzoni mwa Septemba, mwaka huu, kwa mwajiri kuamuru kuwarudisha wagonjwa wote kutoka katika hospitali za rufaa kama walivyokuwa wamepangiwa kwa matibabu kuonana na mabingwa.

"Septemba 22, mwaka huu, chama (tawi) kilikaa na mwajiri na kutoa malalamiko ya ukiukwaji na alikiri na kusema kwamba hafanyi kazi kwa maelekezo ya Tamico, hivyo atashughulikia ajali tu zinazotokea migodini," alisema mwenyekiti huyo.

Pamoja na mambo mengine, Igangula alisema kumekuwa na ubaguzi wa masuala mbalimbali na kubainisha kwa mfano kuwa raia wa kigeni (Wazungu) walioajiriwa na kampuni hiyo hupewa bonasi ya asilimia 20 ya mshahara kwa mwaka, wakati mfanyakazi Mtanzania hapati chochote.

Alibainisha kuwa kwa upande wa nyongeza ya mishahara kima cha chini kwa mfanyakazi wa Kizungu ni dola 20,000 za Kimarekani (sawa na zaidi ya sh milioni 24 kwa mwezi) wakati mshahara wa mfanyakazi Mtanzania ni dola 4,000 za Kimarekani.

Igangula alisema baada ya tofauti hizo chama kilimwomba mwajiri kufanya mkutano kurekebisha hali hiyo Oktoba 5, mwaka huu, ili utekelezaji wake uwe umefikiwa ifikapo Oktoba 8, vinginevyo chama hicho kingeanza taratibu za kisheria za kufanya mgomo.

Alisema baadaye mwajiri alitupilia mbali maombi yao yote na kusema hawezi kutimiza hata moja. Ndipo Oktoba 11 alipewa notisi ya wiki moja kwamba siku chache baadaye wafanyakazi wataanza mgomo.

"Sheria ya ajira ilizingatiwa na kifungu cha 80(2) (a) na (b) na (3) kilihusika. Oktoba 12 fomu maalumu za kugoma zilipitishwa na mpatanishi (commissioner for mediation, Arbitration-CMA), mpatinishi alijaribu kusuluhisha na tulikubaliana masuala kadhaa kama kuondoa ubaguzi na mpango wa bonasi ulipwe Oktoba 18…tulikubalina pia masuala mengine yaingie kwenye mazungumzo," alisema.

Alisema Oktoba 24 mwajiri aliomba kufanyika kikao ili kuondoa utata kwa wafanyakazi na wanachama na kwamba majadiliano yataendelea Oktoba 25.

"Mwajiri kupitia vyombo vya dola alileta kikosi cha FFU wakati mkutano halali unaendelea, wafanyakazi walianza kuhofu kuwapo kwa FFU maana kwa kufanya hivyo kuwapo kikosi hicho kulisababisha wafanyakazi waogope.

Mwajiri aliombwa kifanyike kikao mezani pamoja na viongozi wa chama Oktoba 25 lakini alikataa," alisema. Aliongeza kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Brigedia Jenerali mstaafu Kevin Msemwa, na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali mstaafu Dk. Yohana Balele, waliwakutanisha pamoja viongozi wa Tamico na wa mgodi, lakini hakukuwa na mafanikio.
 
Hawa nao wazembe, waajiri hawashawishi kwa kubembelezwa, never happened. Migomo ndiyo njia pekee ya kumfanya mwajiri ainame, na migomo ya waliogawanyika haiwatishi waajiri. Kama wafanyakazi wa sekta ya madini katika migodi yote ya barrick wakigoma na kuzuia kazi kufanyika and hence paralyse the mining industry waajiri watalazimika kucompromise.
 
Back
Top Bottom