Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Serikali yaomba mapendekezo uanzishwaji viwanda
Wizara ya Fedha na Uchumi imewaomba wafanyabiashara nchini kupeleka mapendekezo ya namna ya utekelezwaji wa miradi mikubwa ya uchumi.
Imesema kuwa mojawapo ya miradi hiyo ni mradi wa reli ya kati pamoja na utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa uchumi wa viwanda kupitia uanzishwaji wa viwanda vidogo, vya kati pamoja na vile vya kimkakati.
Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt Philip Mpango, ametoa ombi hilo jijini Dar es salaam leo, katika mkutano wake na wafanyabiashara, mkutano ambao waziri huyo alitoa mwelekeo wa mipango ya ukuaji wa uchumi, sambamba na ushirikiano baina ya serikali na wafanyabiashara, huku wafanyabiashara nao wakiieleza serikali kero zao.
Kwa upande wake, mwakilishi kutoka sekta binafsi Bw. Salum Shamte amepongeza hatua ya wizara ya fedha kukutana na wadau wa sekta ya biashara na kwamba wao kama wafanyabiashara watashirikiana na serikali kwa lengo la kuhakikisha kunakuwa na ustawi wa biashara pamoja na uchumi endelevu.
Source: EATV