Serikali yaomba madaktari nje ya nchi, BILIONI 200 ZATENGWA KUWALIPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yaomba madaktari nje ya nchi, BILIONI 200 ZATENGWA KUWALIPA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Imany John, Jun 30, 2012.

 1. Imany John

  Imany John Verified User

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  SERIKALI imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.

  Habari kutoka katika moja ya vyanzo vya kuaminika
  zimesema kuwa uamuzi huo wa serikali ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri
  kilichokutana mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

  Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa RaisKikwete alikerwa na tabia ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi zote
  zilizofanywa kuboresha maslahi yao.

  Kwa mujibu wa habari hizo,kiasi cha sh bilioni 200 kimetengwa kwa ajili yakuwaleta na kuwagharimia madaktari hao wa nje na pia baraza limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za jeshi kama Lugalo na zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa pamoja kuagiza madaktari wastaafu wote
  warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.

  Habari zimedai kuwa
  madaktari hao wanasadikiwa watatoka katika nchi rafiki zikiwemo India, China, Cubana Afrika Kusini, na kwamba wataziba kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao
  wamegoma.

  Inaelezwa kuwa mara baadaa ya kukamilika na kuanza rasmi kwa huduma za matibabu, madaktari wa hapa
  nchini waliomo katika mgomo na wale zaidi ya 200 waliodaiwa kufukuzwa na serikali kimyakimya, watalazimika kurejeshwa
  kazini kwa masharti makali.

  Hata hivyo, uamuzi wa
  serikali kuwatimua madaktari wakati suala lao liko mahakamani, umewagawa wabunge.

  Baadhi ya wabunge walijaribu kuhoji suala hilo Bungeni,lakini walikwama baada ya
  Spika Anna Makinda kuzuiamjadala huo kwa madai kuwa suala hilo liko mahakamani.

  Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, alisema kuwa kilichofanywa na serikali nikiini macho kwani juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema serikali haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai
  kuwa kuna kesi mahakamani.
  “Juzi serikali imesema kuwa haiwezi kutoa kauli kwa vile jambo hilo lipo mahakamani,sasa imewezaje kuwafukuza
  madaktari wakati jambo lipo mahakamani?”
  alihoji Dk. Kigwang’ala.

  Aliitaka serikali kuondoa kesi hiyo ili kurejesha majadilianokwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo.

  Mbunge wa Ubungo, John
  Mnyika, alimshangaa Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwani ungeweza kujadiliwa bila kuingilia uhuruwa mahakama.

  Juzi uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili uliwafukuza kazi madaktari 229 walioko
  katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na mgomo unaoendelea wa kushinikiza kulipwa posho zao za mwezi mmoja.

  Hospitali zingine ambako
  madaktari wamefukuzwa
  kutokana na mgomo huo ni pamoja na Mbeya na Dodoma.

  Jeshi lachukua nafasi za
  madaktari, Wakati huo huo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),limeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali la kutoa huduma za kitabibu
  kwa wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini.

  Juzi Waziri Mkuu Mizengo
  Pinda akiwa bungeni alisema serikali imeamua kuwatumia madaktari waliopo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,wastaafu na hospitali zote za jeshi kuendelea kutoa huduma
  ya matibabu kwa wagonjwa.

  Msemaji wa JWTZ Kanali
  Kapambala Mgawe katika
  mahojiano maalum na gazeti hili, alisema juzi baada ya Waziri Mkuu Pinda kutoa agizo hilo, walianza utekelezaji wake ambapo kwa jiji la Dar es Salaam, hospitali Kuu ya
  Jeshi Lugalo Kikosi ya 521,
  Mgulani na ile ya Kikosi cha Navy-Kigamboni na hospitali zake zote kote nchini zilianza kutoa huduma hiyo bila
  vikwazo.

  “Kwanza naomba umma uelewe hivi hospitali za JWTZ hapa nchini kwa asilimia 70 zimekuwa zikiwatibu raia bila vikwazo vyovyote hivyo agizo
  hilo la serikali huenda likaongeza idadi ya wagonjwa kutibiwa katika hospitali zetu
  labda kwa asilimia 90.

  Mgawe alisema madaktari
  wanajeshi wapo kwa ajili ya kulinda taifa na watu wake,hivyo akawahakikishia wananchi wanaougua
  kutosita kwenda katika hospitali za jeshi hilo kutibiwa akidai kuwa hawaoni mantiki ya daktari kugoma.

  Chanzo:TANZANIA DAIMA
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Nafurahi sana kwamba hii serikali inazidi kujichimbia kaburi, Bil 200 kwanini zisitumike kutatua na kuboresha mazingira ya kazi?
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wamekwisha kabisa, tuwaombee fahamu zao zirudi. Kuliko kuboresha hali ya mazingira ya afya hapa, unachukua fedha na kuzitupa kwa madaktari ambao hawataweza hata kuwasiliana na wananchi wako. Bado siamini kama wamefiki kiwango kidogo hivyo cha kufikiri. Siuamini huu uzi.
   
 4. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  This will be a long nasty war.
   
 5. Imany John

  Imany John Verified User

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Chanzo hujakiona?
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,261
  Likes Received: 19,389
  Trophy Points: 280
  pesa zipo
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,943
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  upuuzi tu! Watawalipa sh ngapi? Watakaa kwa muda gani? Wakalimani wangapi watawaajiri? Wataishi wapi? The Govt is putting the cart before the horse. The nation's think tank is perforated! Wapuuzi kweli hawa!
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  Kumbe wana pesa?
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  nakumbuka zanzibar waliwahi kukodi majaji toka nigeria!tumezoea majibu rahisi rahisi toka serikalini
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Umelijua leo? Tatizo ni kukosa busara katika mipango na matumizi ya hizi pesa!!!!!!!!!
   
 11. Imany John

  Imany John Verified User

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Walimu wakigoma tutawaleta wengine from CHINA.
   
 12. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,338
  Trophy Points: 280
  Natamani hao madaktari wakishakuja manesi na wauguzi wengine wagome ili serikali ituletee manesi wa cuba, india na nchi rafiki! Haahaha serikali dhaifu, Cabinet dhaifu, rais dhaifu na maamuzi yao dhaifu! Utashangaa hao madokta wa kutoka nje watalipwa kwa dollar what a shame.
   
 13. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Wajinga ndio waliwao. We acha tu, yatawashinda.
   
 14. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Huu ni muujiza unapendekezwa! Madaktari wa kigeni wengi ya kutosha kuziba pengo la wanaogoma!

  Ki hali halisi ni kwamba wagonjwa wetu wataendelea kuumia/kufa hadi suluhisho la kweli na madaktari wetu wenyewe litakapopatikana.
   
 15. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Huyu dhaifu kweli hana akili kabisa yaani atawawa kikatili hadi atajuta na ataenda kutupwa motoni kwa jinsi anavyowatesa watz, jamani tufunge na kuomba Mungu hayuko mbali nasi time will tell soon
   
 16. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,417
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 180
  Na walimu wanagoma watakodishwa wa kuziba pengo?hapa ni kuwa serekali sikivu ya dhaifu jk inahairisha matatizo badala ya kutatua,is so sad.kuliko kukodi bora wangewapa na urai.
   
 17. P

  Pulpitis Senior Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unategemea nini baraza la mawaziri likiongozwa na Mr Liwalo na liwe likimshauri Mr Dhaifu? Ndio matokeo yake haya.Alafu baadaye ooh nilishauliwa vibaya Mpango ukikwama.nawasubiri kwa Hamu kuona dr wa kichina, na indians akimuhoji mswahili vizuri na kumtibu malaria katika mazingira haya ya vifaa duni.
   
 18. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Liwalo na Liwe
   
 19. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Sasa wanaleta madaktari kutoka nje waje kutumia hivi vifaa scraper au wanaleta na vifaa vipya?Manaake hivi vifaa vyetu za kuungaunga hawajazoea ndio watashindwa kufanya kazi kabisa.
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu edit basi thread haija kaa vizuri.........
   
Loading...