SERIKALI yanyang'anya ukumbi wa STARLIGHT ambao ulikwishalipiwa na MADAKTARI

Hivi TUCTA na Walimu,waaguzi wapo wapi wenzao wanapokandamizwa namna hii...jamani,yaani nimemuona waziri mkuu akiongea kwa hasira ile mbaya.
 
Pinda amesahau kufunga ukumbi mmoja ambao ndo unatumika kuliko hiyo ya Starlight na DonBosco. unaitwa eHALL. Hivi sasa mikutano sio lazima mkutano physically. simu zatosha sana kuwa ukumbi wa mkutano.
 
PM Pinda amesema mikutano ya maDr isiyo na tija ni marufuku kuanzia kesho. So hamna vya Starlight wala Bon Dosco. Kwa kifupi serikali imeamuru Hamna Mikutano ya Madaktari. Warudi kazini na mazungumzo yatapangwa baina ya Serikali na Viongozi wa Madaktari.
Ni kweli inatakiwa serikali iongee na wawakilishi wa madaktari siyo kuongea na kundi looote la madaktari!
 
Yaani Serikali yetu ina watu wasio na akili timamu ,inafanya mambo kitoto sana pasipo kufikilia

Kwa hiyo hapo inamkomoa nani?
 
Hatetewi CCM hapa, hivi kumuweka Waziri Mkuu awangoje halafu wasitokee, wana kiburi aina gani? ikiwa wanaweza kumfanyia hivi waziri mkuu, hao wagonjwa inakuwaje?
Kwani wewe Faiza Foxy waziri mkuu ni kitu gani au ni nani hata awe na dharau,au hata atetemekewe?hapa hakuna kujipendekeza,taarifa ya maandishi aliwapelekea hao ma-Drs ilipelekwa wakiwa wamesha sambaa na tayari walishakubaliana kukutana Monday,sasa leo kaenda kufanyaje leo?
 
Issue ya madaktari iangaliwe katika mitizamo miwili, tunahitaji madaktari kuokoa maisha ya wagonjwa wetu na pili wanatakiwa kusikilizwa kuhusu madai yao. Pinda yuko sahihi kuwaambia warudi sehemu zao za kazi na matatizo yao yatafanyiwa kazi kupitia viongozi wao, sasa madaktari wanatakiwa kusikiliza kiongozi wao anasema nini! Kama kiongozi anakubaliana na serikali na wamewekeana muda wa kutatua hili tatizo, kama halitafanyiwa kazi hapo wanaweza kuendeleza mgomo. Sidhani kama ni busara wazidi kushinikiza serikali ili hali wagonjwa wanakosa tiba hata kufariki. Kama Pinda ametoa vitisho kweli basi hatakuwa na busara hata kidogo katika kutatua matatizo, na kuweka FFU siyo sahihi kama watakuwa wanajadiliana kuhusu yaliyotokea leo au kumsikiliza kiongozi siyo tatizo. Uchumi wa nchi uko vibaya na serikali haina hela, yote haya si waziri mkuu au raisi kusema walipwe sijui 3.5m hii inatakiwa wizara muhimu kama utumishi, fedha, afya, hazina sikae chini na kuona kama revenues, government spending zitakuwa sustainable... wanaosema raisi anatumia milioni 300 kwa safari madaktari wangepewa, leo wakipewa mwezi kesho zitatoka wapi? ya wabunge si issue ya leo walishakaa chini na wakajua hela itatoka wapi. UCHUMI MBAYA NA SERIKALI HAINA HELA, mambo yakiendelea hivi tutaingia kwenye hatua ambayo hata hao wanaolipwa kidogo hawatapa. Mungu ibariki Tanzania.
 
Hiyo mikutano yao kwa sasa ni haramu, imeshapigwa marufuku na Serikali, Ilikuwa wakutane na Waziri Mkuu leo, kilichowafaya wasiende ni nini?

Drs are not cheap like how think madame! hivyo vitisho walizoea kuwapa watu wa kada nyingine, doctors ni watu wanao kutana na mambo ya kutisha zaidi ya hayo ya kufukuzwa kazi. Busara ndogo sna inahitajika kuutatua huu mgogoro, Pinda uwezo wake ni mdogo hili swala nadhani liko juu ya uwezo wake, wasipo angalia atalia machozi
 
Blandina Nyoni kawingiza choo cha kike!! Walichelewesha posho za Intern,wakawafanyia ujeuri sasa ufa unaangusha ukuta,c.h.u.p.i zinawabana manyapara wa CCM!!
 
hata unachokisema hujui, aliyedharau ni nani? Wakati waziri mkuu ndiye aliyengoja?

Hapo tumeridhiswa kuwa si serikali ambayo haisikilizi ni hao vibaraka wachache wanaotaka kuvuruga amani ya nchi, na hao madaktari ni vikaragosi vinavyotumiwa na wajanja wachache kwa ujuha wao wa kuahidiwa hewa.
i hate you with passion!
 
Hakuna kazi isiyo na sulubu zake, ndio maana inaitwa kazi. Wao ndio kazi yao na wewe unaweza kuwa unaona ya kutisha wao wanaona ni kawaida tu.

Lakini hili la kufanya dharau kwa Serikali, hatuliungi mkono hata kidogo, wangekwenda kusikiliza kama hawajaridhika wangesema hilo hapana, ndio mambo yanavyokwenda, sio kususa, wanasusa nini? hawajajifunza kutoka kwa wasusaji wakuu walipoamuwa kususuka?

Ustaadhi Gadaffi alikuwa hivi hivi na ubabe wake yuko wapi leo?
 
Sasa wamezidi. Inaboa bana. Kama hawataki waishie. Tunakufa huku.
 
Kuzuia mkutano ni sawa na sifuri ,madaktari can organize a chart session on the web na kuendelea na mkutano in the virtual space. Serekali hii dizzy kweli.
 
this time wachezea wanaume, madaktari sio walimu, wanaowagawa kwa laki saba na kozi za muda mfupi

Wakiruka kiunzi hiki watumishi wa nchi hii watakuwa wamekombolewa na dhuruma,nitashangaa kama hawakuwa na second plan!hili lilikuwa wazi la kuwazuia kukutana na humu tuliandika sana,nachojua kwa sasa hawahitaji mikutano zaidi ya taarifa,na kufikisha taarifa ni rahisi tu,madaktari walio wengi wana lap top,watumie mitandao kuwasiliana wakilazimisha mikutano watawapa sifa hao maaskari , wakae majumbani na hata wale madaktari waliokuwa wanawaacha kwenye emergence unit waondoke na tusikie jinsi wazee wa posho watakavyowajadili kesho kutwa,lakini mwisho madaktari watashinda tu,suala la kupeleka jeshi ni kichekesho kwani hapo kwao tu hawatoshi na manesi wajiunge kwa huu mgomo sasa.
 
Madaktari ninafungua ukurasa wa Facebook tuwasiliane huko kwa mikakati! Labda mtoto wa mkulima atazuia hata internet access
 
pinda anataka kutuua sie maskini...mbona kati anayotaja yako madai mazuri sasa anakwama nini kuyatekeleza!
 
Pinda ukizidiwa usiku hutakimbizwa India, utakwenda Muhimbili kwanza, nakuhakikishia safari ya India utaisikia ahera. Sindano moja tu ya insulin inakutosha, Mapambano yanaendelea.
Hawa viongozi wetu wana short sight sana....wanasahau kuwa hata wao wanaugua(pinda tunamjua mgonjwa) na watahudumiwa na hawa hawa madaktari...hata kama viongozi watawakwepa madaktari muhimbili wakiugua lakini watakutana nao kokote private watakapoenda....watawakuta hawahawa madaktari.....if they force doctors to go back to work with their problems unsolved...then they should expect the worse.....and more importantly...an increased mortality rate due to negligence.......
Serikali wana play politics (kama walivyozoea)kwenye very serious issue ambapo peoples' lives are at stake....

Rai yangu kwa madaktari:
Kesho kusanyikeni kwenye open space....(e.g viwanja vya jangwani)ili mfanye mkutano wa kimkakati..........this is very crucial at this point....for the sake of unity among you.......
 
hiyo mikutano yao kwa sasa ni haramu, imeshapigwa marufuku na serikali, ilikuwa wakutane na waziri mkuu leo, kilichowafaya wasiende ni nini?

waliogopa wanaweza kumliza...mpokea posho za jairo 280000/-
 
Back
Top Bottom