Serikali yangu: Tanzania itakuwa na mabilionea wa kisiasa au kiuchumi?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,382
1,247
Serikali yangu, Salaam!
Dhamira yenu kuhusu katika utawala wenu kuongeza mabilionea wapya ni nzuri, endelevu, zenye baraka. Lakini huenda dhamira na nia zenu zisilete matokeo chanya pale tutakapojilinganisha au kulinganishwa na nchi majirani zetu.

Nimeandika haya ili tujitathmini na kuwa na njia sahihi - nimeona sehemu maelezo ya Boniface Ndego (Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mara akisema kwamba Jana trh 19/Dec/2020 ktk Ukumbi wa Golden Tulip, Wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya TCCIA Taifa (NEC) ambacho alipata fursa ya Kuhudhuria, kuwa alipata Mshtuko (Shock) Rais wa TCCIA Bw. Paul Koyi alipoeleza Fursa za AfDB.

Rais wa Chemba alitoa taarifa kwamba kila Mwaka AfDB hutenga kati $400mil na $700mil kwa Kila nchi Kwa ajili ya Mikopo ya Makampuni ya Sekta Binafsi. Kwa Africa Mashariki Rais wa Chemba alisema Maombi Kutoka Uganda yalikuwa karibu 300 na Maombi kutoka Kenya yalifika karibu 600, lakini Maombi Kutoka Tanzania yalikuwa 8 tu na kwamba kila Mwaka Fedha zinazotengwa kwa ajili ya Makampuni ya Tanzania huwa zinabaki bila kutumika

Taarifa hii inaleta Maswali mengi sana. tujiulize tatizo Ni nini? Kwamba nchini hatuna makampuni yenye uhitaji wa mitaji Kwamba mamlaka husika hazijui fursa hizo Kwa wahusika hawatoi taarifa ya fursa hizo kwa viongozi wa Serikali yetu

Nachofahamu Tuna Changamoto kubwa ktk eneo hili la mitaji! Mazingira ya kupata mitaji kuwezesha Ubunifu, kukuza biashara ni tatizo kubwa sana kumbe kuna fursa zinakuja na zinapotea kwasababu hazikutumika. Nadhani kuna mahali Sekta binafsi na Serikali hatujajipanga! Kuna mahali mifumo yetu ya biashara haijakaa sawa. Kuna mahali watu tuliopewa dhamana kwajili ya Sekta binafsi hatujafanya kazi yetu sawasawa. Kuna mahali kanuni tunazozitumia zina kasoro.

Naliona Tatizo kubwa Linaweza kuwa ni Kukosekana kwa Malengo ya Pamoja Kila mtu anajitahidi kushindana na Mwenzake, Serikali inashindana na Sekta Binafsi. viongozi Wanashindana na Wananchi, na Mjasiriamali anashindana na Mjasiriamali mwenzake, hatuna Malengo ya Pamoja.

Rai yangu:
Baada ya kupitia maandishi hayo nashauri -
(i). Serikali inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli iziratibu na kuzifuatilia kwa karibu idara zinazoshughulikia maendeleo ya sekta binafsi,

(ii). Kama tunavyoweka nguvu ktk elimu ya uchaguzi, unyunyiziaji, Sensa, Ukimwi basi hata hili la maendeleo ya sekta binafsi lipewe kipaumbele - wahusika wafanye kazi hiyo ya kutangaza AFDB;

(iii). Watanzania waache woga wa kushindana, kujitokeza na kuomba fursa hizo.
Vinginevyo si vizuri sekta binafsi iendelee kisiasa badala ya kuendelea kiuchumi.

Imewasilishwa na
Msakila M Kabende
Economist
Kakonko - Kigoma
21 Desemba 2020
 
Kuwa makini

Ohoooo utaporwa zote pesa ulizokopa huko zikitua tu kwenye ardhi ya wana wa zakayo aka watoza ushuru

Wewe unadhani watu hawataki hizo pesa,wanazitaka lakini utaandaliwa charge sheet

Unaongoza Criminal rocket,Marijuana Gang,Ciggaratte Gang,Bangi Gang,Robbery Gang

Utaandaliwa watoto na mke Bandia kuwa hujawatunza kwa miaka 40 hivyo pesa zote unaporwa wewe unabaki na deni la kulipa huko AfDB

Utapigwa kodi na naniliiii ile,Halafu na mkopo utaendelea kulipa huko African development Bank

Soma nyakati na mazingira ,Kuna wazee wakichungulia tu kuwa mzigo umeingia unafunguliwa mashtaka halafu mzigo wote wanakomba wewe unabaki na deni na pressure

Utachukua huo mkopo halafu ukifika kwenye akaunti yako kitakachokupata kutoka kwa wana wa zakayo hutasahu utaambiwa unaendesha genge la uhalifu,utakatishaji na uhujumu uchumi halafu utaambiwa ulikuwa hulipi kodi tangu mwaka 1945 yaani wakati wa vita ya pili ya dunia mpaka mwaka 2020

Kiasi chote watakomba cha mkopo uliokopa halafu watakusamehe ukafe na presha

Sio kwamba watu hawapendi jifunze toka kwa Mr Hen, Mr Kaflag yaliyowakuta
 
Back
Top Bottom