Serikali yangu kama kweli ina nia ya dhati toka rohoni, zuia ufujaji pesa za umma usio na ulazima fanya hivi:-

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,460
2,000
Ili mbunge au diwani au kiongozi yeyote wa kuchaguliwa na wananchi aweze kujiudhuru basi kujiudhuru kwake lazima kupitishwe na kamati maalum ya jimbo husika ambayo nashauri ingeundwa kutoka kwa wawakilishi wa kila kata yaan madiwani na wenye viti wa vijiji hasa baada ya kuridhishwa na sababu zake za kutaka kujiudhuru ubunge

maana kuchaguliwa anachaguliwa na wananchi halafu kujiudhuru akijisikia tu yeye binafsi kwa sababu zake na matakwa yake tena mengine ya hovyo na wakati wowote anajiudhuru

hapana nadhani hapo ni mwananchi ambaye ni mpiga kura ndiye anaye jeruhiwa na kunyonywa maana alipoteza wakati wake kumchagua na pengine alijeruhika pia na pesa zilizo tumika katika uchaguzi ni kodi anazokamuliwa tena mwananchi huyo huyo nadhani ni basi tu nchi ina bora viongozi na sio viongozi bora na wenye uchungu wa kweli na taifa ,

Hali kadhalika na diwani naye lazima kamati za kata zikihusisha wenyeviti wote wa vijiji na vitongoji wakae wajadili na kukubaliana na sababu za diwani huyo kujiudhuru hapo ndipo ajiudhuru na gharama zoote za kuitisha vikao hivuo vya kamati agharamie mwenyewe

Na baada yapo mbunge huyo au diwani huyo anapoteza sifa za kugombe tena nafasi hiyo kwa mda wa miaka mitano.

Nadhani hiyo ingepunguza ujinga ujinga unao endelea ambao kuna wapumbavu wachache wana ushabikia wakidhani ni ujanja kumbe tuna zidi kurudisha nyuma taifa kiuchumi na kisiasa maana pesa ambayo itaitisha tena uchaguzi huenda ingejaza hata mafuta kwenyw safari za rais na msafara wake tungekuwa tume save kiasi kwa matumiz mengine ya msingi

Hii ina maana kwamba kuanzia nyalandu na kundi lote linalo endeleza ushenzi huo usio na huruma na pesa za taifa hili na mda wa wapiga kura.

HII HAIHUSU ANAENDA CHAMA GANI AU KUTOKA CHAMA GANI AU SABABU ZOZOTE ZILE BALI MWANANCHI NDIYE ANAYE DHURUMIWA HAKI YAKE, MDA WAKE NA JASHO LAKE KWA UZEMBE NA UJINGA WA MTU MMOJA AU WAWILI KWA AMATAKWA YAO YANAYO LITIA HASARA TAIFA NA KUUMIZA WANANCHI.
 
Itoye

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
464
1,000
Mkuu, kwa hili sheria ibadilishwe tu, yeye akijiuzuru au akifukuzwa au akifariki nafasi ibaki ya chama kwa hiyo iwe no jukumu la chama kuleta jina la mtu mwingine, akikidhi vigezo anakula kiapo maisha yanaendelea kama Zimbabwe.
 
Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
6,139
2,000
Ulichokisema ni sahihi kwa kweli, yaani watu wamekuamini wamejipanga kukupigia kura halafu eti unajiuzulu bila kuangalia wananchi wako watachukuliaje maamuzi yako.
 
Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,460
2,000
Ulichokisema ni sahihi kwa kweli, yaani watu wamekuamini wamejipanga kukupigia kura halafu eti unajiuzulu bila kuangalia wananchi wako watachukuliaje maamuzi yako.
Kuna wajinga wachache wanafurahia sana ushenzi huu na kudhan ni ujanja na ni aina mpya ya siasa wameibuni lakin wananchi inatuumiza sana nime tembelea baadhi ya sehemu na kujadiliana na wananchi kuhusu hili kwakweli inaonekana wamekata tamaa kabisa ya kupiga kura wanakerwa na tabia hii iwe serikali inahusika ama ni hiyari ya mtuu lakin wananchi wengi limewakera hili fanya research hata hapo ulipo.

Nadhani ndio maana unakuta kituo kimeandikisha wapiga kura 100000 wanao jitokeza kupiga kura 1700 , wamekata taamaa ila hawana pa kuelezea hisia zao.
 
popoma

JF-Expert Member
May 5, 2017
2,382
2,000
CCM wanasema adui wao mkuu in CDM ila watanzania wanasema adui yao in CCM kwa hiyo mkuu usitarajie jipya kutoka kwa mafisiemu
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,022
2,000
CCM wanasema adui wao mkuu in CDM ila watanzania wanasema adui yao in CCM kwa hiyo mkuu usitarajie jipya kutoka kwa mafisiemu
Njaa ya upinzani ni Neema kwa kijani,mbinu mpya ya kamati ya ufundi baada ya kushindwa siasa za kisera za majukwani hio ni mbinu mbadala.
 
Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
6,139
2,000
kwakweli inaonekana wamekata tamaa kabisa ya kupiga kura wanakerwa na tabia hii iwe serikali inahusika ama ni hiyari ya mtuu lakin wananchi wengi limewakera hili fanya research hata hapo ulipo.
.
Na hili ndilo nilikuwa nalifikiria wakati naandika bandiko langu hapo juu.

Kama mambo yataendelea hivi baadhi ya watu makini wanaojali maslahi mapana watavunjika moyo wa kupiga kura. Matokeo yake tutabaki na wapiga kura wasiofuatilia hata ajenda za wagombea (watu wa mihemeko), hatimaye tutachaguliwa watawala wasio juwa hata wanakwenda kufanya nini kwenye majimbo. Mwakilishi aliyechanguliwa na kuacha bila ya sababu ya msingi ni msaliti kwa wapiga kura wake.
 
kichakaa man

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
3,430
2,000
Pia mbinu nyingine iwepo sheria inayomtaka mtu anayehitaji kujiuzuru atalipia gharama za uchaguzi wa marudio au akijiuzuru nafasi Yake apewe yule aliyekuwa anamfuatia kwa kura kipind cha uchaguzi . ili kuepuka gharama.
 
Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,867
2,000
Haya mapendekezo Mbona hutukuyaona wakati Nyalandu ana kwenda chadema?
Mnajua maana ya demokrasia? Wanacho kifanya wabunge hao ndio demokrasia yenyewe ambayo huwa mnaililia kila leo sasa wao wanaoitimiza.
Demokrasia ina gharama na gharama zake ndio hizo na wala hakuna axcuse kwenye kugharamia demokrasia.....
Inashangaza watu wanao amini kwenye chama cha demokrasia lakini wanaogopa demokrasia na gharama zake.
 
gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,695

Mapendekezo yanatolewa wakat wowote.haimaanishi kwa vile jana hayakusemwa leo yasisemwe.Na kwa nyalandu ilionekana swala lisingeendelea ila sasa imeonekana ni fasheni ndo maana watu wenye akili wanatoa mawazo yao maana kama Taifa tusipokua na taratibu sahihi zakudhibit wanasiasa na vyama vyao watakaokua wanaumia ni wananchi wa kawaida.sasa kwa hali hiyo iyo sio democrasia ni ujinga.
 
Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,460
2,000
Haya mapendekezo Mbona hutukuyaona wakati Nyalandu ana kwenda chadema?
Mnajua maana ya demokrasia? Wanacho kifanya wabunge hao ndio demokrasia yenyewe ambayo huwa mnaililia kila leo sasa wao wanaoitimiza.
Demokrasia ina gharama na gharama zake ndio hizo na wala hakuna axcuse kwenye kugharamia demokrasia.....
Inashangaza watu wanao amini kwenye chama cha demokrasia lakini wanaogopa demokrasia na gharama zake.
Ukiwa mjinga huwezi ona hasara ila kama una akili utawaweka kundi moja nyalandu na kundi lake wote
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom