Serikali Yamwaga Sh1.7 bilioni Kwa wakazi wa Tabata Dampo....

Makange

Member
Jul 27, 2007
27
1
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Stephen Wasira, akizungumza na waandishi wa habari alipotoa ripoti ya uchunguzi na maamuzi ya serikali kuhusu wakazi wa eneo la Tabata Dampo lililovunjwa mwezi uliopita.Serikali imeamua kuwalipa wamiliki wa nyumba 80 zilizovunjwa kila mmoja sh milioni 20 na viwanja bure.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Kandoro.Akisoma Tamko la Serikali jijini Dar es Salaam jana kufuatia matokeo ya Tume Maalumu ya Kuchunguza Ubomoaji wa Nyumba hizo,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Stephen Wassira, alisema uamuzi huo wa serikali unatokana na kubaini kwamba ubomoaji huo haukuzingatia uamuzi wa Baraza la Ardhi.

Akifafanua kuhusu hilo, Wassira alitaja taratibu hizo ambazo zilipaswa kuzingatiwa kwamba ni kufikisha dhamira hiyo ya ubomoaji kwanza katika vikao vya juu vya timu ya menejimenti na vikao vya Baraza la Madiwani.Wassira aliongeza kwamba, taratibu nyingine zilizokiukwa, ni wananchi kutoshirikishwa katika azma ya ubomoaji huo kitu ambacho ni kinyume cha misingi na kanuni za utawala bora huku kukiwa na harufu ya rushwa.

Source: http://haki-hakingowi.blogspot.com/2008/04/serikali-yamwaga-sh1.html
 
Kandoro tunashukuru kwa kulifikisha jambo hili hapa lilipofikia lakini sio upuuzi uliokua ukiletwa na makamb' eti wananchi wahame kabla hawajapa kifuta jasho.

Lakini hizo milioni 20 mbona hawajafafanua,hayo mahesabu yamepigwaje jamani?Nasema hivyo kwa sababu nyumba zilitofautiana ubora sasa hapa mbona naona kama imekaa vibaya.Hawa waathirika wa Tabata kwa muono wangu waliku wanastaili kulipwa malipo ya aina mbili ni kiwa na maana kwamba (i)Malipo ya usumbufu walioupata baada ya kubomelewa nyumba zao(ii)Fidia ya nyumba zao kulingana na thamani ya nyumba yenyewe.

Lakini maelezo ya Wasira yamepwaya kidogo,mbona hajatuambia mpaka lini waathirika wetu watakua wamepata hizo pesa zao jamani.Na hili fungu la kuwalipa hao watu limetoka wapi?

Lakini kwenu nyie wanaharakati wa haki za binadamu,hivi hawa watu ambao kwa tamaa zao wenyewe na ubinafsi wao wameisababishia serikali hasara ya sh.1.7 billion kwanini wasinyongwe hadharani jamani.Hizi pesa zingetosha kabisa kununua vyandarua kwa hospitali zote za TZ bila kumsubiri Bush.Mimi huyu mkurugenzi na washirika wake ningewanyonga tu watake wasitake.Huu ni ushenzi.Mnaopewa madaraka msilewe madaraka haya ni mambo ya kupita tena msisahau kwamba cheo ni dhamana.
 
Hapa ndo huwa nachoka na uongozi wa serikali yetu ya TZ.Ina maana huyu Wassira na Kandoro hawakuwa na taarifa,wameshitukizwa na vyombo vya habari?
Hawa wote ni Manju,wanatunga nyimbo tu ili wapofushe fikra za waathirika wa bomoabomoa.

Hawa wanazima moto,haiwezekani Waziri mkuu,waziri wa TAMISEMI na Mkuu wa mkoa kitendeke kitu ktk eneo la utawala wasijue na kumtoa kafara Mkurugenzi wa manispaa ya ilala John Lubuva
Hii ni propaganda,Neno moja la ukweli ila matano ya uongo.
 
Are we paying these milions because of sloppy actions and negligency of few people, and Governments takes the credit! Na sisi tunajiita watu kweli, huku tunaibiwa kila siku na tunacheka!!!!!! au ndio madili ya watu tena!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom