Serikali Yamwaga neema sekta ya Madini

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019
Serikali imenunua mtambo mkubwa wa madini ambao utasaidia kufanya utafiti wa madini, sambamba na kuwasaidia wachimbaji wadogo katika shughuli za madini nchini

Akizungumza Bungeni leo jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kwa lengo kuunga mkono wachimbaji wadogo nchini kote wakiwemo wachimbaji wa kijiji cha Busiri wilaya ya Biharamulo.

Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa ili kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini, Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imenunua mtambo mkubwa wa kumsaidia kufanya utafiti wa kina kwa kuchoronga miamba kwa bei nafuu ili kubaini mashapo zaidi na kuongeza uzalishaji.

Naibu Waziri, Nyongo aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa wachimbaji wadogo ili wanufaike zaidi na kazi ya uchimbaji.

Wizara kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini inakamilisha uandaaji wa kitabu cha madini yapatikanayo Tanzania toleo la nne ambacho kitaonesha uwepo wa madini katika mikoa, wilaya na vijiji, ambapo kitasaidia wachimbaji wadogo kutambua madini yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na matumizi ya madini hayo.

Aidha, Wizara kupitia Mradi wa Usimamizi endelevu wa Raslimali Madini (SMMRP), inakamilisha kujenga vituo vya umahiri katika wilaya ya Bukoba, Bariadi, Songea, Handeni, Musoma, Mpanda na Chunya ili kuwezesha wachimbaji wadogo kujifunza kwa vitendo.
 
Ingependeza kama Serekali ingewashauri wachimbaji wadogo wadogo wakaunda makampuni ya madini wakauziana hisa,wakapewa mitambo,majengo n.k wakafanya kazi kwa ufanisi na kwa tija zaidi hii wanachofanya sasa aitoleta tija kwa wachimbaji wala taifa
 
mawazo mazuri kabisa
 
Wewe utakukuwa geo unaelewa alafu unavunjika mbavu kwa kicheko
 
Ingependeza kama Serekali ingewashauri wachimbaji wadogo wadogo wakaunda makampuni ya madini wakauziana hisa,wakapewa mitambo,majengo n.k wakafanya kazi kwa ufanisi na kwa tija zaidi hii wanachofanya sasa aitoleta tija kwa wachimbaji wala taifa
Wakianzisha ushirika na kupata hela, aminia kiongozi wao hatakuwa mchimbaji mdogo tena.
Yataanza mambo ya bongo movie na uongozi shupavu wa yule sijui anaitwaje
 
Ndo maana kuna Dar es salaam stock exchange...Dunia imebadirika mno kwa sasa....ata Barick,Williams diamond,Ashanti Gold zinamilikiwa na watu walionunua na wanaoununua hisa kila kukicha..tunatakiwa kuacha mawazo mgando na uswahili uliotujaa...so badilika kifikra hii ni karne ya 21 na ukuta wa Berlin umeshabomolewa aupo .Hii Picha Malkia wa UK anakagua akiba ya dhahabu yetu toka Tanzania walizochota wakati wa ukoloni ambazo ndo zinawapa kibri mpaka leo...UK awana ata mgodi wa chumvi walituwai na wanatesa kwa mali zetu.
_64743346_016736105-1.jpg
 
Hahaaa hizo story zao kila siku fiksifiksi tupu uani mawazi,na mwenyekiti wao wa chama.
Stamico haina hata mia ripoti ya CAG imesema stamico imefilisika sasa hao mtambo wamenunua kwa mapato ya chattle au lumumba
Serikali imenunua mtambo mkubwa wa madini ambao utasaidia kufanya utafiti wa madini, sambamba na kuwasaidia wachimbaji wadogo katika shughuli za madini nchini

Akizungumza Bungeni leo jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kwa lengo kuunga mkono wachimbaji wadogo nchini kote wakiwemo wachimbaji wa kijiji cha Busiri wilaya ya Biharamulo.

Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa ili kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini, Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imenunua mtambo mkubwa wa kumsaidia kufanya utafiti wa kina kwa kuchoronga miamba kwa bei nafuu ili kubaini mashapo zaidi na kuongeza uzalishaji.

Naibu Waziri, Nyongo aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa wachimbaji wadogo ili wanufaike zaidi na kazi ya uchimbaji.

Wizara kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini inakamilisha uandaaji wa kitabu cha madini yapatikanayo Tanzania toleo la nne ambacho kitaonesha uwepo wa madini katika mikoa, wilaya na vijiji, ambapo kitasaidia wachimbaji wadogo kutambua madini yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na matumizi ya madini hayo.

Aidha, Wizara kupitia Mradi wa Usimamizi endelevu wa Raslimali Madini (SMMRP), inakamilisha kujenga vituo vya umahiri katika wilaya ya Bukoba, Bariadi, Songea, Handeni, Musoma, Mpanda na Chunya ili kuwezesha wachimbaji wadogo kujifunza kwa vitendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

Nawahakikishieni, hakuna faida yoyote itakayopatikana kwa kununua drill rig halafu ukaiita kuwa ni mtambo wa kutambua madini, jambo ambalo ni uwongo mkubwa.

Sijui ni nani aliyewadanganya. Kwanza STAMICO haina wataalam wa kufanya utafiti wa madini zaidi ya wataalam wababaishaji wa nadharia. STAMICO haijawahi kugundua deposit yoyote, hawana uwezo wa kugundua, na hawatagundua.
 
Back
Top Bottom